Wasomali wanapiga kazi balaa, kuna mama bilioner wa kisomali kawekeza Kenya shida tupu, sasa hivi anajenga kiwanda cha sukari uganda analima miwa kijiji hapo uganda kwa ajili ya kiwanda chake..
Vijana wa bongo wanapo nikasirisha ni kujifariji kwa maneno ya kipumbavu, watakwambia hao vijana walikuwa mapirates,
Hakuna mwekezaji anae kuja nchini kwako na hela kwenye mabegi hela zote wanazichukua kwenye mabenk yenu ya ndani...
Vijana waache wasubirie ajira za magufuli na kushinda kwenye vijiwe vya siasa na magrup ya whatsapp,
Tanzania atafika siku 96% ya uchumi wa Tanzania utashikwa na raia wa kigeni
yeah,mwekezaji mzuri ni yule anaetumia pesa za watu kuwekeza na sio zake,
kuna kitabu kimoja cha Sydeney sheldon,Rising of the star kama sikosei,
kuna kabinti kanaitwa Lara,
kanaishi na mamake nyumba ya kupanga,maisha yao ya hali chini mno,
baba mwenye nyumba daily kuwadai pango,
so mwenye nyumba kaamua kuuza nyumba ile,ilikuwa imechoka choka,
yule binti kumbe uwekezaji umo damuni,
akamfuata huyo baba na kumwambia anataka kuinunua nyumba,hapo hana hata senti,
yule mzee akacheka,wewe binti una hela ya kununua nyumba wewe,
binti kakomaa,na alikuwa chombo sana,huyo mzee kabla alimtongoza na akamtolea nje,
mwenye nyumba kufupisha akakubali kumuuzia,
sasa anaomba pesa ,badala yake binti anamwambia ntakulipa baada ya kuifanyia renovation,
baada ya ubishani sana,mzee akakubali,
binti akasema kwa sasa naomba mkopo nitaulipa with interest ili nipate pesa ya kufanya ukarabati,
mwenye nyumba katoa jicho kwa mshangao,lakini binti alikuwa negotiator mzuri,hatimae mzee kakubali,akatoa mkopo kwa colateral ya nyumba ileile anayouza na ambayo hajalipwa pesa,
binti kakarabati nyumba vedeadly,
akaja kuuza mara tatu ya bei ya nyumba,akalipa pesa ya kununua nyumba,akalipa mkopo na akabaki na pesa nyingi tu,
sasa ndo akaingia rasmi kwenye Reale estate,
ananunua nyumba mbovu anakarabati na kusukuma kwa bei juu,
akawa bilionea mkubwa,akahama soza africa na kwenda New york,
sasa ananua nyumba Manhatan na kurenavate na kuuza ama kupangisha,
akawa na maskyscrapper Canada,London etc.
Hii ni novel tu,but very inspiring ukiisoma