Elections 2015 Magufuli lugha za Kimataifa ni Kizungumkuti, wenye ufahamu tujadiliane

Elections 2015 Magufuli lugha za Kimataifa ni Kizungumkuti, wenye ufahamu tujadiliane

Hawa wanaong'ang'ana ni wale huwa tunawaita Arts Pure.Huwa husoma masomo na hukuzania sana Kıswahl,Kıingere na Uraia.Wengi wao huwa hawana uwezo wa kutosha kıakili.Magufuli nı mwanasayansi na PhD yake n ya Chemistry,hana haja ya ngwine zenu,ıla kıchwa ni full charged.

Nyie "Wanasayansi" wa hapa Bongo akiwemo na huyo Magufuli mmefanya nini cha maana kulisaidia hili Taifa zaidi ya kukariri tu vilivyoandaliwa na wenzenu?Si ajabu hata practical part ya ulichokaririr hujawahi kufanya hata kwa majaribio. Mkijiita nyie ni "Wanasayansi" Walioko NASA watakuwa kina nani?
 
Nilifikiri utasema treni za umeme kama kenya! Barabara ni wajibu wa kila serikali na sio ahadi ya kampeni!

Kila kitu ni relative hapa Duniani! Kwa wewe unayeishi Kenya ndiyo utaona kwamba Barabara siyo muhimu lkn kwa MTZ wa kawaidia aliyekuwa anatumia siku mbili kusafili km 500 leo hii kama anaweza kutumia masaa 8 kwa nini asione kwamba kuna unafuu?

Hayo mambo ya treni ya Umeme yako nje ya uwezo wetu sasa hivi kwanza hata Kenya wenyewe hawawezi kumudu treni za Umeme lkn hiyo ni mada nyingine sasa hivi tunahitaji Br. za kuunganisha vijiji na vijiji, Wilaya na Wilaya, Mikoa na Mikoa ili tuweze kusafirisha mazao kutoka mashambani kwenda sokoni baada ya kukamilisha hilo ndiyo tuanze kufikiria mambo ya treni ya Umeme lkn kwa sasa hivi hilo halina nafasi na halitekelezeki kwa hali ya kiuchumi tuliyonayo TanZania!
 
Kwa rasilimali tulizonazo Treni ya umeme ni uchafu!!! badala ya kujifunza kiingereza anapoteza muda kupiga pushup
 
Kwa rasilimali tulizonazo Treni ya umeme ni uchafu!!! badala ya kujifunza kiingereza anapoteza muda kupiga pushup

Tatizo ni ulimbukeni! Afya haithibitishwi kwa push ups! MTU tulimwona kabisa kwa babu akihangaikia afya yake hawezi kutuambia chochote! Tunamwombea tu afya yake iimarike!
 
Umesema kweli. Kuna maraisi wengi duniani hawajui kiingereza. Hao wasiojua kiingereza, nao walisoma elimu zao kwa kutumia kiingereza halafu wakawa hawakijui? Naomba jibu.

Labda tuwekane sawa kidogo hapo. Viongozi wengi wa nchi duniani wanajua Kiingereza isipokuwa hawakitumii katika mikutano ya kimataifa kwa sababu siyo lugha rasmi ya nchi zao. Halafu mifumo ya elimu katika nchi nyingi inawalazimu wanafunzi kusoma angalau lugha moja ya kigeni; na Kiingereza mara nyingi kinapewa kipaumbele kwa sababu ya umuhimu wake katika mawasiliano ya kimataifa.
 
China,Korea ni nchi zilizoendelea bila kutegemea mfumo Wa ki capitalist na wanatumia lugha yao hawamjaji kiongozi kwa kutokujua kiingereza wala kifaransa Bali utendaji kazi hizo siasa za kujua lugha za kigeni zipo Tanzania tu
 
Kwani kuongea kiingereza ndio elimu?

Kuifahamu lugha kwa ufasaha pale inapotumika kufundishia (medium of instructions), achilia mbali kuwa sehemu ya elimu, ni kigezo muhimu cha kuruhusiwa kuchukua masomo ya kitaaluma. Ndio maana Watanzania (wako wengi tu) waliosoma nchi kama Urusi, China, Japan, Ukraine, n.k. kwa kutumia lugha za nchi hizo wana uelewa mkubwa wa hizo lugha.
 
