Elections 2015 Magufuli lugha za Kimataifa ni Kizungumkuti, wenye ufahamu tujadiliane

Elections 2015 Magufuli lugha za Kimataifa ni Kizungumkuti, wenye ufahamu tujadiliane

watu mamburula kweli. unatoa mifano ya china na japani kwani wao lugha zao za kujifunzia na mawasiliano official ya kiserikali ni kiingereza? China hawatumii lugha ya kiingerezaa katika shughuli zao sisi tunaitumia kila mahali tangu primary mpaka vyuo vikuu. Hivyo mtu mwenye phd kutoweza kutunga hata sentensi moja sahihi ya kiingereza sio sawa! halafu majukumu anayotaka kupewa yanamlazimu ajue hiyo lugha vizuri kwa sababu itamlazimu kuitumia mara nyingi kuliko alivyokuwa waziri. atakuwa anakutana na wa\geni wengi sana na inabiodi aweze kuwa na ciommunication skills nzuri!

Huyo Lowassa ndio anaweza? Ana sifa gani za kumfanya amshushe Magufuli? Uwezo wa kuitumia lugha umetofautiana baina ya mtu na mtu, na kujua kiingereza sio kuwa na elimu. Kuna watu wengine kuandika kwao ni kuzuri zaidi kuliko kuzungumza. Na pia kuna wengi tu ambao wako empty vichwani lakini maneno ya mdomoni ya kiingereza hayako mbali.
 
Nakushauri ushugulike kwanza na afya ya Lowassa maana kama Magufuli kunywa kile kikombe unalichukulia kama issue kubwa, kumbuka kile kiko na uhusiano wa karibu na swala la imani zaidi. Mimi si muumini wa hayo ila kama kwa Magufuli ambae ni Mlokole lilikuwa jambo ambalo aliona lingemsogeza karibu na anachokiamini, sioni sababu ya watu kutokwa na mishipa ya shingo wakati ukiangalia ni mgombea wao ndie anaehitaji msaada wao kipindi hiki.
Watetezi wa ccm kwa kweli mnakazi sana. Lichama limeshaoza hilo. Halisafishiki linatakiwa lizikwe tu.
 
Uso wa Nyoka nisome vizuri. Sijafagilia Kiingereza; nimezungumzia ufahamu wa lugha iliyotumika kufundishia ni wa lazima. Inaweza kuwa lugha yoyote!

Wewe ndio hujanielewa. Nilipoanza Nimesema kuielewa lugha ya kufundishia hakuwezi kuwa linked na kuielewa fani. Soma Nilichokiandika
 
Watetezi wa ccm kwa kweli mnakazi sana. Lichama limeshaoza hilo. Halisafishiki linatakiwa lizikwe tu.

Chadema na CCM kipi kilichooza? Watu hawaeleweki, maamuzi ya chama yanafanywa na Watu wawili na wote mnafuata bila kuhoji, hicho ni chama kweli?
 
Nyie "Wanasayansi" wa hapa Bongo akiwemo na huyo Magufuli mmefanya nini cha maana kulisaidia hili Taifa zaidi ya kukariri tu vilivyoandaliwa na wenzenu?Si ajabu hata practical part ya ulichokaririr hujawahi kufanya hata kwa majaribio. Mkijiita nyie ni "Wanasayansi" Walioko NASA watakuwa kina nani?

mwanasayansi au ni mwalimu wa chemistry ebu jaribu kuwa mkwel kitaaluma jamaa ni mwalimu
 
Asipoakuwa makini hata UDSM watamnyang'anya hivyo vyeti vyao....maana anakitia aibu chuo kikuu!:thinking::thinking:
 
Nimejaribu kufuatilia uwezo na uelewa na mwenzetu huyu katika arena za kimataifa ni zero na uwenda akafanya vituko kama vya ndugu Mulugo aliyekuwa naibu waziri wa elimu kuwa Tanzania ni muungano wa Tanganyika na Zimbabwe.

Hiyo ilitokana na kushindwa ngeli na kubaki kukariri tu.Upungufu huu wa exposure kimatiafa na lugha ni tatizo na dnio maana watu wasio na uwezo kama akina Makamba wanajitia kimbelembele kama wapiga zomari kwa makufuli huku wakinyendea nafsi kama washuri wake akibahatika kuwa raisi kama shetani atabariki.Mungu yupo upande wa Legwanani the Great.

