Magufuli ndio Rais wa mwisho kutawala kupitia CCM

Kwa mitandaoni nakubali kwa 100%

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ukweli usio kuwa na chenga ambao ccm wanauogopa kuusikia. ila kunawachache ambao wameisha soma alama za nyakati na wameanza kujikana kama kina nape wanasema wanajutia bao la mkono.Na makamba anasema hakuhusika na kutunga sheria makosa ya mtandaoni! Na Bashe naye anataka uchunguzi wa mauwaji na utekaji wakati miaka yote alikuwa kimya. Na kipindi cha kampeni alisikika akihamasisha wanaccm kuwakata mapanga wapizani.yajayo yanafurahisha.
 
Tujikumbushe kauli hizi...

1. Tusipowatoa CCM mwaka huu, tusubiri miaka 50-E.N.Lowasa,2015
2.CCM isipotoka mwaka huu najiuzulu siasa-F.A.Mbowe 2015..

Siasa kama simba na yanga tu na mbio za kushinda Kombe la Mabingwa afrika..[emoji4]
1 & 2 wote matapeli wa kiwango cha SGR
 
.

Jr[emoji769]
 
Kwa katiba hii, hakuna mafanikio kwa chama kingine kuchukua madaraka. Ni vyema kujipa moyo tu ipo day tutafika!
 
Endelea kuota mchana! Endelea kujifariji sioni chama mbadala wa CCM. Labda kutawala mitandaoni ndiyo Chadema wanaweza na huyo mgonjwa labda atatawala huko ugaibuni kwenye media ya mabeberu
Tumechoka wafilsti kututawala lazima tuwakate magovi yenu
 
Sioni mantiki yoyote juu ya ili.

Ikiwa viongozi wenyew wa upinzani walioaminiwa na wananchi kuanza kuwasaliti na kujiunga na utawala unategemea kweli utawala kungoka na unasema Magufuli ndyo wa mwisho?

Unaweza ukasema magu ndyo wa mwisho ila ajaye asiwe magufuli ila kutoka ccm lazma..

Muda utaongea!

wakati ukuta.
 
Kwa namna alivyojiandaa kung'ang'ania madarakani, kwa kinywa chake mwenyewe amekuwa akidai kuwa haoni mtu mwingine anayefaa kusimamia miradi aliyoiasisi zaidi yake.

Baada ya kina Musiba na Juma Nkamia kupima upepo ,mara wengine waende mahakamani kudai katiba ibadilishwe ili atawale milele, sasa ameamua kujitokeza mwenyewe na kutamka kilicho moyoni mwake.

Ndo maana amekuwa akitumia nguvu kubwa kuzima upinzani ili aje kufanikisha azma yake kiulaini.

Nachoweza kuwaeleza ni kwamba, atafanikiwa azma yake kwa sababu, Tanzania ni taifa lenye watu wajinga kupindukia.

Ila baada ya yeye, Rais atakayefuata atakuwa mpinzani na atakabidhiwa Madaraka kwa sekeseke na CCM itafutika kabisa ktk siasa za Tanzania.
 
Bado hujakomaa Kisiasa hivyo rudi tena Shuleni / Chuoni ukajifunze ili usizidi Kutuonyesha ' Udhaifu ' wako ambao kila Siku zinavyoenda unazidi tu Kuongezeka. CCM haina ' Uhuni ' ambao upo na umeota ' Mizizi ' huko Kwenu Upinzani hasa CHADEMA wa Viongozi ' Kung'ang'ania ' Madarakani utadhani wengine mliobaki wote mna Akili za ' Kipa Katoka ' tupu.

Kwa kukusaidia tu nikiwa kama Shabiki / Mdau Mkubwa wa CCM Mwenyekiti wetu Taifa na Rais Dkt. Magufuli wala hatoongeza muda wake Madarakani kama ambavyo ' Wapuuzi ' wengi mnavyomzushia ikiwa ni Agenda yenu Kisiasa hasa baada ya Kushindwa Kukiimarisha chenu ndani ya hii Miaka Mitano.

Muda wake Kuongoza Tanzania ni Mihula Miwili tu huu wa Kwanza wa 2015 hadi 2020 na ule wa mwisho wa 2020 hadi 2025 na baada ya hapo CCM itawaletea Watanzania Rais mwingine mzuri tu ambaye ataendeleza pale ambapo Rais Magufuli atakuwa ameishia kama vile na Yeye alivyorithishwa na Rais Mstaafu Kikwete ambaye nae pia alirithishwa na Rais Mstaafu Mkapa ambaye nae pia alipokea Kijiti kizuri kutoka kwa Rais Mstaafu Mzee Mwinyi ambaye nae pia alipikwa vyema na Kuaminiwa na Hayati Baba wa Taifa ambaye ndiyo Muasisi Mwandamizi wa CCM yetu.

Ninachojua na ambacho pia nina uhakika nacho ni kwamba CCM itaongoza Tanzania miaka Milioni Mia Saba ijayo au mpaka pale Yesu Kristo atakapokuja au dunia itakapopinduka na kuwa nyingine.

Waambie Wapinzani Wenzako mtafute cha Kufanya ila kwa jinsi mlivyo ' Wadhaifu ' hata Muungane wote bado hamna Uwezo wa Kushindana na hata Kuiondoa CCM yangu / yetu Madarakani.
 
One thing which is certain there is a plan in motion two go beyond to term limit
 
raisi wa mwisho kutawala kwa ridhaa ya wananchi kupitia ccm alikuwa kikwete. Magufuli alipachikwa tu kwa nguvu ya policcm na tumeccm wakisimamiwa na team goli la mkono kupitia Nape na Makamba. ndio maana Magufuli hatawali bali ana paraganya, intimidating watu. bila vitisho sasa hivi ccm ingekuwa imebaki historia tu. na hata Magufuli wenyewe na serikali yake nzima wanajuwa kuwa karibu asilimia 80% ya watanzania hawataki hata kusikia ccm. ndio maana ikitokea uchaguzi maalumu wanatowa week mbili za kampeni. kabla hata wananchi hawajajuwa unasikia amepita bila kupingwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…