Nuel27
JF-Expert Member
- Jul 3, 2026
- 461
- 915
Kiongozi Mstaafu wa Chama cha ACT-Wazalendo na Mrufani katika shauri la Kikatiba dhidi ya Serikali, Zitto Zuberi Kabwe, ametoa tamko zito akisikitishwa na hatua ya Mahakama ya Rufani ghafla kusita kumpa nafuu stahiki aliyekuwa CAG, Prof. Mussa Juma Assad, licha ya kuthibitisha rasmi kuwa aliondolewa madarakani kinyume cha Katiba.
Katika tamko rasmi alilolitoa leo, Oktoba 7, 2026, jijini Dar es Salaam, Zitto amebainisha kuwa ingawa Mahakama imetangaza Kifungu cha 6(1) cha Sheria ya Ukaguzi wa Umma (PAA) kuwa batili na kinyume cha Ibara ya 144(1) ya Katiba, imeshindwa kutoa amri ya kumrejesha Prof. Assad kazini au kumpa fidia.
Zitto ameeleza kuwa utenguaji wa Prof. Assad uliotokea Novemba 3, 2019 kwa mgongo wa kuisha kwa muda wa miaka mitano ulikuwa haramu, kwani Katiba inaruhusu CAG kuondolewa kabla ya miaka 65 kwa njia ya Tume Maalum (Tribunal) pekee. Hata hivyo, Mahakama imesita kuchukua hatua za kurekebisha madhara hayo.
"Naiheshimu Mahakama, lakini sikubaliani na uamuzi wake kuhusu nafuu. Kwa mtazamo wangu, kuitetea Katiba kunapaswa pia kujumuisha kurekebisha madhara yanayotokana na ukiukwaji wake. Mahakama imeogopa kuwaadhibu wanaovunja Katiba na imeona aibu kumlinda Prof. Assad," alisema Zitto.
Mwanasiasa huyo aliongeza kuwa Mahakama ilikataa kumrejesha Prof. Assad kwa hofu ya kutengeneza ombwe la kiongozi na aliyemrithi, huku pia ikikataa kutoa fidia kwa kuzingatia kuwa shauri hilo lilikuwa la kikatiba linalogusa wadhifa wa umma na sio mgogoro binafsi wa ajira.
hii inawalinda watakaoshika nafasi hiyo baadaye, lakini haijatoa suluhisho kwa madhara aliyopata Profesa Assad. Hilo bado ni jambo linalotia wasiwasi mkubwa," alisisitiza.
Hata hivyo, Zitto ameweka wazi kuwa msimamo mkuu wa Kikatiba sasa uko wazi na unalinda Ofisi ya CAG dhidi ya kuingiliwa na Mamlaka ya Uteuzi au Bunge, kwani CAG anakagua fedha za umma kwa niaba ya wananchi na anahitaji uhuru kamili.
Akimalizia tamko lake, Zitto ameeleza kuwa timu yake ya mawakili inaendelea kufanya tathmini ya kina ya hukumu hiyo ili kuchukua hatua za ziada za kisheria zitakazohakikisha haki inatendeka kikamilifu.