Elections 2015 Magufuli lugha za Kimataifa ni Kizungumkuti, wenye ufahamu tujadiliane

Elections 2015 Magufuli lugha za Kimataifa ni Kizungumkuti, wenye ufahamu tujadiliane

Mimi ninaishi sweden sasa miaka 26.wale ambao wanaongea kiswedish fluently lakini hawakwenda shule (yaani kukaa darasani na kujifunza)wana shida ktk kuandika na grammatical. Hivyo kuongea lugha si kigezo cha kuijua lugha.lugha ni kuielewa kwa vyote hasa kuandika na grammatical.
Najaribu kuimagine vijana shuleni walilazimishwa kuzungumza kiingereza watasema mbona rais naye hajui? Km unaweza kufikia ngazi ya kuwa rais hujui kingereza iweje mimi mwanafunzi nisumbuliwe kukijua? Kwa kweli kumchagua Magufuli ni kuweka bad precedent kwa vijana wetu!
 
Unaamini kweli unaweza kupata hadi Phd bila kujua lugha uliyotumia kufundishiwa?

Kaka itakuwa aibu kwake na kwa taifa! Unakumbuka kilichomtoa Mulugo unaibu waziri ni nini? Aibu aliyotutia kwa sababu ya kukariri. Sasa hapa tuna mtu anayekariri watu wakadhani ni genius kumbe hamna kitu. Lugha ni muhimu kwa mtu wa ngazi ya urais. hakuna namna unaweza kumtetea hapa!
 
Najaribu kuimagine vijana shuleni walilazimishwa kuzungumza kiingereza watasema mbona rais naye hajui? Km unaweza kufikia ngazi ya kuwa rais hujui kingereza iweje mimi mwanafunzi nisumbuliwe kukijua? Kwa kweli kumchagua Magufuli ni kuweka bad precedent kwa vijana wetu!
 
KUWA NA AKILI TIMAMU WEWE:-
1. THE ISSUE NI TANZANIA KUWA -0Dependant sana kwa matifa yanayoongea Kiingereza
2. Mikutano yote ya kimaendeleo inaendeshwa kwa KIINGEREZA
3.Elimu yetu ya bure bado itarudi chini ya kiwango kwa kujenga GHOROFA LA MSINGI WA MATOPE?
i.e. kuwa na CHEKECHEA MPAKA STND. SEVEN kwa kiswahili then FORM ONE MPAKA UNIVERSITY KWA KIINGEREZA?
4.MAGUFULI AKINI -INTERVIEW MIMI KWA KIZUNGU JAMBO LOLOTE ITABIDI AKAE NA DICTIONARY, NA MKALIMANI KARIBU SANA!!!!!

Hivi wewe upo dunia ipi? Jisomee: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...kwete-azindua-sera-ya-elimu-na-maabara-6.html
 
Mnaosema Magufuli hajui kiingereza ndiyo mnaopaswa kutueleza ni vp Magufuli aliweza kusoma bila kuelewa lugha iliyokuwa akifundishiwa hadi akapata hiyo Phd?
 
Hiv rais wa china anajua hata english kweli?... mi nadhqn hiyo siyo ushu hasa kwa wazalendo...labda kuwe na sababu nyingine.....hasa yenye mashiko

China iko dunia ya kwanza... haihitaji misaada

Anyways, JK alisema "we need to manufacture more teachers"
 
Hakika sasa nnaamini pasi na shaka yoyote ukawa wengi ni kama alivyosema Mkapa. Hivi mtu anaona kujuwa lugha ya nje ndiyo kuwa na akili. Hawa ndiyo wale wakiona mtoto wa Kingereza wa miaka 3 anaongea Kingereza wanashangaa na kumuona wa ajabu. Tanzania tuna safari ndefu sana ya kwenda, hatutofika kesho wala keshokutwa.
Je na Sadam wa KUWAIT?
 
Are you saying kuwa mtu ambaye hajui kusoma kiingereza lakini anakiongea vyema kwa kuwa alikuwa mfanyakazi wa ndani kwa mzungu ni bora kuliko wewe?
watu mamburula kweli. unatoa mifano ya china na japani kwani wao lugha zao za kujifunzia na mawasiliano official ya kiserikali ni kiingereza? China hawatumii lugha ya kiingerezaa katika shughuli zao sisi tunaitumia kila mahali tangu primary mpaka vyuo vikuu. Hivyo mtu mwenye phd kutoweza kutunga hata sentensi moja sahihi ya kiingereza sio sawa! halafu majukumu anayotaka kupewa yanamlazimu ajue hiyo lugha vizuri kwa sababu itamlazimu kuitumia mara nyingi kuliko alivyokuwa waziri. atakuwa anakutana na wa\geni wengi sana na inabiodi aweze kuwa na ciommunication skills nzuri!
 
Mnaosema Magufuli hajui kiingereza ndiyo mnaopaswa kutueleza ni vp Magufuli aliweza kusoma bila kuelewa lugha iliyokuwa akifundishiwa hadi akapata hiyo Phd?

Hapa ndio tunapokuja kusema kuwa degree za kupeana.
 