Tunahitaji kukomboa fikra zako. Mbona waingereza hawatumii kiswahili? Kwa nini wewe ushobokee kiingereza hadi ufikie kuwashinda na wenye kiinglish Chao?

Hujaelewa tatizo hapo? Huyo bwana amesoma degree ya kwanza mpaka kutunukiwa PhD kwa kutumia lugha ya kiingereza kujifunzia iweje aishindwe kuongea?
Hata mtoto wangu wa kidato cha tano anaweza kiingereza vizuri kuliko Magufuli kwa nini tusiwe na mashaka na elimu yake?
Tumekuwa tunasema kuna degree za chupi hizi za Magu tuziiteje? Kuwa sio lugha yake hiyo sio hoja, hawezi kuja mchina kuwepo mchina akajifunza elimu ya sekondari hadi Phd kwa kiswahili halafu akashindwa kuongea kiswahili vizuri.
Ukimchunguza Magu lazima utagundua kuna tatizo mahali, au ni bingwa wa kukariri na sio kufikiri.
 
Tatizo ni ulimbukeni! Afya haithibitishwi kwa push ups! MTU tulimwona kabisa kwa babu akihangaikia afya yake hawezi kutuambia chochote! Tunamwombea tu afya yake iimarike!

Nakushauri ushugulike kwanza na afya ya Lowassa maana kama Magufuli kunywa kile kikombe unalichukulia kama issue kubwa, kumbuka kile kiko na uhusiano wa karibu na swala la imani zaidi. Mimi si muumini wa hayo ila kama kwa Magufuli ambae ni Mlokole lilikuwa jambo ambalo aliona lingemsogeza karibu na anachokiamini, sioni sababu ya watu kutokwa na mishipa ya shingo wakati ukiangalia ni mgombea wao ndie anaehitaji msaada wao kipindi hiki.
 
Labda tuwekane sawa kidogo hapo. Viongozi wengi wa nchi duniani wanajua Kiingereza isipokuwa hawakitumii katika mikutano ya kimataifa kwa sababu siyo lugha rasmi ya nchi zao. Halafu mifumo ya elimu katika nchi nyingi inawalazimu wanafunzi kusoma angalau lugha moja ya kigeni; na Kiingereza mara nyingi kinapewa kipaumbele kwa sababu ya umuhimu wake katika mawasiliano ya kimataifa.

Bado hatujaachana na hoja ya msingi kwamba, Magufuli hajui kiingereza lugha anayodai kusomea katika levels zake zote. Kama hajui, kwa hiyo hajasoma kwa kuwa huwezi kuelewa chcote kwa lugha usiyoijua!.

Hao maraisi uliowasema, ama walisoma kiingereza na wanakielewa vizuri tu ila hawataki kukitumia kwa kuwa si lugha yao. Hawa wanaoptions na priority yao ni lugha zao. Magufuli siyo kabisa. Anapimwa kwamba ni msomi, kumbe hakuna alichosoma kwa kuwa hana ufahamu na lugh a iliyotumika kwenye kusoma kule na hivyo kumbe elimu zero ndani a miaka kwenye vituo vya elimu ( kama hata alikwenda).

Wengine hawa wamesoma kwa lugha zao, hivyo wanajua walichokisoma kwa lugha zao, tena wanaufahamu wa lugha nyingine za kimataifa kama kiingereza. Hawa hata wasipotumia kiingereza, wamesoma hawa kazi ni kutafasiri tu kwenda kwenye lugha inayohitajika katika mazingira lakini they are knowledgable. Siyo huyu Magufuli ambaye hajasoma kabisa hata uelewa wake unaonyesha hivyo.

Hakuna mtu atasema SADDAM WA LIBYA/ AU KUWAIT halafu aseme nikwa kuwa hajui kiingereza. Halafu anasahaua tangu shule ya msingi hadi chuo kikuu na tena ngazi ya PHD anadai kutumia Kiingereza. Magufulli hana elimu. Ni kati ya 69% ya Makamba aliowasema kupitia TWAWEZA kwamba ni majuha wanaoinga mkono ccm!.

Swali la kujiuliza:, Je Magufuli ana vyeti?

