Mahakama Kuu Divisheni ya Uhujumu Uchumi na Rushwa yatupilia mbali mapingamizi 2 kesi ndogo ya Mbowe na Wenzake. Jaji Siyani ajitoa kuendelea na kesi

Mahakama Kuu Divisheni ya Uhujumu Uchumi na Rushwa yatupilia mbali mapingamizi 2 kesi ndogo ya Mbowe na Wenzake. Jaji Siyani ajitoa kuendelea na kesi

..uamuzi mbaya zaidi ni pale Jaji aliposema kuwa maelezo ya Adamoo yalitolewa kwa hiyari.
Hii kesi kwenye hiyo mahakama naona imeisha kwa huu uamuzi wa kutengeneza wa leo ambao kimsingi umetolewa kama asante kwa mamlaka ya uteuzi kwa kumpa jaji cheo.

Mahakama ya rufaa chini ya majaji watatu ndio napopategemea, hawawezi kutoa hukumu kwa "maoni yao" kama alivyofanya Siyani.
 
Tenda haki. Amezungumzia pia muda uliotumika kumtafuta mtuhumiwa mwingine. Kutumia 'maneno maoni yangu' ni lugha za kawaida za kisheria na kimahakama. Hukumu ni tafsiri ya sheria na tafsiri inatolewa na Jaji siyo sheria yenyewe. Sheria inatungwa na Bunge, tafsiri yake inatolewa na mahakama kwa maana ya Jaji baada ya kupata maoni pia ya mawakili.
Jaji mwenyewe haijui haki, unamwambia nani mwingine atende haki? huyo mtuhumiwa mwingine alipatikana au hakupatikana?

Utaamuaje shauri kwa kutumia kitu/mtu kisichoonekana? Sheria sio hisia, siku zote inataka prove beyond any doubt.

Mtuhumiwa anaposema alitoa maelezo baada ya kuteswa, jaji angetakiwa kupata ripoti ya daktari kwa uthibitisho, lakini kuamua kukubali mtuhumiwa alitoa maelezo pekee bila kujali nini kilitangulia kabla ya maelezo yake ni kuinajisi mahakama.
 
Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, leo Jumatano Oktoba 20, 2021 inatarajiwa kutoa uamuzi katika kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu.
Haya. Aga gangi. Mungu mubariki Freeman.
 
Mbowe hafungwi, msitishane eti kwa sababu ya huo uamuzi mdogo

Hizo mbwembwe tu, sijaona jaji wa kumtia hatiani mbowe kwa makosa ya ugaidi
Nyie bavicha bhana!

Mwanzo mlikuwa mnashangilia zile porojo za wale mashahidi kwamba eti ushahidi unawavua nguo selikali?

Aisee
 
Jaji Kiongozi: ni sawa tunapaswa Kunaendele na Shahidi Lakini nikaomba nishauriane na Mawakili. Sasa Nimeona kwamba Shauri hili ni Moja ya Shauri linalopaswa kuisha kwa haraka.

Jaji: Kama Shauri likienda mfululizo ingechukua Miezi kama Minne

Jaji: Hivyo kwa Majukumu niliyonayo nimeona nijitoe aje Jaji mwingine haraka iwezekanavyo zekanavyo

Jaji ananyanyuka anaondoka Zake.
Sababu aliyoitoa wakati wa kujitoa ndiyo inapigilia msumari hoja ya kuwa serikali imeingilia kesi hii ili kuweza kupata matokeo wanayouataka wao.
 
Jaji mwenyewe haijui haki, unamwambia nani mwingine atende haki? huyo mtuhumiwa mwingine alipatikana au hakupatikana?

Utaamuaje shauri kwa kutumia kitu/mtu kisichoonekana? sheria sio hisia, siku zote inataka prove beyond any doubt.

Mtuhumiwa anaposema alitoa maelezo baada ya kuteswa, jaji angetakiwa kupata ripoti ya daktari kwa uthibitisho, lakini kuamua kukubali mtuhumiwa alitoa maelezo pekee bila kujali nini kilitangulia kabla ya maelezo yake ni kuinajisi mahakama.
Hii hukumu huyu jaji ameitoa kwa mujibu wa maoni yake yeye na wala siyo uhalisia wa ushahidi uliotolewa. Ameiandika kihuni huni mno!

Pia eti kwasbabu watuhumiwa walipitishwa pale central, basi yeye akaamini kuwa hawakupelekwa kituo kingine chochote kile na hapo central walitoa maelezo yao kwa hiyari kabisa.

Pia hakuchukulia maanani kuhusu makovu watuhumiwa waliyoyaonyesha mbele za mahakama.
 
jaji: Lilian pia kama Shahidi wa tatu ambaye ni Mke wa Adam Kasekwa alithibitisha kuwa alimuona Adam Kasekwa kuwa kateswa na kwa kuthibisha kwa makovu. ...Na alivyokuwa anatembea

Mimi sijaelewa hukumu ya Jaji Kiongozi huku anakubaliana mtuhumiwa kuteswa lakini Jaji Kiongozi anatupilia mbali na kukubali maelezo yaliyopatikana kwa njia ya kuteswa.
 
Mungu ni mwema wakati wote.

Sheria ni msumeno ndiposa Yesu akamwambia Pilato "....wewe usingekuwa na mamlaka juu yangu kama usingepewa kutoka juu"

Sheria na Siasa za Afrika ni Pasua Kichwa.
 
Si mlikuwa mnashangilia kama huu ushaidi unawavua nguo selikali?

..mambo yakienda vizuri upande wa mashtaka, ccm na polisi hushangilia.

..mambo yakienda vizuri upande wa utetezi, chadema hushangilia.

..ndicho kinachoendelea ktk kesi hii.
 
Wazee wa kuuliza PGO inasemaje wana buy time tu ili hukumu ichelewe inawezekana wanafanya yote haya kwa kujua kuna ukweli wa ushahidi wa diary na kama ipo kweli ikiletwa ndo msumari wa mwsho juu ya jeneza ataenda kunyolewa kipara Kama sabaya kimasiharamasihara.
 
Back
Top Bottom