Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 63,730
- 111,542
Jamaa wa TOTAL walishajitoa kitamboo na Museven hawezi chukua hela za ndani kugharamia huu mradi kama afanyavyo Magufuli kwa kuwadhulumu wafanyakazi na wawekezaji stahiki zao. Huu mradi ni kama haupo labda Magufuli ampe Museven hela za ujenzi wake
Museveni ni tapeli, kisha kakutana na Magufuli asiyemjua vizuri Museveni. Wakati huo mradi unazinduliwa kwa mbwembwe, nilijua ni utapeli kama utapeli mwingine. Nakumbuka utapeli uliokuwa unafanywa na ccm kusema ujenzi wa bomba la mafuta la Uganda ni sehemu ya mafanikio ya Magufuli, kitu ambacho hakikuwa kweli.
Tanzania hatutoi hata senti moja kwenye huo mradi, sisi tunasaka fursa zitakazotokana na huo mradi. Kibaya zaidi tulishapigia hesabu faida itakayotokana na huo mradi. Ni kama tuliandaa kachumbari kisha ndio tukaenda kuwinda swala! Na Magufuli hapa alipo hana hata kumi ya kuwezesha chochote kwenye huo mradi. Kumbuka hapa nchini Magufuli ana miradi miwili inayohitaji 15t+, na hakuna mradi wowote kati ya hiyo imefikia hata robo. Ni wapi atapata hela ya kusaidia chochote kwenye hilo bomba? Ni wazi kuwa ni kupaka rangi upepo.