Mahad Nur: Msomalia Wa City Mall na Victoria Plaza, Vijana wa Kitanzania tuko wapi?

Mahad Nur: Msomalia Wa City Mall na Victoria Plaza, Vijana wa Kitanzania tuko wapi?

Tembea maeneo yote ya starehe alafu angalia wasomali utawakuta wangapi baada ya hapo ndio utapata jibu kwa nini hawa watu wanatusua kuliko sisi!
Starehe ni sehemu ya maisha ya binadamu aliyefanikiwa kiuchumi &kiroho .....

.... km hufanyi starehe yoyote means umefanikiwa kiuchumi tu , kiroho bado ni fukara/masikini kupita kiasi + your life is meaningless.
 
Ila Kuna kingine pia nimegundua kwamba ukitoka nje ya nchi yako unakuwa na exposure na added advantages nyingi either iwe kibiashara au kikazi kuliko ukiwa ndani ya nchi yako otherwise labda uwe fisadi au tapeli.
Ndani ya nchi yako kadri unavyozidi kuwa great thinker na kuthink nje ya box ndio kadri unavyozidi kugundua weaknesses za systems zetu na kuface barriers/hardship.
Hii kitu nimejifunza imagine Kuna kipindi nilitoka nikaajiriwa nchi jirani just kwa junior/middle level.
Maisha niliyoishi kule ni ya kifahari sana kwani nilikuwa nikienda napewa nyumba au kulipiwa hotel uzunguni na pia naendeshwa kwenye landcruiser hata nikienda saloon kunyoa,mshahara mzuri na posho za kutosha hadi zingine unazisahau kwenye akaunti.
Lakini kwa level hyo hyo nikija kufanyia kazi huku bongo naonekana kapuku tu hata vitz ya kutembelea sipewi nagombea daladala Kama za mbagala.

Ni kweli kabisa unavyosema kwani dunia nzima na kila nchi ukiangalia matajiri wakubwa ni foreigners
Kwani zaidi ya biashara hawawezi kupasua
Ukiangalia foreigner hawezi kuja na kutafuta kazi serikalini au kuingia siasa maana inakuwa ngumu sana ku integrate
Lakini akipika chakula chao na kuuza lazima mtakipenda kwani hamkijui na ni kipya kwenu

Pia biashara wanaona opportunities nyingi ambazo wazawa hawazioni au hazipo kabisa na wao wanazianzisha

Kingine wengi wanajipa misaada ya hali na mali na wanakuwa na communities zao za kupanga mikakati ya kibiashara
 
Starehe ni sehemu ya maisha ya binadamu aliyefanikiwa kiuchumi &kiroho .....

.... km hufanyi starehe yoyote means umefanikiwa kiuchumi tu , kiroho bado ni fukara/masikini kupita kiasi + your life is meaningless.
Inategemea ni Starehe zipi! Ninazozungumzia mimi ni hizi Starehe za Kipuuzi.
 
watu wanahela alafu wanaenda somalia kwenye vita vya enzi na enzi,,,,!!
Kama ndugu si watawasalimia tu hata kwa simu.
Yani kabisa wanatoka pepo ya amani TZ wanaenda huko somalia,
kama kutembea si wanahela wangeenda hata states au paris,wakale bata huko,
Mwenyezimungu awarehemu.
Uyo Mahad ana kaka yake anaitwa Mohamed Nur aligombèa uraisi uko somalia na ànaishi hapa TZ amewekeza hapa ana kampun yaķe pale Airport cargö terminal. Hawa jamaa wanaspirit na asīli ingawa nchi yao haieleweki
 
Waswahili hamkosi sababu, Wasomali Kokote waliko na utakapowakuta ni wapiganaji.. kama ulikuwa hujui hata Europe na USA hadi Canada Wanakimbiza sana kwenye Biashara
Nmekaa nao Sana ndola
Mm nawajua in & out
Magumashi kwao lazima
Huko kote uliposema huwezi ona huasilia wao...
Ila nawasifu kwa kupeana michongo wao kwa wao

Ova
 
Network
Network
Network
Hawa jamaa wana network kali saana
msomali wa ilala leo ana network ya wasomali wenzie wa nje zaidi ya nchi 20 so wana Import BUSINESS IDEAS always money comes from ideas and experience
tofauti na mswahili wa kisukuma ana wivu kuvunjia wenzake nyumba na kutaka waishi kama mashetani
 
Akili za wabongo zitaishia kusema wanapata fedha kutokana na ugaidi au pirates hatuendi mbali zaidi ya hapo na hapo ndipo wenzetu wanapotuacha, fursa zipo nyingi ila hatuzioni wao wanakuja kutoka kwao kwenye matatizo wanapofika huku wanapiga fedha tu.

Masikini nao wanamaneno ya kujifariji ili waonekane wema ndio maana hawajawa matajiri. Basi imani yao wanawaambukiza na wengine ndio maana idadi ya masikni ni wengi.
 
Baada ya kuangalia documentary hii ya kijana huyu wa kisomalia Mahad Nur na ndugu yake Mohamed Nur, wanaomiliki City Mall , Victoria Plaza na Africa flight Service, a cargo company , nimejiuliza inakuwaje vijana wa kisomalia kama hawa wanatoka mogadishu wanakuja na kufanikiwa hapa hapa kiasi hiki lakini sisi tupo tu wala hatuzioni hizi fursa sana sana , vijana wamebaki kusubiria ajira.

Kweli hii ni changammoto kubwa sana kwa nchi yetu.

Tusaidiane mawazo



Mtaji baba.
Unajua US walipo saidia kumpindua Rais wa Somalia Siad Barre,Uongozi uliparaganyika kwani utawala mpya haukutilia maanani baadhi ya clans kwenye uongozi. Rais Barre katika uongozi wake alihakikisha umuhimu wa kila clan unatiliwa maanani. Somalia bila kuzingatia hili nchi hiyo haitawaliki. Matokeo yake iligubikwa na ugomvi mkubwa kati ya hizi clans na kuanza kupigana wenyewe kwa wenyewe.
Matokeo hayo yalisababisha wasomali wengi wenye uwezo kukimbilia ulaya pamoja na familia zao kama wakimbizi. Watoto wa wakimbizi hao ambao wamepata elimu nzuri tu walijaribu kurudi nyumbani na kuwekeza lakini hali ya usalama iliwakimbiza.
Wenzetu hawa wana clan system kama wahindi ambapo wanasaidiana sana kupitia mfumo wa hawala ambapo mtu anasaidiwa mtaji na clan nzima ambapo baadaye kulipa naye inabidi asaidie wenzake kwenye clan yao kimtaji.
Baadhi ya clan, zilifaidika sana na ndugu zao walio somalia waliokuwa wanapata pesa nyingi baada ya kuteka meli za mafuta na mizigo kwenye pwani yao. Pesa hizi pia zilizunguka kwenye mtindo huo. Siri ya kuendelea ni kusaidia wengine kwenye clan popote pale walipo.
 
Katika maisha ya sasa jitahidi uwe wa mwisho kuamini. Kwani hata dunia imebaki kipande, there is a secret of unknown.
 
Back
Top Bottom