Magufuli: Nikiwa Waziri nilinyweshwa sumu na viongozi waliochukia utendaji kazi wangu, nilitaka kujiuzulu

Magufuli: Nikiwa Waziri nilinyweshwa sumu na viongozi waliochukia utendaji kazi wangu, nilitaka kujiuzulu

Alipopona aliwasambazia raha Manesi waliokuwa wanamhudumia ile wodi ya kule chini mwishoni maana plan B ilikuwa Sindano ya sumu.
Hapa ni kwamba aliwapa mlungula ili aweze kuishi au ilikuwaje? maana kama ilikuwa ni kudungwa sindano ya sumu manesi si lolote kuzuia hilo tukio kipenzi...

Halafu uje PM sasa 😉
 
Ni hisio tu angejulikana asingepona.Labda waliosomeshwa namba limishwa meno wanaweza akawa mmoja wao
 
Uwe na akili ww,zito hajaalikwa na jiwe,kaalikwa na mkapa,tatizo una mahaba mabaya ya kupitiliza na jiwe,vibaya hivyo

Kwani kuwa na mahaba ni dhambi? JPM anafanya kazi ya kututoa pale tulipokuwa na kwenda mahali pengine bora zaidi sina haja ya kutokumpenda Maendeleo ya Tanzania kwanza mengine baadaye.
 
Hii ni tuhuma kubwa sana kutolewa na Mkuu kabisa wa Nchi.Mwenye uwezo wa kufanya chochote kwa yoyote yule.najiuliza haikuwa busara zaidi kwa yeye kukaa kimya kwa sasa ili taarifa ama hizo aje aweke kwenye kitabu chake kama hicho kilichozinduliwa leo.
 
Ole, Mkuu JF ilianza 2006 ikitokea Jamboforums. Na utawala wa Mkapa ulianzia 1995-2005, sasa labda unataka kusema tuliongelea suala hilo kama tukio la nyuma kwa wakati huo au mie ndio sijaelewa?
 
Hapa ni kwamba aliwapa mlungula ili aweze kuishi au ilikuwaje? maana kama ilikuwa ni kudungwa sindano ya sumu manesi si lolote kuzuia hilo tukio kipenzi...

Halafu uje PM sasa 😉

😂 Hapo mwisho hapo! Tulia kwanza, hakuwapa mlungula lakini wote waliomuhudumia kule Madaktari na manesi walikuwa na imani sana. Wangeachia tu.....
 
kwahio alijua kwamba ni mawaziri, alijua kwamba sababu ilikuwa ni kusifiwa.., lakini hakujua wakati wanampa sumu ? assumptions zinaanzia wapi na kuishia wapi ?, kauli hizi zinaleta maswali kuliko majibu
 
Hii ya Magufuli haikutangazwa Mkuu, iliisha kimya kimya
 
😂 Hapo mwisho hapo! Tulia kwanza, hakuwapa mlungula lakini wote waliomuhudumia kule Madaktari na manesi walikuwa na imani sana. Wangeachia tu.....
Hahah ukuje upande wa pili bwana. Basi ukiona hivyo jua waliosuka huo mpango walikuwa ni watu wa kawaida na kuna mtu mzito aliingilia kati, maana ingekuwa ni amri ya mkuu wa nchi kwa kipindi hicho ni haraka tu sasa hivi angekuwa amekwisha fukiwa chini kipenzi.
 
Mkuu JF ilianza 2006 ikitokea Jamboforums. Na utawala wa Mkapa ulianzia 1995-2005, sasa labda unataka kusema tuliongelea suala hilo kama tukio la nyuma kwa wakati huo au mie ndio sijaelewa?

Wakati tunabadili jina kutoka Jambo forums ulikuwepo?
 
Sio uongo, wala hatafuti huruma kwa hili unamuonea mkuu. Uliza wana Dodoma......
Hajui kuwa unaweza ukalishwa sumu mwisho wa siku ukasurvive vizuri kabisa, ila itategemea kiwango cha sumu ulicholishwa na ukali wa sumu husika kwa Tanzania sumu ziko chache sana labda ndio maana wataalamu waliweza kumpa huduma ya antidote na huduma nyingine ndio maana aka recover.

Ishu ya sumu iko very sensitive sana, maana mtu wakiamua wanakupa ya muda mrefu kidogo mwisho wa siku ukifa wanasema ulipata stroke ukazima kama taa chwaaah.
 
Rais Magufuli akiwa kwenye uzinduzi wa Kitabu cha Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu, Mzee Benjamin Mkapa amefunguka mambo makubwa mno hajawahi kuyasema popote, mambo aliyoyasema ni pamoja na utendaji kazi wake uliomkosha Mzee Mkapa, Kuchukiwa na mawaziri na viongozi wengine wakubwa mpaka kunyweshwa sumu nk

Magufuli amepita majaribu Mengi hadi kufikia kuwa Kiongozi wa Nchi

Tuna mengi ya kujifunza kutoka kwa huyu Mzee.


HOTUBA YA RAIS MAGUFULI KWA UFUPI

Nampongeza Mzee Mkapa kwa kutimiza miaka 81, Mzee Mkapa ni shujaa wangu naomba nitayozungumza leo yasitafsiriwe vibaya na kupotoshwa.

