seedfarm
JF-Expert Member
- Feb 9, 2020
- 260
- 2,655
Mahakama kanda ya Arusha jumatano oktoba 27, 2021 imekubali kupokea kielelezo namba 4 kama ushahidi toka kwa Afisa tehema wa CRDB tawi la kwa Mrombo bwana Geoffrey Abimiel Nko ambaye ni shahidi namba saba wa Jamuhuri Katika kesi ya uhujumu Uchumi inayomkabili Lengai Ole Sabaya.
Francis Mrosso analalamika kuwa aliporwa pesa zake alizotoa toka Bank ya CRDB tawi la kwa Mrombo huku wasaidizi wa Sabaya walisubiri mzigo huo wa pesa hapo Bank.
Hakimu mkazi wa kanda ya Arusha Bwana Kisinda alipinga pingamiza lililoletwa na upande wa utetezi wa Sabaya kuwa halina mashiko, Ambapo wakili wa Sabaya aliomba mahakama taarifa ya CCTV isitumike mahakamani kwa kuwa haina ubora na inaonyesha picha hafifu.
CCTV camera hiyo ilichukuliwa January 22 mwaka huu kuanzia 4:09 jioni mpaka saa 5:05 jioni ikionyesha Vijana wa Sabaya wakizikwapua pesa toka kwa Bwana Francis Mrosso hapo kwa Mrombo tawi la CRDB.