Magufuli ndio Rais ambaye hakuacha legacy yoyote

Katika kumbukizi ya miaka 4 Toka aliyekuwa Rais wa awamu ya 5 Hayati Magufuli atutoke

Magufuli ni Rais ambaye hakuacha Legacy yoyote hapa nchini na badala yake alituachia mzigo ambao Rais Samia anapambana kusawazisha mambo

1. Aliharibu upande wa diplomasia
Magufuli ndo aliwaita wawekezaji mabeberu na kuwaona wabaya na kuwatangazia kila jina baya.
Alisema wazi kwamba yeye hataki Tanzania, hakuwahi kuhudhuria vikao vya kidplomasia popote
Alipika propaganda za uongo ati hakuna covid 19
Baada ya Rais Samia ndo alijitahidi kutembea na kuwaleta wawekezaji ambao Kwa Sasa angalau kidogo tunaona nuru

2. Kuharibu democrasia
Magufuli alipiga marufuku mikutano ya vyama vya siasa, ili asikike yeye tu ndo propaganda zake za kuita watu wanyonge
Vifo vya wapinzani wengi kama Azzory Gwanda, Ben Saanane n.k
Kupigwa risasi Kwa Tundu Lissu
Kusingizia kesi na kufunga watu waliompinga kama Yusuph Manji na Kabendera

3. kuuwa uchumi wa Taifa.
Magufuli ndo alinunua ndege 8 bila kushirikisha bunge na Kwa maamzi yake binafsi baadae ndege zote zikawa mbovu na kuishia karakana.
Alishindwa kutambua kuwa mahitaji ya wananchi sio ndege Bali ni miundo mbinu ya afya, barabara, madaraja n.k
Alimfukuza makampuni Shindani ya ATCL kama Fast jet
Shirika la ndege lilifirisika na Sasa mama Samia ndo analifufua taratibu

4. Kuzuia ajira Kwa vijana
Magufuli ndo alifungwa ajira za umma, hasa ualimu na afya
Na kusababisha vijana waliotoka kaya masikini kurundikana mtaani bila suluhu
Mamilion ya graduates wako mtaani sababu ya sera mbovu za Magufuli.
Pongezi Kwa Rais Samia anajaribu kupunguza japo mzigo ni mkubwa

5 Kodi Kandamizi
Magufuli aliwakandamiza wafanyabiashara na wananchi Kwa ujumla kulipa Kodi utitiri hapa wafanyabiashara wengi wakifunga biashara na wengine kumhamisha biashara zao kwenye mataifa mengine.
Magufuli alianzisha Kodi Kwa wafanyabiashara wadogo kama kitambulisho ambapo hata muuza mboga alilazimika kulipa Elfu 20 ili afanye biashara

6. Kilimo na uvuvi
Utawala wa Magufuli tulishuhudia kudorora la soko la mazao
Mfano kwetu Kagera tuliuza kahawa kg sh 900 ila kipindi cha Samia tumeuza sh 7000
Magufuli alikuwa sekta ya uvuvi akishirikiana na waziri wake Luhaga Mpina, fika Kanda ziwa, Zanzibar, Nyasa na Kigoma hawataki kusikia jina la Magufuli

7 Matumizi mabaya ya madaraka.
Sio tu Hayati Magufuli alitumia madaraka yake vibaya ila pia wateule wake mfano Sabaya
Sabaya alikata watu vipanja, alichoma watu moto, alinyanganya watu hela na alijisifu kuwa ni DC pekee angeweza kumpigia simu Magufuli usiku wa manane na akapokea
Wakuu wa wilaya walitumia mamlaka Yao vibaya na kuwaweka mahabusu wapinzani Kwa masaa 24 ilikuwa kama fashion kipindi cha Hayati Magufuli
Wala hakukemea

8 Kula hela maafa ya Bukoba
Kipindi cha utawala wake Bukoba walipata tetemeko na akaitisha michango Kwa ajili ya watu wahanga
Cha ajabu aliwakana na kusema serikali haikuleta tetemeko