Swali la Pili:, Kavipata kutoka wapi?

Swali la tatu: Kavipata je?

Swali la NNe. Nani kamtunuku?

HOJA:- MAGUFULI NA WALIOMTUNUKU VYETI WOTE WACHUNGUZWE TENA NA VYOMBO VYA KIMATAIFA AMBAVYO HAVINA UFISADI!.

Kumlinganisha Magufuli na Maraisi wasiotumia Kiingereza ama kwa kutokukifahamu au kwa kutokutaka ni ufisadi wa mawazo. Magufuli hajui!. Na kwa kuwa hajiui atuambie kasoma kwa ktumia lugha gani ili tujue kama anakijua alichokisoma. Or else Kiingereza chake, utetezi unaotelewa wa aibu vyote vinajustify akiliyake ya SADDAM WA LIBYA/KUWAIT.
 
Hao wote uliowataja hawakutumia kiingereza kwenye masomo yao. Huyu pombe alitumia kiingereza toka class 3 mpaka Phd. Besides, huyu mtu alisoma seminary na amefundisha mpaka secondary, alipitaje huko kote na hii broken? Kingine, amekuwa waziri for 20 years alishindwa nn kujiongeza kwenye lugha hii muhimu japo informally ili kuepukana na hii aibu? Hii nchi ya ajabu sana viongozi hawaandaliwi then tunashangaa kwanini tumestuck.

Huyu alikuwa mwalim wa sekondari na anafundisha kwa english?! tusishangae tunapoambiwa elimu yetu imeshuka na tunazalisha wahitimu wasioweza ushindani katika soko la ajira. Fikiria mtu kama magufuri anawakirisha nchi katika kujadili mikataba na wawekezaji! Tumeliwa, tafakari, chukua hatua
 
Jamani hilo tatizo ni sugu kwa watu wanaosomea masomo ya sayansi,wasomi wengi sana wanasumbuliwa na kiingereza kwa sababu kadhaa ikiwamo mfumo wa elimu tuliyonayo na namna mhusika alivyochukulia suala la lugha katika masomo yake,kwa maghufuli hiyo ni changamoto kubwa kwake hasa katika.shughuli za kidiplomasia.
 
Kuifahamu lugha kwa ufasaha pale inapotumika kufundishia (medium of instructions), achilia mbali kuwa sehemu ya elimu, ni kigezo muhimu cha kuruhusiwa kuchukua masomo ya kitaaluma. Ndio maana Watanzania (wako wengi tu) waliosoma nchi kama Urusi, China, Japan, Ukraine, n.k. kwa kutumia lugha za nchi hizo wana uelewa mkubwa wa hizo lugha.
Sasa huwezi kulink uelewa wa fani kwa kutumia uelewa wa medium inayotumika kuifundishia. Unapokikana kiingereza, si kuikana elimu na kujua kiingereza si kuwa na ujuzi au elimu, kuna wengi wanaoongea kiingereza kizuri sana lakini kufundishwa ujuzi wowote ni tatizo kwao.
Huwezi kumpima mtu kwa kigezo cha kujua kuongea kiingereza. Kuna kiingereza cha kuongea, kusikia, kuandika n.k
Unaposoma unaweza kuelewa na kujibu maswali kwa kujieleza kimaandishi lakini ukipewa nafasi upresent mada, magoti yanaisha nguvu na tumbo linajaa gesi.
Lakini kuna mtu anaeweza kuongea sana kiingereza lakini ukimchallenge kidogo tu kwa swali jepesi ambalo liko technical utashangaa anatweta na kuitafuta leso.
Tunahitaji kiongozi aliejipanga kuongea na sisi, sio mtu aliejiandaa kutuletea wakoloni weupe na kuendelea kutufanya watumwa.
 
