Magufuli ndio Rais wa mwisho kutawala kupitia CCM

Magufuli ndio Rais wa mwisho kutawala kupitia CCM

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
52,828
Reaction score
165,667
Nyakati za CCM kuendelea kutawala nchi hii zimefika mwisho na yote haya mnayoyashuhudia leo hii ni viashiria tu vya anguko la CCM katika siku zijazo.

Kelele za wana-CCM majukwaani, mitandaoni, Bungeni na kwingineko, ni sawa tu na mateke ya farasi anaekata roho hivyo hayaepukiki na watarusha sana mateke mpaka mtawahurumia.

Walizoea madaraka na zaidi wana hofu ya nini kitawapata baada ya wao kupoteza madaraka maana wengi wao ni watuhumiwa wa mambo mbalimbali walipokuwa wakishika madaraka katika ofisi za umma kwahiyo baadhi yao wana hofu ya kushughulikiwa.

Pia, kuna wanaotarajia kuteuliwa kushika madaraka siku zijazo na kuna wanaotarajia kugombea nafasi mbalimbali katika chaguzi zijazo, hivyo wote hawa pamoja na tegemezi wao ni lazima warushe mateke kama farasi anaekata roho maana wanakwenda kunyang"anywa tonge mdomoni jambo ambalo hawawezi kulikubali kirahisi.

Na lazima mjue hii ndio siri ya wao kushikamana hata katika kutetea mambo ambayo hata dini zetu zinayapinga kwani wanajua wasiposhikamana na kumtetea boss kwa nguvu zote ataanguka, na akianguka wanajua na wao ndio itakuwa mwisho wa matumaini yao.

Hata hivyo,CCM wajue tu it is already too late na Magufuli ndio anahitimisha utawala wa CCM katika nchi hii na atarithiwa na kiongozi kutoka moja ya vyama vya upinzani hapa nchini ingawa kutakuwa na magumu ya hili jambo kutimia zikiwemo gharaza za kulipa kwa baadhi ya watu maana kwa Afrika mambo haya hayaepuikiki but all in all CCM haina nafasi tena kwa sasa.

Ukweli ni kwamba CCM imeanza kuporomoka miaka mingi na ndio maana hata wagombea uraisi wa chama hicho kila chaguzi kura zao zinashuka na wa kujilaumu ni CCM wenyewe kwa matendo yao, matendo ambayo awamu hii sasa yamekihiri na hata dunia imeanza kuwanyooshea kidole huku awamu hii ikizidi kabisa kujiweka mbali na wananchi wa kawaida hivyo kuzidi kuchochea anguko lake.

Kwa maneno mengine, CCM hii ya Magufuli inayojali maendeleo ya vitu kuliko ustawi wa maisha ya watu, plus matendo ya watu wasiojulikana, na pressure ya mataifa kutoka nje kupinga haya yanayoendelea hapa nchini kwa sasa, combination hii ya mambo ndio itakwenda kuhitimisha utawala wa CCM siku si nyingi.

Kumbukeni pia utafiti wa Twaweza ulioonyesha poromoko la Mkulu kwa kiwango cha SGR ndani ya muda mfupi tu.

Nina hakika hata baadhi ya wana-CCM wanajua ukweli huu akiwemo yule mwanasiasa alie-post picha ya saa mtandaoni ingawa hakufafanua anamanisha nini lakini kila mwenye akili alielewa ujumbe aliokusudia kuufikisha katika jamii.

Nimalizie kwa kuwaambia kuwa, Tundu Lissu is just a catalyst kwenye mchakato unaondelea wa anguko la CCM.

Mtarusha sana mateke lakini haitasaidia.

Kila chenye mwanzo kina mwisho.

Time will tell.
 
Tena 2015 Baada Ya Lowasa Kuingia Pale Wakasema Kwamba Watashinda Uchaguzi Sa4 Asubuhi[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]

Sent using Jamii Forums mobile app

Ni lini CCM ilishinda kihalali !!?.Mkibanwa mbavu na Wapinzani mnaanza kuua Raia kwa kutumia Policccm..

Tunajua Mfumo mzima una kifeva Chama Tawala kupitia Taasisi za Serikali ,na hivi Majuzi mmejiimarisha zaidi kwa kupitisha Sheria mbaya ya Vyama vya Siasa kwa kuumpa Uungu Msajili wa Vyama vya Siasa huku ikizingatiwa ana wajibika kwa alie mteua (Raisi) ambae anatokana na Chama Tawala..

R.I.P.. Akwilina ..
 
Nasikitika kuona kuna mtanzania atapata ugonjwa moyo matokeo ya urais yatakapotangazwa 2020. Jiandae kupata matibabu kwa sababu CCM ipo na itaongoza mpaka pale watanzania watakapokuwa na mawazo tofauti na waliyo nayo sasa kuhusu upinzani
 
Mwaka 2015 chadema kura million 6...ccm million 8...kwa kusaidiwa na kuiba.akiamungu kwa hasira za kizazi kipya 2020 sizani kama wataweza kuiba.watu wanahasira kuanzia huko huko ccm kwenyewe it is just a matter of time.
 
CCM haita tawala milele ila upo uwezekano mkubwa kunasiku ika anguka, ila kwa hali iliyopo inawezekana ikachukua miaka 20-25 kwa kadirio la karibu ikiwa CCM itapasuka yaani ukitokea mgogoro mkubwa ndani ya CCM.