9. Magufuli alihujumu uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu 2020
Mtu mwenye akili timamu anajua wazi kuwa CCM haiwezekani kushinda vitongoji, vijiji/ mitaa, kata na majimbo yote
Lakini Kwa Magufuli alifanya hivi kuiba na kudhulumu Imani ya Watanzania

10. Alianzisha miradi isiyoisha.
Mfano SGR Kwa miaka yote alokaa madarakani mbali na kujenga SGR kipande lakini hakununua hata kichwa kimoja cha train

JNHPP
Huu mradi licha ya kuimbwa na machawa wake, lakini hakuna ulipoufikisha, aliacha mifereji, vifusi na tractor zikiwa site miaka nenda Rudi.
Umeme unajumuisha uzalishaji, kuhifadhi, usafirishaji na usambazaji
Yeye hata hatua ya uzalishaji hakuifikia

Haya ni baadhi tu
Binafsi nasema Magufuli ndo Rais ambaye hakufanya vyema katika utawala wake

RIP Hayati Magufuli
Mrundi tangu lini ataje mazuri ya Tanzania. Huna lolote
 
Kila mtu afaidi ujinga wake
 
Attachments

  • 10C2E98D-2184-4947-A6DD-F1AE75EC7556.jpeg
    10C2E98D-2184-4947-A6DD-F1AE75EC7556.jpeg
    103.8 KB · Views: 23
Bilashaka hizi habari nyingi ulizoandika nahisi umezinukuu au kusimuliwa.

Hayati hakuacha legacy kwasababu hakuwa kiongozi wa watu wa chche hasa wajuu, alifany mambo yaliyokuwa na tija kwa maslahi mapana ya Taifa bila kutafuta umaarufu.

Wengi waliomchukia mwendazake ni wababaishaji walioshindwa kuikwepa sheria aliyokuwa akiinyoosha hasa kodi kukwepwa na wafanya biashara wakubwa.

Embu tembea uone machinga anapokonywa kibiashara chake na manispaa, zunguka uone barabara zilizojengwa hyo awamu kwa muda mfupi, Hao unaowaita wawekezaji ndo hao wanatusainisha mikataba kandamizi inayodumaza uchumi.

Sitaki kuamini kama unasifu mikopo zaidi ya kujifunza kuuza mali kwa faida!.. Mf. Wawekezaji waliobainika kufanya uhuni wa makilinikia ulitaka awaalike ikulu wapumzike kwenye bustani?? Mwizi hhafai .

Semeni yote ila kwangu HE WAS THE BEST AND HE IS STILL.

NB: TUPUNGUZENI UCHAWA, UCHAWA UNAFANYA MTU AONE MKAA NI MWEUPE KULIKO KARATASI
 
Katika kumbukizi ya miaka 4 Toka aliyekuwa Rais wa awamu ya 5 Hayati Magufuli atutoke

Magufuli ni Rais ambaye hakuacha Legacy yoyote hapa nchini na badala yake alituachia mzigo ambao Rais Samia anapambana kusawazisha mambo

1. Aliharibu upande wa diplomasia
Magufuli ndo aliwaita wawekezaji mabeberu na kuwaona wabaya na kuwatangazia kila jina baya.
Alisema wazi kwamba yeye hataki Tanzania, hakuwahi kuhudhuria vikao vya kidplomasia popote
Alipika propaganda za uongo ati hakuna covid 19
Baada ya Rais Samia ndo alijitahidi kutembea na kuwaleta wawekezaji ambao Kwa Sasa angalau kidogo tunaona nuru

2. Kuharibu democrasia
Magufuli alipiga marufuku mikutano ya vyama vya siasa, ili asikike yeye tu ndo propaganda zake za kuita watu wanyonge
Vifo vya wapinzani wengi kama Azzory Gwanda, Ben Saanane n.k
Kupigwa risasi Kwa Tundu Lissu
Kusingizia kesi na kufunga watu waliompinga kama Yusuph Manji na Kabendera

3. kuuwa uchumi wa Taifa.
Magufuli ndo alinunua ndege 8 bila kushirikisha bunge na Kwa maamzi yake binafsi baadae ndege zote zikawa mbovu na kuishia karakana.
Alishindwa kutambua kuwa mahitaji ya wananchi sio ndege Bali ni miundo mbinu ya afya, barabara, madaraja n.k
Alimfukuza makampuni Shindani ya ATCL kama Fast jet
Shirika la ndege lilifirisika na Sasa mama Samia ndo analifufua taratibu

