Unataka kuweka picha kama vile CCM inamilikiwa na mtu binafsi au familia kama chadema, wakati siyo kweli CCM ni Mali ya Watz, ni mtoto wao wamemzaa, wamlea na sasa amekuwa wakati chadema ni mali ya Mtei ameizaa, ameilea na ataamua ni nani amuachie siku zake zikiisha!
Hivyo basi kwa kuwa CCM ni mali ya Watz ina maana Mtz yoyote yule mwenye sifa anaweza kuwa Kiongozi CCM rejea Raisi Magufuli alikuwa Mwalimu tu wa Sekondari leo hii ni Raisi wa nchi ya JMTZ, hata Kikwete mwenyewe hatokei ukoo wa kitajiri na maelite bali ni Mtz wa kawaida ambaye amekulia CCM na leo hii ni Mwenyekiti wa CCM, angalia watu wenye vyeo vikubwa CCM halafu uniambie kama ni maelite kizazi cha ngapi, lkn njoo chadema, nipe stori kama hizo chadema nitajie Viongozi wa chadema ambao ni masikini yaani walioanzia from nothing to the TOP nitajie mmoja TU ili upate uhalali wa kusema CCM wanataka kutawala milele.
Kwa maana kama kuna yoyote yule mwenye kila dalili za udikteta na kujilimbikizia Uongozi na Madaraka ni chadema, Mbowe ni Mwenyekiti wa Chama na pia na Mkuu ya Upinzani Bungeni na Mtoto wa mwanzilishi wa Chama Mzee Mtei yaani kaoa kwa Mtei, sasa ni nani kati ya CCM na chadema wanastahili kuitwa Chama cha kidikteta?
Kama tu Mbowe amekuwa Mwenyekiti wa Chama bila hata ya uchaguzi na ndiyo anaamua nani agombee Uraisi na asingombee je akiwa Raisi wa nchi kuna dalili yoyote ile ya yeye kuachia madaraka?
Ninaweza kukutajia ni lini kutakuwa na Uchaguzi CCM wa kuchagua Mwenyekiti wa Chama nitajie ni lini kutakuwa na Uchaguzi chadema wa kuchagua Mwenyekiti wa chama!
Angalia CCM Kikwete anaaga hivyo anaondoka anaingia mwingine, haya niambie Mbowe anaondoka lini? Ameongoza Chama kilichoshindwa uchaguzi mara tatu, kidemokrasia Dunia nzima Viongozi hujiuzulu punde chama wanachokiongoza kinaposhindwa sasa Mbowe kashindwa mara tatu na bado leo hii anasimamisha makende yake Bungeni eti anaunda Baraza la Mawaziri Kivuli, analipi jipya? Ni nani dikteta kati ya CCM na chadema?
Angalia Uongozi wa CCM ni sura ya Watz wa nchi nzima, Kikwete anatoka Bagamoyo, Kinana - Arusha, Nape - Mtwara/Lindi, mwingine Iringa ukija kwenye Halmshauri Kuu ya CCM ni sura ya nchi nzima sasa njoo chadema nitajie viongozi wake na wanatoka wapi?
Asilimia zaidi 85 ya viongozi wanatoka eneo ambalo halifikishi hata asilimia 10% ya WatanZania wote halafu unathubutu kuita CCM Chama cha kidekta? Kuna udikteta zaidi ya chadema?