Magufuli na Kim Jong-Un ni Marais pekee duniani sijawahi kuwaona wakifanyiwa interview

Mtu mwenye sera ya kuvunja Muungano, mwenye kuongea bila kujali Hadhi ya Mwl Nyerere ni wakufanya naye mdahalo si ni kujizalilisha
Kwa hio Magu ana-deserve kufanya interview na nani ambae atakua ni wa standard yake mkuu?
 

Ummy Mwalimu aliwaambia Kamati ya Kudumu ya Bunge ya huduma ya Jamii kwamba Hospital ya rufaa kubwa kanda ya ziwa nzima itajengwa chato kwa sababu Chato ndio ipo katikati ya kanda ya ziwa.,mpk wajumbe wa kamati hio ikabidi wacheke tu.

Ama kweli kwny hii miaka ya 2015-2020 Chato imeibuka ghafla kua iko ki-strategic zaidi kwny kila eneo.
 

Hebu acha kudanganya watu. Kwenye mambo ya budget kwa nchi zilizoendelea lazima nchi ipate baraka za bunge. Na kama unafuatilia mambo ya siasa utasikia kuna neno linaitwa "government shutdown".

Shutdown inapotokea maana yake serikali inashindwa kujiendesha kwasababu hakuna pesa iliyoidhinishwa na bunge. Ilitokea wakati wa utawala wa Trump pale Democrats na Republicans walivyoshindwa kukubaliana juu ya pesa za serikali.
 
Ipi shutdown pia yapo maamuzi ya rais yasiyohitaji baraka za bunge.

Nimekupa mfano wa Russia na US nenda katafute habari zaidi kuhusu madaraka ya marais wao.
 
Ipi shutdown pia yapo maamuzi ya rais yasiyohitaji baraka za bunge.

Nimekupa mfano wa Russia na US nenda katafute habari zaidi kuhusu madaraka ya marais wao.

Wewe ni porojo tu. Mimi nimekupa mfano wa shutdown. Hebu na wewe nipe mfano wa nchi moja iliyoendelea ilivyotumia fedha bila idhini ya bunge ketetea hoja yako.
 
Wewe ni porojo tu. Mimi nimekupa mfano wa shutdown. Hebu na wewe nipe mfano wa nchi moja iliyoendelea ilivyotumia fedha bila idhini ya bunge ketetea hoja yako.
Bajeti za ulinzi za Russia zinapitishwa na Putin. Masuala nyeti kama vile Kuuliwa kwa Husseini yule general wa Iraq serikali ya Trump haikuhitaji baraka za Congress.

Fuatilia kwa wenye kuelewa sheria za nchi utaelezwa juu ya masuala ya dharura ambapo sio lazima wawakilishi wa wananchi wahusishwe.
 
Nchi zinazofanya midahalo kama Marekani zina hali mbaya sana
Muda ni pesa unapoteza mda kuwapa maadui ramani ya jinsi ulivojenga chatto ili wakuangamize.. Hizo nchi zinazofanya midahalo hamna amani kila kukicha wanaviziana,,,, hayo yote ni kuweka siri za nyumbani kwako ziwe ya dunia.
 

Kwanza tuitoe Russia kwenye mjadala huu kwasababu si nchi ya kidemokrasia.

Pili, nafikiri umekose. Yule general alikuwa ni mu Iran sio Iraq kama ulivyoandika. Jina lake pia umelikosea anaitwa Qassim Suleimani siyo Husseini.

Tatu ile ilikuwa ni secret operation, ni kweli Trump hakuhitaji idhini ya bunge. Lakini naamini pesa iliyotumika kukamilisha operation hiyo ilitoka kwenye defense budget ambayo ilishaidhinishwa na Congress.
 
Magu ni mtu mwenye jaziba sana si ajabu kwenye mdahalo anaweza kurusha ngumi
 
Kaka elewa tu kwamba sio kila manunuzi yanafanywa kwa idhini ya bunge na marais wote tangu uhuru wamekuwa na utaratibu huo.
 
Huyu Kim Jong-Un la hapa ni likilaza la kutupwa yan, kiazi kibichi!
 
Utamheshimu Mtu aliyetaka kukuua? Wewe kwa akili yako unaweza kumheshimu Jambazi?
 
Sijawahi kuwaona hawa Marais wawili wakifanyiwa interview. Ni kawaida kuwaona wakuu wa nchi wakihojiwa kuhusu vitu mbalimbali. Mahojiano hayo huwapa fursa waandishi wa habari kuwauliza viongozi maswali ambayo wananchi wangependa kujua majibu yake...
Ha ha ha jamaa mjanja sana wewe. Unatumia maneno matamu kumvuta rais wetu kwenye kina kirefu chenye mamba wakali.
 
Sijawahi kuwaona hawa Marais wawili wakifanyiwa interview. Ni kawaida kuwaona wakuu wa nchi wakihojiwa kuhusu vitu mbalimbali. Mahojiano hayo huwapa fursa waandishi wa habari kuwauliza viongozi maswali ambayo wananchi wangependa kujua majibu yake...
Kim Jong Un huwa mara chachechache ana.ruhusu interview kwani anajua Kifaransa alisoma Chuo Kikuu Switzerland lakini huyu wa kwetu labda ajaribu Mwandishi wa Habari mbobezi Pascal Mayalla (Njaa), Homeboy.

Angalizo:
Lazima awe mwangalifu asije akapigwa teke asifanye interview na akakosa kabisa nafasi ya uteuzi aliotafuta miaka mingi na badala yake yakampata makubwa zaidi. Lissu hatafuti uteuzi anataka tu waonyeshane ubabe mafahari wawili!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…