Magufuli: Nikiwa Waziri nilinyweshwa sumu na viongozi waliochukia utendaji kazi wangu, nilitaka kujiuzulu

Magufuli: Nikiwa Waziri nilinyweshwa sumu na viongozi waliochukia utendaji kazi wangu, nilitaka kujiuzulu

Wilderness Voice,

Ahsante kwa maelezo yako." Kuchukua kozi" na kusoma kozi" zinamaanisha kitu kimoja na ni kiswahlili kinachoeleweka kwa watu wote. Kuhusu swali lako la kuwa na ushahidi kuwa Magufuli anahusika kuwapoteza watu, ninao ushahidi wa kimazingira ambao hauna shaka na pia yeye kama rais na amiri jeshi mkuu wa majeshi yote/na pia mkuu wa serikali ambayo ina jukumu la kuhakikisha usalama kwa raia wake anahusika moja kwa moja na vitendo hivyo vya kijinai.

1. Rais alishasema kuwa "huwezi ukapinga pinga halafu uachwe uka-survive" Haukupita muda Lissu akapigwa risasi katika mazingira yaliyotengenezwa na serikali, kama hilo halitoshi akanyimwa matibabu (Kwa sababu hakufa, wakataka kwa nguvu afe kwa kukosa matibabu), Iweje mbunge tena mkuu wa kambi ya upinzani apigwe risasi kwenye majengo ya serikali yenye ulinzi wa masaa 24 ya askari polisi? Je waliompiga risasi huyo mbunge wamekamatwa hadi leo....licha ya gari lao namba kujulikana? Acha hayo mahaba ndugu yangu.

2. Katika kipindi cha huyu bwana Magufuli, Maiti za watu zinaokotwa nyingi zikiwa ndani ya viroba....Ina maana Magufuli ameshindwa kuzuia haya mauaji? Kwanini yeye asiwe mhusika namba moja kama hata haya mambo hayatolei angalau tamko la kusema kuwa waliohusika watapatikana ile watanzania tuwe na amani.

3. Waandishi wanaoandika kuhusu haya mauaji wanapotea.....kisingizio kinachotolewa na wasukuma ( Andrew Chenge, Sirro nk) kuwa wanakimbia familia zao ni ushamba uliokithiri. Ni wasukuma tu wanaokimbia familia zao. Hao watu wamefichwa au wameuawa kama alivyosema Kabudi.

4 Wasanii kama Roma Mkatoliki na wengine wametekwa kwa sababu ndogo tu(Trivial reasons). Rais hajui kuwa taasisi ya rais haina immunity ya kuachwa kusemwa. Kama rais anahangaika na watu wadogo wadogo ni rais wa aina gani huyo? (Rais hana busara amejawa na "tantrums" na "temper"......Mbona ataua wengi tu kwa sababu watanzania wengi ni waelewa siyo watu wa kusifu uongo)

5. Ben Saanane amepotea kwa kutaka kujua kama huyo mheshimiwa amepata hiyo Ph. D yake kihalali maana kila kitu kinamshinda....Inashangaza kiasi kwamba inashusha heshima ya kusoma.

6. Mengi yanayotokea katika utawala wake inaonekana hata kusikitika haoni kama ina maana. Watu wanauawa ovyo au wanatekwa ovyo ovyo mchana mchana na hao usalama wake wa Taifa lakini anaona ni sawa. Kwa jinsi hii utasema yupo safi?

NB: Kuna mengi mabaya anayafanya huyo Magufuli, anataka kujiaminisha kuwa yeye ni Mungu, anaonea watu, anabaka demokrasia kwa kisingizio cha kuleta maendeleo. ....Hiyo si sawa! Na wewe unajinasibu kuwa unaipenda Tanzania wakati unashindwa kukemea mateso wanayoyapata watanzania wenzako?
 
Kwani Waziri Mkubwa ni Waziri Mkuu?

Kwani kati ya "Waziri" na "Naibu Waziri" ni yupi Waziri Mkubwa?

Waziri Mkuu ni mkubwa kwa Waziri.

Waziri ni Mkubwa kwa Naibu Waziri.