Baada ya kuchaguliwa kuwa Mbunge, mzee Mkapa aliniteua kuwa Naibu Waziri wa Ujenzi chini ya Mama Anna Abdallah, hata sikujua kwanini aliniteua, lakini nazidi kukushukuru mzee Mkapa

Moja ya mambo akifurahia jambo hafichi furaha yake na akichukia hafichi chuki yake, nakumbuka Mzee Mkapa pale tulipofanya kazi vizuri alipata furaha sana kwenye kazi za barabara mpaka akatamka kuwa mimi ni Askari wake namba moja.

Nilichojifunza kwa Mzee Mkapa ukimshauri kitu na kikitekelezwa hata yakitokea makosa hatakuacha peke yako atasimama na wewe

Wakati nikiwa Naibu Waziri wa Ujenzi na nitoe siri leo, makatibu wakuu wengi hawawaheshimu manaibu waziri, lakini nilipokuwa natoa maagizo yalipokuwa hayatekelezeki, mzee Mkapa alikuwa anatoa maagizo yeye na maagizo hayo yanatekelezeka

Nilipofanya kazi vizuri Mzee Mkapa hakusita kunisifia na sitosahau siku aliyotangaza kuwa, Mimi (Magufuli) ni askari wake wa mwamvuli, baada ya kutangazwa hivyo nilichukiwa na Viongozi wengi akiwemo wa ngazi za juu hadi kufikia hatua ya kunyweshwa sumu Dodoma

Nashukuru Mungu baada ya kunyweshwa sumu na kupona, nilienda kwa Mzee Mkapa na kumueleza azma yangu ya kujiuzulu, nakumbuka aliniangalia kwa jicho la mama na mwana na kuniambia usijiuzulu akanipa ulinzi na kuendelea kuchapa kazi

Nilichojifunza kwake Mzee Mkapa ni mtulivu, Mcha Mungu, mwanadiplomasia, mwanafunzi wa Sera na falsafa za Mwl. Nyeyere, asiye mnafiki na msema kweli

Niwahimize viongozi wastafau kuandika vitabu, nafurahi kusikia vitabu vya Mzee Kikwete na Mzee Mwinyi vipo katika hatua za mwisho kukamilia, hili lisiishie kwa Marais wastaafu, ningefurahi kusikia Maalim Seif akaiandika kitabu, Mzee Warioba na wengine wakiandika.

Kuna issue hii ya uchaguzi wa 2019. Tusiondoshwe ktk mjadala huu kupitia "remote factors". Rais hawezi kulalamika na kutafuta huruma ktk kipindi hiki na kuelekea 2020 kupitia mambo ya kihistoria.

Kama amejirizisha na jambo ni wakati wake wa kutenda ili haki yote ipatikane. Taasisi ya Urais ituambie tumefikia wapi na mchakato wetu wa uchaguzi 2019. Kujaribu kututoa ktk mjadala huu, itakuwa ni kutotendea haki umma wa Watanzania.
 
Zitto nae mropokaji kama waropokaji wengine tu
Sifahamu lakini wakati ule nakumbuka hapa JF tuliliongelea na alikwenda kutibiwa kwenye one of the Scandinavian countries. Kama sikosei Mzee Mwanakijiji vile vile aliligusia. Lakini hatukujua kama alipewa sumu, hilo linashtusha ndio mfahamu siasa zetu za Tanzania zilivyo. Mwenyezi Mungu atakulinda tu hata kama mafisi yako porini yanakusubiri.

Last time tuliongelea kutoruhusu kila Tom Dick and Harry kutaka kusalimiana na rais, ifike mahali huo mtindo uachwe maana waovu huwa hawana sura. Nimeshangaa leo hata Zito kajitokeza ambaye alivumisha ule udaku wake, the boy is not ashamed? Hivi Wizara ya Mambo ya Ndani imechukua hatua gani? Au walitaka kuchukua hatua akifa? Haya mambo ni lazima sasa yachukuliwe kwa upana na ukubwa wake. As a Country we need to act now.
 
Hivi ni nani aliyemlinda Mussolini au Hitler hadi kupata madaraka makubwa yaliyosababisha Vita ya pili ya dunia na kuangamiza wanadamu kwa mamilioni!!!? Ni Mungu huyu huyu uliyemnukuu au Kuna mwingine!!!?
Kama wewe ni mtu wa kuamini Mungu wa dini za Israel na Uarabuni basi ujue mfalme au raisi yeyote hata umuone katili au mbaya ujue ameletwa na kusimikwa na Mungu kwa makusudi flani.
Huenda ikiwa kutokana na kukithiri kwa uovu au madhambi flani kwa walioletewa huyo kiongozi au for greater good of the mankind in general.
Soma hapo chini ukizingatia maandishi yaliyo kolezwa wino(bold font).

Romans 13:1
Every person is to be in subjection to the governing authorities For there is no authority except from God, and those which exist are established by God.

1 Peter 2:13-14
Submit yourselves for the Lord's sake to every human institution, whether to a king as the one in authority, or to governors as sent by him for the punishment of evildoers and the praise of those who do right.
 
Back
Top Bottom