Father of All
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 7,672
- 9,039
Bila ushabiki. Kama ungeulizwa nini ushauri wako kwa mama kuhusiana mzozo wa bandari ambao mahakama kuu ilitolea uamuzi? Je, unashauri tuendelee hivi au tukate rufaa?
Je, akili na nguvu vinavyotumika kuhakikisha hii kitu inafanikiwa zinaonyesha maanguko au mafanikio huko tuendako hasa ikizingatiwa kuwa, kama taifa, tuna uzoefu mbaya na mikataba kama tutajikumbusha tulivyopigwa kwenye karibu mikataba yote iliyoingiwa baada ya Mwalimu Kambarage kuachia ngazi?
Ngoja Baba yenu nianze kumpasha mama yenu. Bi Mkubwa, kwa mwendo huu hatufiki. Kumbuka. Maulaji yana mwisho. Wakati mwingine ukiupiga mwingi, mwisho unaweza kuwa shubiri. Chonde chonde, mama punguza spiidi. Wasikilize hawa wenye nchi uliyopata baada ya waliyemchgua hata kama ni kwa kuchakachua kurudisha namba.
Je, nani hatakufa? Wayajua ya kesho? Waachie wenye bandari waamue badala ya kuwabambikizia maamuzi hata kesi binti yangu.
Sema na mama. Mwambie kupitia uzi huu unachotaka kumwambia mama bila woga wala kumung'unya maneno.