Hivi kama alikuwa mwalimu alifundisahaje huko natafuta wanafunzi wake angalau nipate expreience ya huyu ndg yetu mapadlock

==================
Magufuli ni Mwalimu kitaaluma. Wakati anafundisha somo la kemia alikuwa anafundisha kwa kiswahili?

FaizaFox njoo huku lile neno lako linahusika hapa
 
Pretending that the video is not a fake, I would answer you as follows: You can`t judge someone`s intellect from the use of a borrowed language even if he used it throughout his studies. I have good examples to back that, some of which are Chinese friends I know who went to English medium universities after taking intensive English courses in their country and some out of their country but who can`t make any serious conversation in English. But that doesn`t mean that, they didn`t gain from the studies they took in English, they are very good in their professions and you can`t talk in their backs in English without them understanding what you are saying.
Magufuli using English in a speech might have been caused by many reasons some of which can be; The absence of an interpreter or he thought he could make matters more clearer if he spoke himself.
Even if the video was true and not a fake, you can`t disqualify someone with a good achievement record in his career for a thoughtless reason as, the inability to use a language that doesn`t belong to him and which he learned in school. English didn`t build our roads and bridges.
I think someone who deserves to be disqualified is who mentioned in church, that its time for Northerners and Lutherans to lead Tanzanians. Such a statement might sound simple to you, but for those who know our history, it meant a lot. In the 1960`s Northerners tried to create their own republic, something which led to the exile of one of their famous Local Chiefs from that part to Rome. If our intention is to keep our peace and stay united, why these statements?
The person we need to be banish from the election process, is someone who doesn`t have a history of achieving anything in his career except for claims of accomplishments he puts forward without even simple proof.
The person we need to banish from the election process is someone who claims to have done tough decisions without telling us what those tough decisions were exactly so we could know.
The person we need to banish from the election process, is that someone who can`t argue and present matters in his mother tongue to convince us that he deserves our vote.
The person who needs to go, is someone who is telling us that our children will have free education from nursery school to university without showing us how.
The person who needs to go, is someone who can`t remember stuff and yet his gang is trying to convince us that he will bring changes through very well thought ideas.
Lets stop arguing about trivial matters when we have very serious issues to discuss which are more important to our country.

We don`t need a beggar president who will elude us with his English while governing our country on a foreign dime. We need someone we can understand, we are not English or Americans.

Excellent! You said it well bro! Big-up sana. #HapaKaziTu CHAGUA MAGUFULI.
 
Du! Kwa vipi? Kwa kutumia 'learning theories' zipi?

Kuwa na ueledi mkamilifu (expertise) wa lugha ni kuelewa kuizungumza, kuiandika, na kuisoma. Ukipungukiwa na kimojawapo, huwezi kutambulika kama muelewa wa lugha hiyo.
 
Excellent! You said it well bro! Big-up sana. #HapaKaziTu CHAGUA MAGUFULI.

Tuko pamoja Mkuu. Tatizo wengine wanakuja hapa kuleta posts wakiwa na uchungu wa talaka ndio maana ukiangalia posts nyingine zimejaa emotions zaidi kuliko logic. Mtu anashindwa kutuonyesha mazuri ya huyo candidate anaemtetea baada ya kutuletea video feki, sasa sijui tufanye nini. Huyo candidate wake nae ni Kilaza kabisa, haongei English ambacho ndicho kipengele muhimu cha mada hii pamoja na kusomea huko kilikotokea, halafu mtu kashupaa tu.
 
Asipoakuwa makini hata UDSM watamnyang'anya hivyo vyeti vyao....maana anakitia aibu chuo kikuu!:thinking::thinking:
Kwa akili hizi za kitumwa zilizojaa kasumba ya kikoloni kamwe hamuwezi "kumkomboa" mtanzania toka kwa mkoloni mweusi. Mkapa ataendelea "kuwatukana" kwa raha zake. Badilikeni, watanzania sio wajinga kama mnavyofikiria.
 