Mi ndo maana naona elimu ya kikanjanja tanzania itaendelea kutuletea makanjanja wengi kuongoza nchi. Ni aibu .nashauri taifa la hofu, tusiogope... Tufanye mabadiliko. Maamuzi magumu mwaka huu. Nadhani itakua suluhisho.

Kiingereza siyo lugha ya Taifa. Namshauri Rais Magufuli atufungulie ukurasa mpya kwa kutumia kiswahili popote aendako na kwenye dhifa za kitaifa. Sisi Tanzania ni nchi pekee katiba nchi zilizotawaliwa na uingereza yenye lugha ya Taifa. Magufuli onyesha mfano kwa kuikuza ienee duniani kote. Kiingereza ni lugha ya biashara acha ibaki kwenye makabrasha wataalamu waihangaikie. Usijali UDSM watakupa wakalimani kila unaposafiri ambako hawajui kiswahili. Ukiweza hili utawaonyesha viongozi wa Sfrika kuwa Tanzania bado inaendelea kuwakomboa.
 
Hiv rais wa china anajua hata english kweli?... mi nadhqn hiyo siyo ushu hasa kwa wazalendo...labda kuwe na sababu nyingine.....hasa yenye mashiko

Sababu ipo.. MAENDELEO! China wana uchumi unaokuwa kwa kasi ya kumpa hofu mmarekani il tz ina uchumi unaoshuka kwa kasi ya ajabu.. there you are
 
katika nchi hii makanjanja wapo wengi sana. huyu magufuli anapaswa achunguzwe kama kweli vyeti alivyo navyo ni vya kweli au magumashi. haiwezekani msomi wa level ya PhD asijue kiingereza! haya ni maajabu ya Musa!
 
Kama english ya jk ni questinable sasa huyu Magufuli si questinable zaidi!?hili ni janga la kitaifa!
 
Lowassa kuna interview na TV ya Kenya kasema "our people are more poorer"

Nikasema duuh.

Wewe uliwahi sema Kikwete hajui kingereza humu
ingawa watanzania wanao mponda Magufuli wanamuona Kikwete ni afadhali sana
sasa huyu Magufuli unamuweka mizani ipi?
 
Wewe uliwahi sema Kikwete hajui kingereza humu
ingawa watanzania wanao mponda Magufuli wanamuona Kikwete ni afadhali sana
sasa huyu Magufuli unamuweka mizani ipi?

Mimi, Kikwete na Magufuli hatuchekani.

Magufuli anaongea kiingereza kama cha Waganda, ukimsikiliza unajua hajasoma nje na anaongea kwa lafudhi ya kwao, lakini unaona anaweza kufikiri kwa Kiingereza akiongea Kiingereza. Albeit he gets sloppy at times, so unbecoming for a chemist.

Kikwete anaongea Kiingereza cha kufikiri katika Kiswahili kwanza halafu kutafsiri maneno kutoka Kiswahili kwenda Kiingereza.
 
Ni kama unasema wanao mponda sana humu hawamtendei haki....
 
Ni kama unasema wanao mponda sana humu hawamtendei haki....

Sio tu hawamtendei haki.

Hawaitendei kazi takatifu ya kuponda viongozi haki.

Magufuli ana mengi sana ya kuponda ambayo hayako as argumentative as anajua Cockney English or not kiasi kwamba ukiniambia habari hizo -ambazo nazo zina umuhimu wake- napata concern kama unaelewa priorities za nchi.
 
Mimi, Kikwete na Magufuli hatuchekani.

Magufuli anaongea kiingereza kama cha Waganda, ukimsikiliza unajua hajasoma nje na anaongea kwa lafudhi ya kwao, lakini unaona anaweza kufikiri kwa Kiingereza akiongea Kiingereza. Albeit he gets sloppy at times, so unbecoming for a chemist.

Kikwete anaongea Kiingereza cha kufikiri katika Kiswahili kwanza halafu kutafsiri maneno kutoka Kiswahili kwenda Kiingereza.

Kiranga umeisikiliza hiyo clip lakini? Comment yako hapa ni kama unasema shida ya Magufuli ni matamshi kitu ambacho si kweli. Ingekuwa shida ya lafudhi watu wangemsema kwenye Kiswahili pia kwani anakitamka kwa lafudhi hiyo hiyo. Clip hii haina uwingi wala umoja, haina tenses, haina vocabularies yaani ni vurugu mtindo mmoja. Nionavyo mimi hata kama ingekuwa Phd aliisomea kirusi bado kithungu chake kilipaswa kuwa kizuri kdg kuliko hii broken lakini sasa hata Phd tunaambiwa ni ya kithungu.
 
Akiwa waziri magufuli alihonga nyumba za serikali. Sasa akiwa rais atahonga nn?
Kumbuka rais wa awamu ya tatu alihonga wizara ya fedha kwa ajili ya dili la mwanamke.
Rais wa awamu ya nne alikuwa anahonga wilaya na mikoa.
Ccm inanuka uchafu haisafishiki. Magufuli ni dodoki chafu
 
Back
Top Bottom