CCM haitashindwa na upinzani kutokea nje Upinzani Utatokea Ndani kwakua Chadema iliyokua tishio siku za nyuma imekufa yenyewe kabla ya CCM, Imeuliwa na maMvi kutoka CCM.

Kama CCM ilipita salama uchaguzi 2015 kwasasa ni ngumu kuipoteza, maMvi na mipesa yake alishindwa kuipasua CCM akaenda kuinunua Chadema. Ni ngumu sana CCM kuanguka ata ao Mabeberu ambao wanajaribu kumtumia Lisu ili CCM ikose imani kwa wananchi wanalitambua hilo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tujikumbushe kauli hizi...

1. Tusipowatoa CCM mwaka huu, tusubiri miaka 50-E.N.Lowasa,2015
2.CCM isipotoka mwaka huu najiuzulu siasa-F.A.Mbowe 2015..

Siasa kama simba na yanga tu na mbio za kushinda Kombe la Mabingwa afrika..[emoji4]
 
Hata Kikwete mlisema hivyo hivyo,
huyo Tu ndu Lisu wenu ni naive
kama ninyi mnaomfuata na kumuamini na haelewi jinsi Dunia ilivyo, anaamini kabisa kwamba Muzungu ni mtu fair na atamtangaza Raisi wa JMTZ kama Guido, lkn msichokijua hakuna maslahi yoyote ya Muzungu yaliyohatarishwa hapa Bongo, kwanza hata Majeshi yetu yako Kongo sasa Muzungu atake kufanya ,,regime change” JMTZ kwa lipi?

Kwanza mngekuwa na akili hata mngeelewa jambo pekee lililomgusa Muzungu ni ushoga na Wanafunzi wa kike kufukuzwa Shuleni kwa kupata Mimba na hata interview yote ya hardtalk ilihusu hilo, Muzungu alitaka kujua msimamo wa Upinzani kuhusu Ushoga basi, hayo mengine yoote ujinga tu.

Hivyo Muzungu mnayekimbilia kwake hajali chochote kuhusu madai yenu mnayoshitaki.
Kwa maelezo yako unaonekana unatambua uwezo wa mzungu kuweka mtu wao kwenye uongozi wowote akiamua.
 
CCM ilishachokwa lakini vyama vya upinzani haviwezi kuitoa ccm kwa sababu kwanza hakuna kitu wanachosimamia kikaeleweka kwa wananchi kwa mfano sasa tundu lissu anazunguka ulaya na marekani akionyesha wazi anataka wamusaidie ili waje wanufaike baadae, kuunga mkono mahusiano ya jinsia moja kitu ambacho ni tofauti na utamaduni wetu kwa hiyo msijidanganye mtaitoa ccm kwa propaganda za mitandaoni
 
Nimalizie kwa kuwaambia kuwa, Tundu Lissu is just a catalyst kwenye mchakato unaondelea wa anguko la CCM.
Kwa sheria za uchaguzi za sasa ambapo matokeo ya urais hayapingwi kokote pale baada ya kutangazwa; kwa kuwa sasa hivi mwenyekiti wa CCM ndiye huteua majaji huko NEC na kwa kuwa mwenyekiti huyo ndiye anayeteua wanachama wa CCM kuwa maDED (ambao by default wanakuwa wawakilishi wa NEC huko majimboni), CCM haitoanguka kamwe. Huo ndio ukweli
 
Hata wewe ni msemaji wa chama..!
Kweli mmepoteana duh..
Siasa ni kutumia akili nyingi sio jazba, vitisho na laana tunazoshuhudia, unaposimama na kuamini kupitia lissu ndio ccm itang'oka unajisumbua ndugu anajulikana ikungi na dar na huko kwa shangazi

Mlipoamua kumfukuza mzee wa watu Slaa na mitusi mikubwa kuwa mla mihogo kupotea kulianzia hapo, maono ya mzee huyu yalifika mbali na yalitikisa hata neno fisadi likawa key kubwa ya kusikika, lakini mwkiti alijali maslahi yake badala ya uzalendo kwa chama na taifa ikajakauli mbiu ya kubadilisha gia angani haya ndio matokeo, na usisahau kuna kundi kubwa halikukubali haya mabadiliko

Kwa hiyo ndugu kutukana, majungu kwenda kwa wazungu kushitaki yakimalizika mwisho wake ni nini..
Povu, matusi Ruksa..lakini ukweli usemwe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
CCM ilishachokwa lakini vyama vya upinzani haviwezi kuitoa ccm kwa sababu kwanza hakuna kitu wanachosimamia kikaeleweka kwa wananchi kwa mfano sasa tundu lissu anazunguka ulaya na marekani akionyesha wazi anataka wamusaidie ili waje wanufaike baadae, kuunga mkono mahusiano ya jinsia moja kitu ambacho ni tofauti na utamaduni wetu kwa hiyo msijidanganye mtaitoa ccm kwa propaganda za mitandaoni
Kwani haki ya faragha ina maana gani ktk katiba

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Endelea kuota mchana! Endelea kujifariji sioni chama mbadala wa CCM. Labda kutawala mitandaoni ndiyo Chadema wanaweza na huyo mgonjwa labda atatawala huko ugaibuni kwenye media ya mabeberu
Magufuli mgonjwa zaidi ana moyo wa plastic itakuwa miguu 2020 atapumzishwa idiwe tabu ccm bye bye
 
Back
Top Bottom