Magufuli kwa ukali: " Wewe RM yaani unazidiwa kuamua na mwandishi wa habari Msigwa, kweli?!

Magufuli kwa ukali: " Wewe RM yaani unazidiwa kuamua na mwandishi wa habari Msigwa, kweli?!

Suzy Elias

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2021
Posts
1,067
Reaction score
6,200
Kisa kingine cha kweli acha niwashirikishe kuhusu JPM kipindi alipokuwa W UJ.

Kama sikosei ilikuwa mwaka 2013 kipindi hicho miradi miwili ya barabara kuanzia Songea mjini hadi Namtumbo na Likuyu hadi Mbinga ilikuwa inatekelezwa kwa ufadhili wa MCC.

Songea - Namtumbo Mkandarasi wake ilikuwa Kampuni ya Wafaransa iliyoitwa Sogea Satom na Likuyu - Mbinga Kandarasi wake ilikuwa Kampuni ya ki China iliyoitwa Sinohydro kama sikosei.

Sasa basi, kwenye mradi wa Songea - Namtumbo uliokuwa chini ya Wafaransa mwishoni aliletwa Mkenya mmoja kuwa msimamizi wa Kitengo cha Earthwork. Kwa mjibu wa wafanyakazi waliokuwa chini yake jamaa alikuwa na kiburi, jeuri na dharau ya kuwatweza Watanzania huku akiwatukana eti hawamuwezi kwa lolote!

Bwana ee, ghafla wafanyakazi wale wakaanzisha mgomo wa kumlalalmikia Mkenya yule ajabu Mamlaka kuanzia Mhandisi wa Tanroads mkoa hadi Idara ya kazi Mkoa walisimama upande wa kumtetea Mkenya.

Ikumbukwe kipindi hicho Gerson Msigwa alikuwa bado Mkuu wa TBC redio Kanda ya Kusini na baadhi ya wafanyakazi walikuwa na namba yake wakampigia ili aweze kuja atoe habari kuhusu jambo lile.

Kweli Gerson Msigwa alienda na alipotaka kufahamu ni kwa nini wafanyakazi wale wagome kutoka kwa yule Mkenya ndipo alipokumbana na nyondo kama zote kutoka kwake akimtisha hawezi kumfanya lolote.

Kama binadamu, Gerson Msigwa naye akafura kwa hasira akimkanya yule Mkenya aache dharau. Kitendo cha Gerson kumkanyq Mkenya bila kupepesa macho hakika kilimfurahisha sana JPM alipopenyezewa na mnyetishaji wake hali iliyompelekea kumpigia simu Meneja wa Tanroads Mkoa wa Ruvuma akimzodoa kushindwa kuchukua maamuzi kwa wakati hadi mwandishi wa habari aingilie kati.

Toka siku lile, JPM alimkubali sana Gerson Msigwa.

NB: Gerson ukiisoma hii habari natambua atacheka sana kwa sababu ilimfanya ajawe na hasira!
 
Back
Top Bottom