Mahakama Kuu Divisheni ya Uhujumu Uchumi na Rushwa yatupilia mbali mapingamizi 2 kesi ndogo ya Mbowe na Wenzake. Jaji Siyani ajitoa kuendelea na kesi

Majaji wengi wataikimbia hii kesi maana ni ya kubumba, ila serekali inalazimisha hukumu isiyo ya haki ili kufuta aibu ya kusema uongo. Tatizo kila jaji anajua atatoa hukumu isiyoendana na ushahidi, hivyo inabidi wajitoe kuepuka lawama, na wakati huo huo kulinda mlo.
 
Mbona kwa sabaya ulikuwa unashangilia?
Hawa ni wakupuuza tu,
Kwa Sabaya mahakama imetenda haki. Kwa Mbowe mahakama haitendi haki.
Wanapenda wayatakayo wao ndio yatokee nje na hapo hakuna haki.
Wao ndio mizani ya haki!
 
Na usithubutu kabisaaah, hata Baba D mwambie asithubutu maana utaishi maisha ya roho juu juu Kama sio kuokota maiti ya mumeo ikielea katika moja ya mito maarufu hapa nchini!

Fanya maisha yako, tunza familia yako, toa maoni yako kwa kile unachoamini bila presha usije kujiumiza

Hapo maisha yanakua powa sana
 
Kukubaliwa au kutokubaliwa kwa maelezo ya watuhumiwa na mahakama kuna nafasi kubwa kwenye kuamua kama hukumu ya mwisho itakuwa ya haki au isiyo ya haki.

- Jaji ametoa hukumu kwa kutumia maoni yake.

..hata mimi naona hii ni habari mbaya kwa upande wa utetezi.
 
Soma vizuri hints za hukumu yake. Amenukuu vifungu vya 50(2) na 51 vinavyotoa exemptions juu ya masaa 4 ya kuchukua maelezo ya mtuhumiwa. Mambo ya sheria hayataki mahaba. Baki na mahaba yako na Mbowe lakini sheria itendee haki.
jaji: Kwa Upande wangu naona kuwa Ucheleweshaji katika Shauri hili palikuwa na Sababu, Matakwa ya Sheria yalikuwa yamezingatiwa.

Muda wa Masaa Manne hautojumuishwa kwa sababu za Usafirishaji.

Kwa hiyo walikamatwa tarehe 5 wakahojiwa tarehe 7, na jaji anaona masaa 48 kutoa 4 unabaki na masaa 44 ambayo ndiyo muda wa kumsafirisha mtu kutoka Moshi hadi dsm? Tena kwa gari la serikali siyo public transport.
Kwa kuwa ni maoni yake, tuyaheshimu, kwenye rufaa anaweza jaji mwingine akawa na maoni tofauti
 
Tenda haki. Amezungumzia pia muda uliotumika kumtafuta mtuhumiwa mwingine. Kutumia 'maneno maoni yangu' ni lugha za kawaida za kisheria na kimahakama. Hukumu ni tafsiri ya sheria na tafsiri inatolewa na Jaji siyo sheria yenyewe. Sheria inatungwa na Bunge, tafsiri yake inatolewa na mahakama kwa maana ya Jaji baada ya kupata maoni pia ya mawakili.
 
Kibatala na wenzake ni weupe sana kwenye sheria
 
Amewaachia huru wazanzibar kwa kesi ya ugaidi,sasa analipiza kisasi kwa kufunga wanadam,huyu bibi wadharau.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…