  • Thanks
Reactions: SMU
"I am a politicians". "I dont want to take this time as saying so many political...."

"Simple and clear is only congregations to you.."
"To the University Korindor... , Co... Cor,.. Colimbia univeristy to the assistance we are getting to this hospt"..
Kuna haja hawa wasomi wa namna ya magufuli wangechunguzwa hizi PhD wanazipataje maana ni aibu...
 
Mhhhhh.... haya hapo chini...

Hakika sasa nnaamini (nina amini) pasi na shaka yoyote ukawa wengi ni kama alivyosema Mkapa.

Hivi mtu anaona kujuwa (kujua) lugha ya nje ndiyo kuwa na akili.

Hawa ndiyo wale wakiona mtoto wa Kingereza wa miaka 3 anaongea Kingereza wanashangaa na kumuona wa ajabu.

Tanzania tuna safari ndefu sana ya kwenda, hatutofika (hatutafika) kesho wala keshokutwa.
 
Itakapofika wakati wa kubargain country's interests na first world ndipo utakapojua umuhimu wa kiingereza

Hapo ndipo akina Makamba wanapojidai ................... Naona safari za nje Makamba ndiye atakuwa msemaji mkuu wa Rais
 
"I am a politicians". "I dont want to take this time as saying so many political...."

Kuna haja hawa wasomi wa namna ya magufuli wangechunguzwa hizi PhD wanazipataje maana ni aibu...

PhD za sayansi hazihitaji ujue sana kiingereza labda phD ya sheria.

Pamoja na kwamba kutoongea kingereza kwa ufasaha haimaanishi kuwa kiongozi mbaya, hiyo ni dalili tosha kwamba mfumo wetu wa elimu una walakini, ikiwa mtu wa PhD bado hawezi kutunga sentensi fasaha ya Kiingereza.

Ila sasa kuna suala la Raisi kuongea huko UN, ambako Kiswahili bado hakijapitiswa kuwa lugha ya UN.

Yale yale ya Id Amin kumwambia Malkia wa Uingereza I must revenge this visit by inviting you to Uganda, na pia kiongozi wa Bunge letu mwaka jana akiwa kwenye kipidindi cha TV alipataja watazamaji kama "our lookers".
 
  • Thanks
Reactions: SMU
"i am a politicians". "i dont want to take this time as saying so many political...."

"simple and clear is only congregations to you.."
"to the university korindor... , co... Cor,.. Colimbia univeristy to the assistance we are getting to this hospt"..
Kuna haja hawa wasomi wa namna ya magufuli wangechunguzwa hizi phd wanazipataje maana ni aibu...

huyu jamaa ana sili ya congo mixer ya kirundi cum hutus
lakini kazaliwa biharamulo,pia huongea kinyambo na kisukuma.
 
Asipoakuwa makini hata UDSM watamnyang'anya hivyo vyeti vyao....maana anakitia aibu chuo kikuu!:thinking::thinking:

Ukweli ni kuwa hapa Tz waliosoma sayansi hata walimu wa vyuo vikuu kiingereza ni shughuli.
Pia hata nyie mlioko humu jamii wengi wenu ndivyo ilivyo. Angalia wakati wa presentation, ni kizungumti. Sasa hili la nyani alioni kund.. inatoka wapi?
 
Ukweli ni kuwa hapa Tz waliosoma sayansi hata walimu wa vyuo vikuu kiingereza ni shughuli.
Pia hata nyie mlioko humu jamii wengi wenu ndivyo ilivyo. Angalia wakati wa presentation, ni kizungumti. ...
Wote hao wanagombea urais wa Tanzania? Hutajisikia fahari kumsikia Rais wa nchi yako akizungumza kwa ufasaha? Pamoja na mabaya yake, napenda sana namna Ben Mkapa anavyotuwakilisha inapokuja suala la kuzungumza (hasa kwa kimombo). Sasa huyu Magufuli atatufanya tuwe tunabadili channel....kukwepa aibu!

Lakini kulitizama kivingine, pengine litapunguza appetite ya Rais (kama atashinda) kuzurura hovyo nje ya nchi na hivyo kutupunguzia gharama.
 
Back
Top Bottom