HOTUBA YA JPM ITAKAYOISHI MILELE NA KUREJEWA NA VIZAZI VIJAVYO
Nanukuu
Mimi ndio Rais ninajuwa siri zote za Nchi hii. Linisingeweza kuzungumza haya kama haya ninayozungumza siyajui,ni kuguswa tu na roho mtakatifu nashindwa kuwataja, tumechezewa mno ndiyo maana nayasema haya hadharani ndugu zangu kwamba tumechezewa mno.
Nataka niwahakikishie ndugu zangu katika awamu hii ya 5 chini ya Uongozi wangu HAKUNA KUCHEZEWA. Waje wanalia, Waje wanazunguka, Watajitahidi kutuchonganisha lakini tuseme hakuna kuchezewa. NI AIBU! Tanzanite zilikuwa zinasombwa tu?
Ndio maana nchi inayoongoza kuuza Tanzanite Duniani sio Tanzania! ๐น๐ฟ Nchi ya pili inayoongoza kuuza Tanzanite sio Tanzania! ๐น๐ฟ Wakati Madini ya Tanzanite yako Tanzania tu๐ฃ ๐น๐ฟ. Na ndio maana yaliitwa Tanzanite kutokana na neno Tanzania ๐น๐ฟ.
Fedha zote zilizokusanywa za Tanzanite duniani,Tanzania imepata asilimia tano (5.%) Asilimia tisini na tano (95.%) zimeliwa na wengine wa nje, mnataka ndugu zangu niache kulizungumza hili? sasa nilichaguliwa kuwa Rais wa nini? kama sitazungumza huu uozo hadharani? Nikakae kimya tu kwa kumuogopa nani? Sababu ya maisha yangu?
Si nafuu nizikwe kaburini lakini niuseme ukweli Watanzania waujue? Kwa hiyo ninataka kuwaambia ndugu zangu vita ya uchumi ni ngumu zaidi kiliko vita ya kawaida, kumnyang'anya Mtu alichozowea kukipata bure! Na kuwadharau watanzania ni mambumbumbu, wapumbavu Wajinga, si jambo rahisi, ndio maana nawaomba sana wote tusimame kwa pamoja tuwe wa moja tupiganie haki zetu.
Siku zote nawaambia ndugu zangu sio kwamba sina damu, au sio kwamba mimi sipendi hela. NAJUA MKIAMUA TUTAFIKA.
R.I.P. JPM๐๐๐ ๐ญ๐ญ๐ญ,MWAMBA, SHUJAA SIMBA WA VITA๐น๐ฟ
PUMZIKA KWA AMANI MWANA WA AFRIKA