Mahad Nur: Msomalia Wa City Mall na Victoria Plaza, Vijana wa Kitanzania tuko wapi?

This is one of Hard working family na wametumia vizuri opportunities walizopata. Mzee wao alikuwa mpambanaji sana na alitumia kila nafasi aliyopata zuri/mbaya kutengeneza pesa ,sasa anakula pension yake huko watoto waki-takeover .
 

Yeah, smart people use other people money to make money.
 

Mkuu nimecheka sana.....eti MV. LIEMBA hadi Marekani!😀😀😀
 
Huyo mwenye paradise ndio baba wa hawa vijana mkuu.
 
Watu wengi wenye maono uwezi kumkuta anafatilia ishu ndogo ndogo kama taarifa mshenzi za kina ITV,TBC, clouds TV, azam TV na nyinginezo unakuta MTU anaangalia business news za Blomberg, BBC business news, CGTN business news, Fox Business news na Discovery news na kuna Fox F1 news uko ndio ipo dunia na telaviv technology na California technology uko ndio ipo dunia na sio ivi ivi vichanel vya ndani vinatengeneza mauzui ya kipuuuzi puuzi
 

Hahahahhaa, haya endelea kusubiria haki yako ya kupewa pesa na kaka yako, ujamaa ni ujuha wa zamani.....bdala ya kukaza msuli unapiga story nyiiingi na kuwalaumu wenyenacho.
 
Vijana wa Tanzania acheni kuangalia huyu ana nini yule ana nini! tumieni ubongo wenu kuwa wajasiriamali! hawa lazima walianza chini mpaka wakafika hapa!

Tanzania ni nchi ilobarikiwa na rasilimali nyingi sana tumieni rasilimali zenu mtafanikiwa!
Rasilimali zipi? Izi ambazo wanasema aridhi ni Mali ya serikali au?
 
Litapwasi ndio wapi?
Huku ndanindani ukivuka Mtakanini unaingia kushoto unapandisha Kilimasela, ukishuka unavuka Mtombawala, unaacha gari unachukua pikipiki kutoka Mwashegeshi mpaka Njiapanda ya Mwabusalu, hapo sasa pikipiki haivuki unachukua basikeli mpaka Bhusangu, unavuka pori la akiba Maswa, baada ya hapo hata baiskeli haipiti unatembea kwa mguu mpaka Litapwasi, siyo mbali sana, ni kama kutoka hapa mpaka Bangwe.
 
sisi network zetu za nje ni za kutumiana Latest Smartphone na Story za Kina Rick Ross!
Watanzania tunapagawa na vitu kama smartphone, Facebook, WhatsApp, Instagram, jamii forum, Siasa na mipira, kubeti
Wenzetu hawana upuuuzi wa kudata na upuuuzi huo,
 
Nakupa big up boss wangu. Umeongea point kubwa sana, ndugu yangu
 
Watanzania hawana Backup huko nje?.
Unawazungumzia watanzania ambao ndugu zao, wakiwa njee wakiwapa misaada ufanyia matanuzi baada ya kuwekeza. Unakuta MTU anatoa Pesa ajenge nyumba akirudi ni kituko
 
Hahahahhaa, haya endelea kusubiria haki yako ya kupewa pesa na kaka yako, ujamaa ni ujuha wa zamani.....bdala ya kukaza msuli unapiga story nyiiingi na kuwalaumu wenyenacho.
Naona unanisoma tu hili u reply wala sio kuelewa, ni wapi nimesema kwamba mimi nimekaa tu nasubiri msaada? Hujaona sehemu nimekwambia hadi mimi kufikia hatua ya kumpigia hodi my bro ilikuwa ni baada ya jitihada zangu binafsi kukwama?

Kwa hizi comments zako natumai wewe ni mtu mwenye mafanikio sana na katika safari yako hujawahi kusaidiwa hata kidogo katika maisha yako na ndio maana unaniona mimi wa maajabu. Ni kweli ujamaa ni mfumo wa kizamani kwenye mazingira sahihi ambayo ni rafiki na mifumo mingine tofauti na ujamaa.
 
Haya shukrani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…