4. Kuzuia ajira Kwa vijana
Magufuli ndo alifungwa ajira za umma, hasa ualimu na afya
Na kusababisha vijana waliotoka kaya masikini kurundikana mtaani bila suluhu
Mamilion ya graduates wako mtaani sababu ya sera mbovu za Magufuli.
Pongezi Kwa Rais Samia anajaribu kupunguza japo mzigo ni mkubwa

5 Kodi Kandamizi
Magufuli aliwakandamiza wafanyabiashara na wananchi Kwa ujumla kulipa Kodi utitiri hapa wafanyabiashara wengi wakifunga biashara na wengine kumhamisha biashara zao kwenye mataifa mengine.
Magufuli alianzisha Kodi Kwa wafanyabiashara wadogo kama kitambulisho ambapo hata muuza mboga alilazimika kulipa Elfu 20 ili afanye biashara

6. Kilimo na uvuvi
Utawala wa Magufuli tulishuhudia kudorora la soko la mazao
Mfano kwetu Kagera tuliuza kahawa kg sh 900 ila kipindi cha Samia tumeuza sh 7000
Magufuli alikuwa sekta ya uvuvi akishirikiana na waziri wake Luhaga Mpina, fika Kanda ziwa, Zanzibar, Nyasa na Kigoma hawataki kusikia jina la Magufuli

7 Matumizi mabaya ya madaraka.
Sio tu Hayati Magufuli alitumia madaraka yake vibaya ila pia wateule wake mfano Sabaya
Sabaya alikata watu vipanja, alichoma watu moto, alinyanganya watu hela na alijisifu kuwa ni DC pekee angeweza kumpigia simu Magufuli usiku wa manane na akapokea
Wakuu wa wilaya walitumia mamlaka Yao vibaya na kuwaweka mahabusu wapinzani Kwa masaa 24 ilikuwa kama fashion kipindi cha Hayati Magufuli
Wala hakukemea

8 Kula hela maafa ya Bukoba
Kipindi cha utawala wake Bukoba walipata tetemeko na akaitisha michango Kwa ajili ya watu wahanga
Cha ajabu aliwakana na kusema serikali haikuleta tetemeko

9. Magufuli alihujumu uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu 2020
Mtu mwenye akili timamu anajua wazi kuwa CCM haiwezekani kushinda vitongoji, vijiji/ mitaa, kata na majimbo yote
Lakini Kwa Magufuli alifanya hivi kuiba na kudhulumu Imani ya Watanzania

10. Alianzisha miradi isiyoisha.
Mfano SGR Kwa miaka yote alokaa madarakani mbali na kujenga SGR kipande lakini hakununua hata kichwa kimoja cha train

JNHPP
Huu mradi licha ya kuimbwa na machawa wake, lakini hakuna ulipoufikisha, aliacha mifereji, vifusi na tractor zikiwa site miaka nenda Rudi.
Umeme unajumuisha uzalishaji, kuhifadhi, usafirishaji na usambazaji
Yeye hata hatua ya uzalishaji hakuifikia

Haya ni baadhi tu
Binafsi nasema Magufuli ndo Rais ambaye hakufanya vyema katika utawala wake

RIP Hayati Magufuli
Kusema hakuacha legacy yoyote napingana na wewe, uthubutu wa kuanzisha miradi mikubwa hakuna raisi wa kufanana naye kati ya awamu zote, nakubali alikuwa na mapungufu yake
 
Kwa Afrika mabeberu wanataka rais mda wote uwe monta wao sasa huyu ndugu hizo staili hakuzifagilia hata kidogo embu mcheki Ghadafi wale jamaa kila kitu walikuwa wanapata kutoka selikarini bado walimuondoa tu , hata huyu ndugu yetu walimuondoa sababu alijitoa Kwa maskini na mda wote alikuwa anasema nimejitoa sababu ya WATANZANIA na mwisho HAKUNA ALIEKAMILIKA KILA KITU WOTE TUNA MAPUNGUFU R. I. P POMBE WATANZANIA TULIKUPENDA KWA KWELI
 