China,Korea ni nchi zilizoendelea bila kutegemea mfumo Wa ki capitalist na wanatumia lugha yao hawamjaji kiongozi kwa kutokujua kiingereza wala kifaransa Bali utendaji kazi hizo siasa za kujua lugha za kigeni zipo Tanzania tu

Bw. Wambura point hapa ni pale lugha inapotumika kufundishia (medium of instructions) na mwanafunzi akasoma masomo ya kitaaluma mpaka ngazi ya mwisho kabisa (Phd) kwa kutumia hiyo lugha na kufuzu vizuri. Inaingia akilini kweli huyu mtaalam asiwe na ufahamu wa hiyo lugha aliyopatia utaalamu wake? Kweli? Hebu tuweke ushabiki wa kisiasa kando! Mfano: unatoka nchini kwenda China kuchukua masomo ya shahada ya kwanza kwa kutumia lugha ya Kichina (miaka 5) na kufuzu vizuri. Je unafikiri tutakuelewa kama baada ya kurudi utakuwa hata kuomba maji kwa Kichina huwezi?
 
Acha ufala wewe. Lugha zisizo na staha nani anashindwa dunia hii? Unajidhalilisha.

Kashupalia kweli video feki ili tu Magufuli ashuke akidhani tunaiamini video wakati tunamuinjoi anavyojitoa ufahamu. Magufuli si wa kushuka leo, its late to come with a stupid fake video move, Tulishaamua kumchagua Magufuli.
Bora mdeal na afya ya Lowassa badala ya kuwaste energy katika kujaribu kumtaint na takataka. Au basi mngekuja na sifa njema za Lowassa ili na sisi tufanye maamuzi.
 
Binafsi siamini kama kujua kiingereza ndicho kigezo muhimu cha kuwa kiongozi. Wapo wanaojua kiingereza vizuri sana lakini maisha yao bado duni kuliko baadhi ya darasa la saba, au wapo wanaojua sana kiingereza lakini hawana sifa wana uwezo wa kuweza kujenga hoja na kuwa viongozi kwa Tanzania. Lakini pia tukumbuke wapo wanaojua kuongea lugha ya kiingereza hata bila kujua kuisoma. Ukiacha mazingira ya nyumbani Waziri Mkuu kama Japan hajui kiingereza lakini ni moja wa viongozi mahiri na wanaoheshimika duniani, Rais wa China hajui kiingereza lakini bado anaongoza taifa la pili kwa uchumi duniani na lenye watu wengi zaidi duniani. Kwangu mimi hoja lugha kuwa gumzo ni ishara ya taifa lenye ufinyu wa fikra na kuwa bado social revolution haijafanyika.
watu mamburula kweli. unatoa mifano ya china na japani kwani wao lugha zao za kujifunzia na mawasiliano official ya kiserikali ni kiingereza? China hawatumii lugha ya kiingerezaa katika shughuli zao sisi tunaitumia kila mahali tangu primary mpaka vyuo vikuu. Hivyo mtu mwenye phd kutoweza kutunga hata sentensi moja sahihi ya kiingereza sio sawa! halafu majukumu anayotaka kupewa yanamlazimu ajue hiyo lugha vizuri kwa sababu itamlazimu kuitumia mara nyingi kuliko alivyokuwa waziri. atakuwa anakutana na wa\geni wengi sana na inabiodi aweze kuwa na ciommunication skills nzuri!
 
Sasa huwezi kulink uelewa wa fani kwa kutumia uelewa wa medium inayotumika kuifundishia. Unapokikana kiingereza, si kuikana elimu na kujua kiingereza si kuwa na ujuzi au elimu, kuna wengi wanaoongea kiingereza kizuri sana lakini kufundishwa ujuzi wowote ni tatizo kwao.
Huwezi kumpima mtu kwa kigezo cha kujua kuongea kiingereza. Kuna kiingereza cha kuongea, kusikia, kuandika n.k
Unaposoma unaweza kuelewa na kujibu maswali kwa kujieleza kimaandishi lakini ukipewa nafasi upresent mada, magoti yanaisha nguvu na tumbo linajaa gesi.
Lakini kuna mtu anaeweza kuongea sana kiingereza lakini ukimchallenge kidogo tu kwa swali jepesi ambalo liko technical utashangaa anatweta na kuitafuta leso.
Tunahitaji kiongozi aliejipanga kuongea na sisi, sio mtu aliejiandaa kutuletea wakoloni weupe na kuendelea kutufanya watumwa.

Uso wa Nyoka nisome vizuri. Sijafagilia Kiingereza; nimezungumzia ufahamu wa lugha iliyotumika kufundishia ni wa lazima. Inaweza kuwa lugha yoyote!
 
Back
Top Bottom