Jamani katika hali ya kawaida ni rahisi zaidi kumtoa Rais madarakani anayemaliza muda wake kikatiba kwa kutumia kura,kuliko Rais aliye tumikia kipindi cha muhula mmoja tu.
Japo upo uwezekano pia wa kumtoa ndani ya mhula mmoja endapo wananchi wataamua iwe hivyo kupitia box la kura.
Sasa najiuliza,kwa kauli ya Rais Magufuli kuwa,Wapinzani wasahau kuitawala nchi hii.Je,Ipi nafasi ya vyama hivi 2020?
Vitaingia kwenye uchaguzi kushindana ili vishinde au kutimiza wajibu?Maana kama ni kusinda washaambiwa wasahau.
Kumbuka na wakati huo ndio utakuwa muhula wa kwanza wa miaka 5 kwa JP umemalizika.Akiwa na muhula mwingine mmoja mkononi,Hivi ikitokea watanzania wakasema kwenye ballot box mzee kapumzike tuangalie na hii timu nyingine,Atakuwa tayari?Ataheshimu maamuzi ya wananchi?
Bado natafakari ile kauli ya wapinzani wasahau,Hivi ilikuwa ya ki siasa au Rais alimanisha?