Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hapa ni kwamba aliwapa mlungula ili aweze kuishi au ilikuwaje? maana kama ilikuwa ni kudungwa sindano ya sumu manesi si lolote kuzuia hilo tukio kipenzi...Alipopona aliwasambazia raha Manesi waliokuwa wanamhudumia ile wodi ya kule chini mwishoni maana plan B ilikuwa Sindano ya sumu.
Ukute mtu alikula tu kumbikumbi huko wakamdhuru basi alidhani kawekewa sumu
Kwa sababu hakuna ushirikina kama unavyowaza. Ondoka kwenye kivuli cha ushirikina ulichojifunika.Kifimbo kilishindwa vipi zuia kifo
Uwe na akili ww,zito hajaalikwa na jiwe,kaalikwa na mkapa,tatizo una mahaba mabaya ya kupitiliza na jiwe,vibaya hivyo
Hapa ni kwamba aliwapa mlungula ili aweze kuishi au ilikuwaje? maana kama ilikuwa ni kudungwa sindano ya sumu manesi si lolote kuzuia hilo tukio kipenzi...
Halafu uje PM sasa 😉
Hii ya Magufuli haikutangazwa Mkuu, iliisha kimya kimya
Hahah ukuje upande wa pili bwana. Basi ukiona hivyo jua waliosuka huo mpango walikuwa ni watu wa kawaida na kuna mtu mzito aliingilia kati, maana ingekuwa ni amri ya mkuu wa nchi kwa kipindi hicho ni haraka tu sasa hivi angekuwa amekwisha fukiwa chini kipenzi.😂 Hapo mwisho hapo! Tulia kwanza, hakuwapa mlungula lakini wote waliomuhudumia kule Madaktari na manesi walikuwa na imani sana. Wangeachia tu.....
Mkuu JF ilianza 2006 ikitokea Jamboforums. Na utawala wa Mkapa ulianzia 1995-2005, sasa labda unataka kusema tuliongelea suala hilo kama tukio la nyuma kwa wakati huo au mie ndio sijaelewa?
Hajui kuwa unaweza ukalishwa sumu mwisho wa siku ukasurvive vizuri kabisa, ila itategemea kiwango cha sumu ulicholishwa na ukali wa sumu husika kwa Tanzania sumu ziko chache sana labda ndio maana wataalamu waliweza kumpa huduma ya antidote na huduma nyingine ndio maana aka recover.Sio uongo, wala hatafuti huruma kwa hili unamuonea mkuu. Uliza wana Dodoma......
Kuna issue hii ya uchaguzi wa 2019. Tusiondoshwe ktk mjadala huu kupitia "remote factors". Rais hawezi kulalamika na kutafuta huruma ktk kipindi hiki na kuelekea 2020 kupitia mambo ya kihistoria.Rais Magufuli akiwa kwenye uzinduzi wa Kitabu cha Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu, Mzee Benjamin Mkapa amefunguka mambo makubwa mno hajawahi kuyasema popote, mambo aliyoyasema ni pamoja na utendaji kazi wake uliomkosha Mzee Mkapa, Kuchukiwa na mawaziri na viongozi wengine wakubwa mpaka kunyweshwa sumu nk
Magufuli amepita majaribu Mengi hadi kufikia kuwa Kiongozi wa Nchi
Tuna mengi ya kujifunza kutoka kwa huyu Mzee.
HOTUBA YA RAIS MAGUFULI KWA UFUPI
Nampongeza Mzee Mkapa kwa kutimiza miaka 81, Mzee Mkapa ni shujaa wangu naomba nitayozungumza leo yasitafsiriwe vibaya na kupotoshwa.
