Mahad Nur: Msomalia Wa City Mall na Victoria Plaza, Vijana wa Kitanzania tuko wapi?

Mahad Nur: Msomalia Wa City Mall na Victoria Plaza, Vijana wa Kitanzania tuko wapi?

This is one of Hard working family na wametumia vizuri opportunities walizopata. Mzee wao alikuwa mpambanaji sana na alitumia kila nafasi aliyopata zuri/mbaya kutengeneza pesa ,sasa anakula pension yake huko watoto waki-takeover .
 
yeah,mwekezaji mzuri ni yule anaetumia pesa za watu kuwekeza na sio zake,
kuna kitabu kimoja cha Sydeney sheldon,Rising of the star kama sikosei,
kuna kabinti kanaitwa Lara,
kanaishi na mamake nyumba ya kupanga,maisha yao ya hali chini mno,
baba mwenye nyumba daily kuwadai pango,
so mwenye nyumba kaamua kuuza nyumba ile,ilikuwa imechoka choka,
yule binti kumbe uwekezaji umo damuni,
akamfuata huyo baba na kumwambia anataka kuinunua nyumba,hapo hana hata senti,
yule mzee akacheka,wewe binti una hela ya kununua nyumba wewe,

binti kakomaa,na alikuwa chombo sana,huyo mzee kabla alimtongoza na akamtolea nje,

mwenye nyumba kufupisha akakubali kumuuzia,
sasa anaomba pesa ,badala yake binti anamwambia ntakulipa baada ya kuifanyia renovation,

baada ya ubishani sana,mzee akakubali,
binti akasema kwa sasa naomba mkopo nitaulipa with interest ili nipate pesa ya kufanya ukarabati,
mwenye nyumba katoa jicho kwa mshangao,lakini binti alikuwa negotiator mzuri,hatimae mzee kakubali,akatoa mkopo kwa colateral ya nyumba ileile anayouza na ambayo hajalipwa pesa,
binti kakarabati nyumba vedeadly,

akaja kuuza mara tatu ya bei ya nyumba,akalipa pesa ya kununua nyumba,akalipa mkopo na akabaki na pesa nyingi tu,
sasa ndo akaingia rasmi kwenye Reale estate,
ananunua nyumba mbovu anakarabati na kusukuma kwa bei juu,
akawa bilionea mkubwa,akahama soza africa na kwenda New york,
sasa ananua nyumba Manhatan na kurenavate na kuuza ama kupangisha,
akawa na maskyscrapper Canada,London etc.

Hii ni novel tu, but very inspiring ukiisoma

Yeah, smart people use other people money to make money.
 
Wasomali hawana kodi kama huku dubai hawana ushuru wowote wa port.huwa wanakuja na meli zao chakavu wanapakia bidhaa kiasi wanachohitaji bila kodi aina yoyote(exempted)kisha wanaondoka!
Jamaa wana roho ngumu wale wanaweza kusafiri na MV LIEMBA hadi marekani.

Mkuu nimecheka sana.....eti MV. LIEMBA hadi Marekani!😀😀😀
 
Wasomali kuna watu naona hawawaelewi vzuri wasomali kwa Money laundry wako vzuri sana
Hela chafu wanayoipata wanajua wapi pa kuipeleka na kuinvest au kuwapa wasomali wenzao walipo Sehemu fulani wanampa na anaifanyia kitu fulani.....
Syo mitanzania utakufa lijitu linakwiba mihela anakuwa na mabilion Hata kuwapa watu wengine awekeze hataki wasomali wao kwa Syo wachoyo ........
Hata yule msomali aliyekuwa anamikiki paradise alikimbiaaa somali kitambo akajaga Bongo na hela zake akawekeza na bado somali alikuwa n'a mtandao fulani hko
Mtanzania sahv unaweza ukawa n'a mipango mizuri ya kufanya na unahitaji cash lakini Nenda bank uone Nenda kakope uone bullshyt huko ukatako kutano nazoooo utakimbiaaa

Wasomali ni namba nyingine Syo kama Sisi Acha Sisi tuendeleee kubaniana tu

Ova
Huyo mwenye paradise ndio baba wa hawa vijana mkuu.
 
Hakuna utekaji meli sikuhizi,kuna patrol za kutosha,
jamaa wana akili kubwa wale,
ukiwakuta wanapiga story ndo utaona tofauti yao na sisi,
wanaongelea mambo makubwa ,ishu za mbele,
jamaawanaweza kukesha usiku kucha na asubuhi ukawakuta kama ulivyowaacha saa nane za usiku ukienda kulala,
mradi pawepo na coca baridi,miraa na Tv,
hawaangalii sijui ITV,STARTV,
wanaangalia discovery,series za law etc
Watu wengi wenye maono uwezi kumkuta anafatilia ishu ndogo ndogo kama taarifa mshenzi za kina ITV,TBC, clouds TV, azam TV na nyinginezo unakuta MTU anaangalia business news za Blomberg, BBC business news, CGTN business news, Fox Business news na Discovery news na kuna Fox F1 news uko ndio ipo dunia na telaviv technology na California technology uko ndio ipo dunia na sio ivi ivi vichanel vya ndani vinatengeneza mauzui ya kipuuuzi puuzi
 
Wala hata sio kubiashana, nilikuwa nakurekebisha tu hapo ulipo danganya hili kujustify unachokiamini, bado nakukatalia kabisa kwenye suala la kupata starting points wahindi huwezi ukawalinganisha na mbongo wao wana privileges. Mbali na kusaidiwa kazi yenye maslahi ya kiupendeleo unafahamu mashariti rahisi yaliyopo kwenye hizi benki zao ambazo ziko diaspora chini ya diaspora community OCI(Oversees Citizen of India)? Wewe unafikiri huwa wanaambiwa eti kupata mkopo ni hadi awe na nyumba pamoja na biashara ya miaka miwili??? Muhindi ana privileges wewe sema hapo kwenye nidhamu ukilinganisha na mbongo nnakukubalia.

