Magufuli: Nikiwa Waziri nilinyweshwa sumu na viongozi waliochukia utendaji kazi wangu, nilitaka kujiuzulu

Magufuli: Nikiwa Waziri nilinyweshwa sumu na viongozi waliochukia utendaji kazi wangu, nilitaka kujiuzulu

Mpaka sasa nimejiuliza maswali mengi bila kupata majibu. Sijui kama lengo ilikuwa ni kutujulisha au ni kupata sympathy. All in all, in my opinion it was given at the wrong platform .
 
Kutokana na kukwepa kifo kwa sumu ile na kupewa ulinzi, yawezekana ndio maana ulinzi wake kama Rais upo hivi (angalia picha). Hapa ni kwenye mazingira haya ambayo huashiria kwenye mazingira mengine hali ni hii hii au zaidi.

1573617492146.png


1573617525848.png


1573617560083.png
 
Kuna vigogo Wa CCM walihusika, mbaya zaidi mmoja ameshakwenda Ikulu Mara kadhaa
 
Rais Magufuli akiwa kwenye uzinduzi wa Kitabu cha Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu, Mzee Benjamin Mkapa amefunguka mambo makubwa mno hajawahi kuyasema popote, mambo aliyoyasema ni pamoja na utendaji kazi wake uliomkosha Mzee Mkapa, Kuchukiwa na mawaziri na viongozi wengine wakubwa mpaka kunyweshwa sumu nk

Magufuli amepita majaribu Mengi hadi kufikia kuwa Kiongozi wa Nchi

Tuna mengi ya kujifunza kutoka kwa huyu Mzee.


HOTUBA YA RAIS MAGUFULI KWA UFUPI

Nampongeza Mzee Mkapa kwa kutimiza miaka 81, Mzee Mkapa ni shujaa wangu naomba nitayozungumza leo yasitafsiriwe vibaya na kupotoshwa.

Baada ya kuchaguliwa kuwa Mbunge, mzee Mkapa aliniteua kuwa Naibu Waziri wa Ujenzi chini ya Mama Anna Abdallah, hata sikujua kwanini aliniteua, lakini nazidi kukushukuru mzee Mkapa

Moja ya mambo akifurahia jambo hafichi furaha yake na akichukia hafichi chuki yake, nakumbuka Mzee Mkapa pale tulipofanya kazi vizuri alipata furaha sana kwenye kazi za barabara mpaka akatamka kuwa mimi ni Askari wake namba moja.

Nilichojifunza kwa Mzee Mkapa ukimshauri kitu na kikitekelezwa hata yakitokea makosa hatakuacha peke yako atasimama na wewe

Wakati nikiwa Naibu Waziri wa Ujenzi na nitoe siri leo, makatibu wakuu wengi hawawaheshimu manaibu waziri, lakini nilipokuwa natoa maagizo yalipokuwa hayatekelezeki, mzee Mkapa alikuwa anatoa maagizo yeye na maagizo hayo yanatekelezeka

Nilipofanya kazi vizuri Mzee Mkapa hakusita kunisifia na sitosahau siku aliyotangaza kuwa, Mimi (Magufuli) ni askari wake wa mwamvuli, baada ya kutangazwa hivyo nilichukiwa na Viongozi wengi akiwemo wa ngazi za juu hadi kufikia hatua ya kunyweshwa sumu Dodoma

Nashukuru Mungu baada ya kunyweshwa sumu na kupona, nilienda kwa Mzee Mkapa na kumueleza azma yangu ya kujiuzulu, nakumbuka aliniangalia kwa jicho la mama na mwana na kuniambia usijiuzulu akanipa ulinzi na kuendelea kuchapa kazi

Nilichojifunza kwake Mzee Mkapa ni mtulivu, Mcha Mungu, mwanadiplomasia, mwanafunzi wa Sera na falsafa za Mwl. Nyeyere, asiye mnafiki na msema kweli

Niwahimize viongozi wastafau kuandika vitabu, nafurahi kusikia vitabu vya Mzee Kikwete na Mzee Mwinyi vipo katika hatua za mwisho kukamilia, hili lisiishie kwa Marais wastaafu, ningefurahi kusikia Maalim Seif akaiandika kitabu, Mzee Warioba na wengine wakiandika.

Jonh usijali,we are with you and praying for you real hard,The God of Jacob and Isack never fails.
 
Hata Tundu Lissu atakuja kusimulia alivyopigwa risasi kibao hadharani wakati Wa utawala wa Magufuli!
Siku hazigandi!
 
Mungu alimlinda Mja wake Mkuu, Mungu alimuandaa Magufuli kuwa Rais wa Tanzania
Kuja kuikomboa Tanzania kutoka kwenye mikono ya Mafisadi, wauza madawa ya kulevya na wapiga dili

Magufuli ni sauti ya wanyonge zandrano,
 
Wakuu Jana nilisikia mojawapo wa Mawaziri waliomuonea wivu JPM kupendwa na Rais Mkapa, wakati akiwa waziri na Askari mwavuli, basi Mawaziri wa ngazi za juu na hali iliyosababisha yeye kulishwa sumu.

Swali langu; Je, Kuna ngazi za Mawaziri zaidi ya WM then Mawaziri? Au ilikuwa inamlenga mtu Fulani? Nani alikuwa waziri wa ngazi ya juu wakati huo?
Tuko huru kujadili kwa sababu Kama ilikuwa classified, basi JPM amefanya declassified jana.

Kwa kweli nchi za ulimwengu wa 3, bado hatujui kufanya declassification. Tukifanya declassification tunaweza kuishia kutengeneza tatizo kubwa zaidi. Ticha tu ndo alikuwa anajua kufanya declassification kwa maslahi ya Taifa na siyo kwa maslahi binafsi.
 
Back
Top Bottom