Baada ya kuchaguliwa kuwa Mbunge, mzee Mkapa aliniteua kuwa Naibu Waziri wa Ujenzi chini ya Mama Anna Abdallah, hata sikujua kwanini aliniteua, lakini nazidi kukushukuru mzee Mkapa
Moja ya mambo akifurahia jambo hafichi furaha yake na akichukia hafichi chuki yake, nakumbuka Mzee Mkapa pale tulipofanya kazi vizuri alipata furaha sana kwenye kazi za barabara mpaka akatamka kuwa mimi ni Askari wake namba moja.
Nilichojifunza kwa Mzee Mkapa ukimshauri kitu na kikitekelezwa hata yakitokea makosa hatakuacha peke yako atasimama na wewe
Wakati nikiwa Naibu Waziri wa Ujenzi na nitoe siri leo, makatibu wakuu wengi hawawaheshimu manaibu waziri, lakini nilipokuwa natoa maagizo yalipokuwa hayatekelezeki, mzee Mkapa alikuwa anatoa maagizo yeye na maagizo hayo yanatekelezeka
Nilipofanya kazi vizuri Mzee Mkapa hakusita kunisifia na sitosahau siku aliyotangaza kuwa, Mimi (Magufuli) ni askari wake wa mwamvuli, baada ya kutangazwa hivyo nilichukiwa na Viongozi wengi akiwemo wa ngazi za juu hadi kufikia hatua ya kunyweshwa sumu Dodoma
Nashukuru Mungu baada ya kunyweshwa sumu na kupona, nilienda kwa Mzee Mkapa na kumueleza azma yangu ya kujiuzulu, nakumbuka aliniangalia kwa jicho la mama na mwana na kuniambia usijiuzulu akanipa ulinzi na kuendelea kuchapa kazi
Nilichojifunza kwake Mzee Mkapa ni mtulivu, Mcha Mungu, mwanadiplomasia, mwanafunzi wa Sera na falsafa za Mwl. Nyeyere, asiye mnafiki na msema kweli
Niwahimize viongozi wastafau kuandika vitabu, nafurahi kusikia vitabu vya Mzee Kikwete na Mzee Mwinyi vipo katika hatua za mwisho kukamilia, hili lisiishie kwa Marais wastaafu, ningefurahi kusikia Maalim Seif akaiandika kitabu, Mzee Warioba na wengine wakiandika.
Sifahamu lakini wakati ule nakumbuka hapa JF tuliliongelea na alikwenda kutibiwa kwenye one of the Scandinavian countries. Kama sikosei Mzee Mwanakijiji vile vile aliligusia. Lakini hatukujua kama alipewa sumu, hilo linashtusha ndio mfahamu siasa zetu za Tanzania zilivyo. Mwenyezi Mungu atakulinda tu hata kama mafisi yako porini yanakusubiri.
Last time tuliongelea kutoruhusu kila Tom Dick and Harry kutaka kusalimiana na rais, ifike mahali huo mtindo uachwe maana waovu huwa hawana sura. Nimeshangaa leo hata Zito kajitokeza ambaye alivumisha ule udaku wake, the boy is not ashamed? Hivi Wizara ya Mambo ya Ndani imechukua hatua gani? Au walitaka kuchukua hatua akifa? Haya mambo ni lazima sasa yachukuliwe kwa upana na ukubwa wake. As a Country we need to act now.
Andiika kiswahili vizuri bwashee!
Kazi ya mwenge ni nnKwa sababu hakuna ushirikina kama unavyowaza. Ondoka kwenye kivuli cha ushirikina ulichojifunika.
Kama wewe ni mtu wa kuamini Mungu wa dini za Israel na Uarabuni basi ujue mfalme au raisi yeyote hata umuone katili au mbaya ujue ameletwa na kusimikwa na Mungu kwa makusudi flani.Hivi ni nani aliyemlinda Mussolini au Hitler hadi kupata madaraka makubwa yaliyosababisha Vita ya pili ya dunia na kuangamiza wanadamu kwa mamilioni!!!? Ni Mungu huyu huyu uliyemnukuu au Kuna mwingine!!!?