Uchaguzi 2020 Magufuli: Wapinzani wakishinda watavunja-vunja madaraja na kuuza scraper!

Hizi hoja za maendeleo ya watu au vitu kidogo huwa zinanichanganya, sababu siamini kama kuna maendeleo ya watu bila vitu au maendeleo ya vitu bila watu.
1. Hivi daraja hujengwa kwa ajili ya nani?
2. Ndege hununuliwa kwa ajili ya nani?
2. Umeme ni kwa ajili ya nani?
Labda nimeenda mbali sana.
Hivi unaponunua makochi ndani kwako, vitanda, nguo hivi vyote ni vitu. Lakini vitu hivi ni kwa ajili ya watu. Naamini kwamba tunaposema mtu fulani ameendelea ni pamoja na vitu anavyomiliki.
Nimejiuliza sana kwamba hivi maendeleo ya vitu yakoje? Sanamu huvishwa nguo? Sanamu hupelekwa shule na watu kuachwa nyumbani! Wanasiasa wananichanganya kidogo. Kwa mbali ni kama nimekimbia mada lakini nahitaji msaada.
 
Mkuu inaposemwa maendeleo ya vitu maana yake ni vitu visivyo na tija kwa jamii pana. Mfano unanunua ndege huku sekta ya kilimo iko hoi ambayo ikiboreshwa ingegusa maisha ya zaidi ya 75% ya watz.

Unatengeneza Standard gauge railway, wakati huna volume ya mizigo ya kusafirisha. Ingeanza kuimarishwa sekta ya kilimo(mali ghafi ), kisha uzalishaji (viwanda) na baadae ndio uje kwenye miundombinu.

Watu wanaambiwa uchumi umekua wakati wao hawawezi kumudu hata mahitaji yao ya kawaida ambayo kabla waliyamudu.

Unaamuru miradi ifanywe ambayo bunge halija ridhia maana yake hakukuwa na bajeti yake wala mpango kazi, yaani unatumia fedha za walipa kodi kwa utashi wako na hutaki hiyo miradi hata ikaguliwe.

Matokeo yake, unashindwa kuajiri, huongezi mishahara wala kupandisha madaraja watumishi, unatoa mikopo finyu kwa wanafunzi, hulipi mafao wastaafu, unaua biashara kwa kubambika watu kodi nk nk kisa unafanya miradi uliyojiamlia mwenyewe nyumbani kwako. Hii yote inafanya watu wapoteze ajira, mitaji na vipato vyao hivyo kuathiri maendeleo ya watu.

Kwa kifupi ni kuwa usipopanga vipaumbele vyako kwa usahihi yaani nini kianze kisha nini kifuate unaweza kufanya maendeleo ya vitu yanayo athiri/kukwamisha maendeleo ya watu.
 
Kuna mnyanyembe mmoja alikua amevaa tshirt ya Chadema.aling'oa alama ya barabarani.tulimgongesha kichapo cha kimataifa kisha tukampeleka ngomeni kwa pilato.
Bila picha hainogi! Huu nao ni utopolo Kama wa huyo msingiziaji!
 
"UCHAGUZI WA MWAKA HUU NI MGUMU SANA"BY TUNDU LISU
 
Huenda aliongea kisiasa tu kama utani sidhani kama kuna mpinzani anaweza kuvunja miundombinu hata kuharibu tu hawawezi maana ni watu wenye akili timamu.
 
mzee maghu bwana amenifannya nicheke na kutoa hasira zangu za siku ya leo , binfsi naona siku za kampeni kama zinachelwa ,uchaguzi huu mtam haitasauliaka kamwe da mungu ibarik tz
 
JPM hana muda wa kuongea atawafanyia nini Watanzania, bali ana muda wa kuwatumikia kwa vitendo!
 
Halafu nilimsikia msajili wa vyama vya siasa akiwaeleza wagombea kueleza wao watafanya nini endapo watachaguliwa na si kuwaponda wenzao lakini huyu mchattle anakwenda kinyume mapema mapema sana
Dr Bashiru yeye amefika mbali na kusema eti hao wanaosema kazi na bata wanalala na bata wachafu 🤣🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…