mkuu nimetamani kujua mood yako ilikuwaje wakati unaandika hii comment....maana duh!!
Humu watu wana Joto na hasira na maisha yao, mtu ana aamka saa 11 Alfajir anagombea daladala kurudi saa2 usiku na degree yake afu mshahara laki4 ataacha kumchukia mtu bila sababu kweli aliyeishia O level?
Hembu waulize sababu hasa wanayo mchukia huyo Diamond kama wanayo basi, sana sana watakuambia ana Show off? Ha ha ha ha Jealous bana!!
Do not judge a book by its cover judge what is inside umejua kuwa ni chuki kisa wana comment usichotaka all in all education is the key ya maisha hayo mengine maneno ya kujifariji
Mfano wewe hebu niambie unachomchukia ni nini? Yeah i know, education is the key lakini pia inauma kuona mtu hajasoma afu amekupiga bao kwa mafanikio ili hali mtu umesotea miaka nenda Rudi.
Yule msanii anayesemekana kuwa ni bilionea kuliko msanii mwingine yeyote Tanzania ambaye pia ameanza kujenga hekalu lake huku likiwa halijakamilika kwa mvua tatu sasa (miaka mitatu), ambaye pia amekuwa akiwafunika wasanii wote wa Tanzania kwa shoo kali na ghali, ambaye pia amekuwa akiombwa namba za simu pamoja na collabo na wasanii wa Marekani akiwemo Chriss Breezy mkali wa so cold na with you bila kusahau forever, lakini yeye huwakatalia kutoa namba na collabo kwa sababu ni mkali mno.
Msanii ambaye vilevile Mbeya nzima hakuna Hotel ya kulala yeye wakati huo huo amepanga magheto mawili yenye price ya thirty five thousands huko maeneo ya Sinza, sasa mashabiki kama si wa Keko, Ukonga au Segerea, nyimbo kama kamwambie, my number one na kitorondo hazitakuwa ngeni masikioni mwao kwa sababu burudani hiyo mujarabu watakuwa wakiipata face to face tena bure kabisa kutoka kwa Diamond kwa sababu sasa atakuwa akilala na kuamkia jela kwa kwa fifteen years period na hata uji wa mahindi wa kesho uliowekwa chumvi ataanza kuuupata huko na kama hili litafanyika, basi atatoka akiwa na umri wa January Makamba.
Hii imetokana na msanii huyo nguli kabisa kutinga gwanda za kijeda na kukatia miuno jukwaani wakati wa shoo fiesta mwishoni mwa wiki jana.
Pamoja na mbwembwe hizo, mashabiki walionekana kumzomea na kutaja jina la mfalme Kiba mzee wa cinderela macmuga na mwana.
Kwa mujibu wa magazeti, inasemekana jamaa zake wa karibu walimwambia kuhusu hizo gwanda lakini alitia ngumu.
Kwa undani wa habari hizi jisomee gazeti la leo la lete mambo na Visa.
una lako jambo.
1. Kwani ni wongo kama ndoma hana mjengo mkubwa kabisa wenye swimming pool unaogoma kumalizika hadi leo?
2. Je ni uongo kuwa ma pro wake akina hod wamekuwa hawaji hapa na kusema ndomo ameombwa namba za simu na lundo la wasanii wa marekani kama akina chris lakini amekuwa akiwakatalia.
3. Je ni uongo kuwa pro wake huwa hasemi kuwa bosi wake ndomo ndio msanii ghali afrika mashariki?
4. Je ni uongo kuwa mbeya nzima hakuna hoteli ya kulala msanii wenu kwa sababu ya hadhi yake?
5. Je si kweli kuwa domo alisema atamsaidia mfalme wa tanzania kimziki ali kiba eti akihitaji collabo lakini sisi tukamwonesha yeye ni nani na kiba ni nani katika tanzania hii tena mbele ya swahiba wake davido na ti!
Ujinga kweli umejaa
T.I aliyekuja juzi mkajazana nae umejiuliza alienda jela mara ngapi na bado hao wakamuita kuja kutumbuiza, mboa hawakuita wengine wengi huko.
so jua jela haimmaliziii mtu au kumuulia nyota ukiwa nayo unayooooooooooo
wivuweye.com
Ha ha ha ha uzi umenichekesha sana wamsamehe tu bure kijana wa watu mana amekuwa na gundu tangia u Germany Uk na fiesta watampa pressure bora wamrushe kichura au wampigishe mbizi ili aendeleze gurudumu la mziki wakimfunga hatutaskia vitorondo tena