Elections 2015 Magufuli lugha za Kimataifa ni Kizungumkuti, wenye ufahamu tujadiliane


Huyo Lowassa ndio anaweza? Ana sifa gani za kumfanya amshushe Magufuli? Uwezo wa kuitumia lugha umetofautiana baina ya mtu na mtu, na kujua kiingereza sio kuwa na elimu. Kuna watu wengine kuandika kwao ni kuzuri zaidi kuliko kuzungumza. Na pia kuna wengi tu ambao wako empty vichwani lakini maneno ya mdomoni ya kiingereza hayako mbali.
 
Watetezi wa ccm kwa kweli mnakazi sana. Lichama limeshaoza hilo. Halisafishiki linatakiwa lizikwe tu.
 
Uso wa Nyoka nisome vizuri. Sijafagilia Kiingereza; nimezungumzia ufahamu wa lugha iliyotumika kufundishia ni wa lazima. Inaweza kuwa lugha yoyote!

Wewe ndio hujanielewa. Nilipoanza Nimesema kuielewa lugha ya kufundishia hakuwezi kuwa linked na kuielewa fani. Soma Nilichokiandika
 
Watetezi wa ccm kwa kweli mnakazi sana. Lichama limeshaoza hilo. Halisafishiki linatakiwa lizikwe tu.

Chadema na CCM kipi kilichooza? Watu hawaeleweki, maamuzi ya chama yanafanywa na Watu wawili na wote mnafuata bila kuhoji, hicho ni chama kweli?
 

mwanasayansi au ni mwalimu wa chemistry ebu jaribu kuwa mkwel kitaaluma jamaa ni mwalimu
 
Asipoakuwa makini hata UDSM watamnyang'anya hivyo vyeti vyao....maana anakitia aibu chuo kikuu!:thinking::thinking:
 
Magufuli ni Mwalimu kitaaluma. Wakati anafundisha somo la kemia alikuwa anafundisha kwa kiswahili?

FaizaFox njoo huku lile neno lako linahusika hapa
 

Excellent! You said it well bro! Big-up sana. #HapaKaziTu CHAGUA MAGUFULI.
 
Du! Kwa vipi? Kwa kutumia 'learning theories' zipi?

Kuwa na ueledi mkamilifu (expertise) wa lugha ni kuelewa kuizungumza, kuiandika, na kuisoma. Ukipungukiwa na kimojawapo, huwezi kutambulika kama muelewa wa lugha hiyo.
 
Excellent! You said it well bro! Big-up sana. #HapaKaziTu CHAGUA MAGUFULI.

Tuko pamoja Mkuu. Tatizo wengine wanakuja hapa kuleta posts wakiwa na uchungu wa talaka ndio maana ukiangalia posts nyingine zimejaa emotions zaidi kuliko logic. Mtu anashindwa kutuonyesha mazuri ya huyo candidate anaemtetea baada ya kutuletea video feki, sasa sijui tufanye nini. Huyo candidate wake nae ni Kilaza kabisa, haongei English ambacho ndicho kipengele muhimu cha mada hii pamoja na kusomea huko kilikotokea, halafu mtu kashupaa tu.
 
Asipoakuwa makini hata UDSM watamnyang'anya hivyo vyeti vyao....maana anakitia aibu chuo kikuu!:thinking::thinking:
Kwa akili hizi za kitumwa zilizojaa kasumba ya kikoloni kamwe hamuwezi "kumkomboa" mtanzania toka kwa mkoloni mweusi. Mkapa ataendelea "kuwatukana" kwa raha zake. Badilikeni, watanzania sio wajinga kama mnavyofikiria.
 
Reactions: SMU
"I am a politicians". "I dont want to take this time as saying so many political...."

"Simple and clear is only congregations to you.."
"To the University Korindor... , Co... Cor,.. Colimbia univeristy to the assistance we are getting to this hospt"..
Kuna haja hawa wasomi wa namna ya magufuli wangechunguzwa hizi PhD wanazipataje maana ni aibu...
 
Mhhhhh.... haya hapo chini...

 
Itakapofika wakati wa kubargain country's interests na first world ndipo utakapojua umuhimu wa kiingereza

Hapo ndipo akina Makamba wanapojidai ................... Naona safari za nje Makamba ndiye atakuwa msemaji mkuu wa Rais
 
"I am a politicians". "I dont want to take this time as saying so many political...."

Kuna haja hawa wasomi wa namna ya magufuli wangechunguzwa hizi PhD wanazipataje maana ni aibu...

PhD za sayansi hazihitaji ujue sana kiingereza labda phD ya sheria.

Pamoja na kwamba kutoongea kingereza kwa ufasaha haimaanishi kuwa kiongozi mbaya, hiyo ni dalili tosha kwamba mfumo wetu wa elimu una walakini, ikiwa mtu wa PhD bado hawezi kutunga sentensi fasaha ya Kiingereza.

Ila sasa kuna suala la Raisi kuongea huko UN, ambako Kiswahili bado hakijapitiswa kuwa lugha ya UN.

Yale yale ya Id Amin kumwambia Malkia wa Uingereza I must revenge this visit by inviting you to Uganda, na pia kiongozi wa Bunge letu mwaka jana akiwa kwenye kipidindi cha TV alipataja watazamaji kama "our lookers".
 
Reactions: SMU

huyu jamaa ana sili ya congo mixer ya kirundi cum hutus
lakini kazaliwa biharamulo,pia huongea kinyambo na kisukuma.
 
Asipoakuwa makini hata UDSM watamnyang'anya hivyo vyeti vyao....maana anakitia aibu chuo kikuu!:thinking::thinking:

Ukweli ni kuwa hapa Tz waliosoma sayansi hata walimu wa vyuo vikuu kiingereza ni shughuli.
Pia hata nyie mlioko humu jamii wengi wenu ndivyo ilivyo. Angalia wakati wa presentation, ni kizungumti. Sasa hili la nyani alioni kund.. inatoka wapi?
 
Ukweli ni kuwa hapa Tz waliosoma sayansi hata walimu wa vyuo vikuu kiingereza ni shughuli.
Pia hata nyie mlioko humu jamii wengi wenu ndivyo ilivyo. Angalia wakati wa presentation, ni kizungumti. ...
Wote hao wanagombea urais wa Tanzania? Hutajisikia fahari kumsikia Rais wa nchi yako akizungumza kwa ufasaha? Pamoja na mabaya yake, napenda sana namna Ben Mkapa anavyotuwakilisha inapokuja suala la kuzungumza (hasa kwa kimombo). Sasa huyu Magufuli atatufanya tuwe tunabadili channel....kukwepa aibu!

Lakini kulitizama kivingine, pengine litapunguza appetite ya Rais (kama atashinda) kuzurura hovyo nje ya nchi na hivyo kutupunguzia gharama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…