Kwa hiyo ukisema Waziri Mkubwa inategemea unalinganisha Waziri Mkuu na Waziri na Naibu Waziri au Waziri na Naibu waziri.
 
field marshall1,

Ha ha ha ha! Nilijua tu utakuja na sababu zile zile, Na pia elewa maana ya Common mistakes, ukijua hutobisha. Umetoa hadithi kibao za matukio kukariri na kusema wanachosema watu. Katika sheria hasa sheria ya jinai (Criminal Law) unapotaka kujua mtu kafanya kosa uwa vinaangaliwa vitu viwili: Cha kwanza ni Tendo je muhusika kafanya tendo yeye mwenyewe kama yeye kama ni kitendo cha kuuwa kunaushahidi wa kuonyesha kilichofanyika ni tendo lake"Actus reus" na pili inaangaliwa mind ya mtu wakati anafanya hicho kitendo alijua kuwa anakifanya amekikusudia kukifanya inaitwa "mens rea"

Pili katika ushahidi ukoje? ni mazingira gani yaliyopo kuonesha au kuashiria kitendo kilifanywa na yeye. Kiufupi labda hujanielewa. Hapa ndo nikaongelea ushahidi wa kusikia. Unachosema wewe umesikia hayo yote unayohadithia. Unafuata mkumbo tu. Huna ushahidi kamili ukiulizwa leo. Na kisheria ili umweke mtu hatiani lazima uwe na ushahidi ulokamilika. Ushahid wa kusikia "Hearing evidence is not evidence at all"

Hivi unauhakika gani Serikali ndo ilimpiga Lisu risasi? Kwanini Lisu asipeleke madai yake mbele ya mahakama za kimataifa kwamba ni serikali ndo ilimpiga risasi? Kupotea kwa Ben saanane, kwa nini chama (Chadema) akijaishitaki serikali kuwa wamehusika katika upoteaji wa Ben? Ndugu yangu acha porojo za kisiasa. Tumia akili yako si kila lisemwalo weye unashabikia bila kuchambua. Siasa inauwanja mpana. Umzaniae siye kumbe ndiye! Chunguza kisemwacho si kujiaminisha nawe unaandika vitu bila ku digest!
 
Waziri mkubwa huenda walikuwa ni baadhi ya Mawaziri, lakini hakuwa waziri Mkuu, ila kwa kiherehere cha Magu huenda alichukiwa na wengi ,na LAITI angechukiwa na waziri Mkuu enzi hizo angeishia msmu wa kwanza wa unaibu uwaziri, ila hata hivyo nguvu za giza zinasaidia.
 
Waziri mkubwa huenda walikuwa ni baadhi ya Mawaziri, lakini hakuwa waziri Mkuu, ila kwa kiherehere cha Magu huenda alichukiwa na wengi ,na LAITI angechukiwa NA waziri Mkuu enzi hizo angeishia msmu wa kwanza wa unaibu uwaziri, ila hata hivyo nguvu za giza zinasaidia.
Rais siyo kiherehere ndg!
 
Kwani Waziri Mkubwa ni Waziri Mkuu?

Kwani kati ya "Waziri" na "Naibu Waziri" ni yupi Waziri Mkubwa?

Waziri Mkuu ni mkubwa kwa Waziri.

Waziri ni Mkubwa kwa Naibu Waziri.

Kwa hiyo ukisema Waziri Mkubwa inategemea unalinganisha Waziri Mkuu na Waziri na Naibu Waziri au Waziri na Naibu waziri.
Umejibu vizuri mkuu,pia inawezekana mkubwa kwa umri kati ya mawaziri wote waliokuepo. [emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]
 
Umejibu vizuri mkuu,pia inawezekana mkubwa kwa umri kati ya mawaziri wote waliokuepo. [emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]

Aisee ila pia ikawa ni Wizara Kubwa kwa maana ya kimajukumu na unyeti wake Mfano Wizara ya TAMISEMI au Mambo ya Nje.

Na Waziri atakuwa mkubwa kwa kuwa Wizara nayo ni kubwa
 
Back
Top Bottom