field marshall1
JF-Expert Member
- Sep 17, 2017
- 1,171
- 2,732
Wilderness Voice,
Ahsante kwa maelezo yako." Kuchukua kozi" na kusoma kozi" zinamaanisha kitu kimoja na ni kiswahlili kinachoeleweka kwa watu wote. Kuhusu swali lako la kuwa na ushahidi kuwa Magufuli anahusika kuwapoteza watu, ninao ushahidi wa kimazingira ambao hauna shaka na pia yeye kama rais na amiri jeshi mkuu wa majeshi yote/na pia mkuu wa serikali ambayo ina jukumu la kuhakikisha usalama kwa raia wake anahusika moja kwa moja na vitendo hivyo vya kijinai.
1. Rais alishasema kuwa "huwezi ukapinga pinga halafu uachwe uka-survive" Haukupita muda Lissu akapigwa risasi katika mazingira yaliyotengenezwa na serikali, kama hilo halitoshi akanyimwa matibabu (Kwa sababu hakufa, wakataka kwa nguvu afe kwa kukosa matibabu), Iweje mbunge tena mkuu wa kambi ya upinzani apigwe risasi kwenye majengo ya serikali yenye ulinzi wa masaa 24 ya askari polisi? Je waliompiga risasi huyo mbunge wamekamatwa hadi leo....licha ya gari lao namba kujulikana? Acha hayo mahaba ndugu yangu.
2. Katika kipindi cha huyu bwana Magufuli, Maiti za watu zinaokotwa nyingi zikiwa ndani ya viroba....Ina maana Magufuli ameshindwa kuzuia haya mauaji? Kwanini yeye asiwe mhusika namba moja kama hata haya mambo hayatolei angalau tamko la kusema kuwa waliohusika watapatikana ile watanzania tuwe na amani.
3. Waandishi wanaoandika kuhusu haya mauaji wanapotea.....kisingizio kinachotolewa na wasukuma ( Andrew Chenge, Sirro nk) kuwa wanakimbia familia zao ni ushamba uliokithiri. Ni wasukuma tu wanaokimbia familia zao. Hao watu wamefichwa au wameuawa kama alivyosema Kabudi.
4 Wasanii kama Roma Mkatoliki na wengine wametekwa kwa sababu ndogo tu(Trivial reasons). Rais hajui kuwa taasisi ya rais haina immunity ya kuachwa kusemwa. Kama rais anahangaika na watu wadogo wadogo ni rais wa aina gani huyo? (Rais hana busara amejawa na "tantrums" na "temper"......Mbona ataua wengi tu kwa sababu watanzania wengi ni waelewa siyo watu wa kusifu uongo)
5. Ben Saanane amepotea kwa kutaka kujua kama huyo mheshimiwa amepata hiyo Ph. D yake kihalali maana kila kitu kinamshinda....Inashangaza kiasi kwamba inashusha heshima ya kusoma.
6. Mengi yanayotokea katika utawala wake inaonekana hata kusikitika haoni kama ina maana. Watu wanauawa ovyo au wanatekwa ovyo ovyo mchana mchana na hao usalama wake wa Taifa lakini anaona ni sawa. Kwa jinsi hii utasema yupo safi?
NB: Kuna mengi mabaya anayafanya huyo Magufuli, anataka kujiaminisha kuwa yeye ni Mungu, anaonea watu, anabaka demokrasia kwa kisingizio cha kuleta maendeleo. ....Hiyo si sawa! Na wewe unajinasibu kuwa unaipenda Tanzania wakati unashindwa kukemea mateso wanayoyapata watanzania wenzako?