Kuna watu wengi sana wanambeza mh. Raisi. Lakini kiukweli anahaki ya kuwatetea wakulima. Mkulima auze korosho zake kwa 3000 halafu huku ulaya tununue madukani 25000 kwa kilo. Hilo ni kwa sababu ya hawa walanguzi wa middleman. Najua kwamba zinapitia process nyingi hadi zifikie hapo madukani lakini kwa hiyo bei ya 3000 hadi 25000 ni kubwa sana.
Kuna kipindi chai tv kilicho tayarishwa na Mama mmoja mwingereza. Alifuatilia zao la cocos linalo l
Imwa huko West Afrika. Ameonyesha jinsi linavyo limwa hilo zao na ni watu wa Aina gani ni wa rika gani na wanauza bei gani, na akafuatilia hao ma middleman, wengi wao ni wahindi, jinsi wanavyo nunua na wanavyo minya bei ili wao wapate faida kubwa zaidi. Yaani inatia huruma sana.
Kwahiyo ili kuwasaidia wakulima inatakiwa serikali iingilie Kati na ikiwezekana wanunue hayo mazao.
Huku ulaya kuna kitu kilianzishwa kinaitwa FAIR TRADE.. hilo linahusu jinsi ya kumsaidia mkulima. Yaani ukinunua bidhaa za fair trade utakua umemsaidia mkulima. Yaani bidhaa zao zinahusiana direct na mkulima, ni hao wakulima wanao fanya kazi zao kwenye mazingira mazuri bila kuwahusisha watoto. Na wanalipwa vizuri.