Iko wapi hiyo legacy aliyoiacha?
Mnawehuka kwa jinsi alive piga kazi. Leo ni miaka mitano lkn bado mnajaribu kumbomoa. Nyie mnaowaita wazungu mabwana wamewapa nini? Mpaka mkalambe miguuì na bado mtadaiwa mpaka mkome! Magufuli taswira ya viongozi shupavu na hili vuguvugu linaendelezwa na kina Ibrahima Traore mpaka marais vibaraka wote pamoja na chawa wao kama nyinyi waishe. Fukuza wazungu wote wanyonyaji. Huo mradi JNHPP, SGR na mabarabara ndiyo mnayojisifia nayo sasa hvǰ ba mnatumia kama karata ya kupatia kura, si mlisema ni gharama na haifai? Tena mbona mmemalizia? Amefunua watu wengi kujiamini
na kufikiri kizalendo. Watu kama nyinyi ndiyo wazungu wanawataka ili muwauzie nchi kwa bei chee. Nyakati hizo tushavuka
 
Magufuli ni Rais ambaye hakuacha Legacy yoyote hapa nchini na badala yake alituachia mzigo ambao Rais Samia anapambana kusawazisha mambo
Yawezekana Rais Magufuli hakuacha urathi mkubwa ila kwa uchache aliwaachia Rais Samia Hassan ambae alikuwa ni makamu wake wa rais hata huo pia ni urathi. Shukuruni na jivunieni Rais Magufuli kumchagua Samia Hassan kuwa makamu wake wa rais na hatimae kuwa rais kamili kwa mjibu wa ibara ya 37(5) ya Katiba.
 
Alikuwa ni mtu wa hovyoo sana ....Toka Dunia iumbwe hakuwahi kutokea mtu wa hovyo kama magufuri....Nb: endeleeni kukaza huko na Mimi nakaza huku 😀😀😀
 
😀😀 muacheni mzee wa watu amepumzika huko

1. Kawaachia SGR mmeifikisha wapi
2. Kawaachia mradi wa umeme Vijijini REA kwa 27000 saivi umepanda hadi 325,000
3. Kawaachia daraja la busisi hadi saivi limefikia wapi..?
4. Vipi ule mradi wa umeme wa mwalimu nyerere uliokua mkombozi kwa mwananchi kwa kupunguza bei naona unaendelea vizuri

Kweli magufuli alikua mjinga sana 😢
Kwani wakati wa magufuli vilifika wapi
 
JNHPP
Huu mradi licha ya kuimbwa na machawa wake, lakini hakuna ulipoufikisha, aliacha mifereji, vifusi na tractor zikiwa site miaka nenda Rudi.
Umeme unajumuisha uzalishaji, kuhifadhi, usafirishaji na usambazaji
Yeye hata hatua ya uzalishaji hakuifikia
Wasomi wa bongo bana mnajiona mna akili sana na na hivi viji half baked analyses vyenu. Magufuli was battlin' for that project, and it was clear as day the odds were stacked against him, even his own minister Makamba was throwin' shade, but homie stood tall and held his ground like a boss. Msinge muua wajinga nyie Tanzania ingekuwa mbali sana.
Aliharibu upande wa diplomasia
Magufuli ndo aliwaita wawekezaji mabeberu na kuwaona wabaya na kuwatangazia kila jina baya.
Alisema wazi kwamba yeye hataki Tanzania, hakuwahi kuhudhuria vikao vya kidplomasia popote
Alipika propaganda za uongo ati hakuna covid 19
Baada ya Rais Samia ndo alijitahidi kutembea na kuwaleta wawekezaji ambao Kwa Sasa angalau kidogo tunaona nuru
Hiyo COVID-19 yako Leo Iko wapi?. And what did your Samia really do with those COVID-19 funds she was given? Build these tiny classrooms?

Anyways pambana Ili uzidi kuonekana msomi humu jukwaani na viuchambuzi uchwara vyenu.
 
Back
Top Bottom