Kuhusu huyo kaka yangu hakupewa mtaji wowote kwanini yeye alimaliza tu masomo ya juu akapata ajira miezi michache baadae! Ni kipindi ambacho tatizo la ajira lilikuwa bado halijawa sugu kama ilivyo sasa hivi. Binafsi naona Nina haki ya kusaidiwa na yeye sababu ni mwana ukoo mwenzangu na Niko kwenye hali ambayo inahitaji msaada. Na ninaamini endapo kama atanisaidia atakuwa amenisaidia sio tu mimi bali ukoo mzima kwa ujumla wakiwemo watoto wake.

Inaonekana wewe ni muhumini mzuri wa mfumo wa maisha ya kibepari. Hilo linawezekana palipo na msingi mzuri na mazingira ya nchi nzima kwa ujumla sio kwa Tanzania hii ambayo juzi hii nimeskia kati ya 100 ni watu 8 tu ndio wana uwezo wa kujitegemea. Na pia unemployment inatisha sana wala hakuna mipango thabiti ya kukabiliana nayo zaidi ya kejeri tu za wana siasa kuwaita wanainchi wao wavivu

Hahahahhaa, haya endelea kusubiria haki yako ya kupewa pesa na kaka yako, ujamaa ni ujuha wa zamani.....bdala ya kukaza msuli unapiga story nyiiingi na kuwalaumu wenyenacho.
 
Vijana wa Tanzania acheni kuangalia huyu ana nini yule ana nini! tumieni ubongo wenu kuwa wajasiriamali! hawa lazima walianza chini mpaka wakafika hapa!

Tanzania ni nchi ilobarikiwa na rasilimali nyingi sana tumieni rasilimali zenu mtafanikiwa!
Rasilimali zipi? Izi ambazo wanasema aridhi ni Mali ya serikali au?
 
Litapwasi ndio wapi?
Huku ndanindani ukivuka Mtakanini unaingia kushoto unapandisha Kilimasela, ukishuka unavuka Mtombawala, unaacha gari unachukua pikipiki kutoka Mwashegeshi mpaka Njiapanda ya Mwabusalu, hapo sasa pikipiki haivuki unachukua basikeli mpaka Bhusangu, unavuka pori la akiba Maswa, baada ya hapo hata baiskeli haipiti unatembea kwa mguu mpaka Litapwasi, siyo mbali sana, ni kama kutoka hapa mpaka Bangwe.
 
sisi network zetu za nje ni za kutumiana Latest Smartphone na Story za Kina Rick Ross!
Watanzania tunapagawa na vitu kama smartphone, Facebook, WhatsApp, Instagram, jamii forum, Siasa na mipira, kubeti
Wenzetu hawana upuuuzi wa kudata na upuuuzi huo,
 
Wale woote ambao wako chini ya miaka 40, mjitahidi kufanya set-up ya kibiashara ili familia baadaye ziwe na family business na sio kupiga blah blah hapa..
Ukimsikiliza jamaa anaeleza kabisa walikuwa na business Mogadishu kabla ya vita na ilikuwa furniture business na material walitoa Tanzania, hii ilikuwa family business ya baba zao au babu zao kutokea hapo ndio set-up ilifanyika..

"Tanzania is blessed"
Nakupa big up boss wangu. Umeongea point kubwa sana, ndugu yangu
 
Watanzania hawana Backup huko nje?.
Unawazungumzia watanzania ambao ndugu zao, wakiwa njee wakiwapa misaada ufanyia matanuzi baada ya kuwekeza. Unakuta MTU anatoa Pesa ajenge nyumba akirudi ni kituko
 
Hahahahhaa, haya endelea kusubiria haki yako ya kupewa pesa na kaka yako, ujamaa ni ujuha wa zamani.....bdala ya kukaza msuli unapiga story nyiiingi na kuwalaumu wenyenacho.
Naona unanisoma tu hili u reply wala sio kuelewa, ni wapi nimesema kwamba mimi nimekaa tu nasubiri msaada? Hujaona sehemu nimekwambia hadi mimi kufikia hatua ya kumpigia hodi my bro ilikuwa ni baada ya jitihada zangu binafsi kukwama?

Kwa hizi comments zako natumai wewe ni mtu mwenye mafanikio sana na katika safari yako hujawahi kusaidiwa hata kidogo katika maisha yako na ndio maana unaniona mimi wa maajabu. Ni kweli ujamaa ni mfumo wa kizamani kwenye mazingira sahihi ambayo ni rafiki na mifumo mingine tofauti na ujamaa.
 
Huku ndanindani ukivuka Mtakanini unaingia kushoto unapandisha Kilimasela, ukishuka unavuka Mtombawala, unaacha gari unachukua pikipiki kutoka Mwashegeshi mpaka Njiapanda ya Mwabusalu, hapo sasa pikipiki haivuki unachukua basikeli mpaka Bhusangu, unavuka pori la akiba Maswa, baada ya hapo hata baiskeli haipiti unatembea kwa mguu mpaka Litapwasi, siyo mbali sana, ni kama kutoka hapa mpaka Bangwe.
Haya shukrani
 
Back
Top Bottom