Mahakama kuu imesema msanii Elizabeth Michael (Lulu) ana kesi ya kujibu

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Mahakama Kuu Dar leo imemkuta msanii wa filamu, Elizabeth Michael 'Lulu' na kesi ya kujibu baada ya mashahidi 4 wa Jamhuri kutoa ushahidi.

mwananchi

==========================================



Shahidi wa kesi ya kuua bila kukusudia inayomkabili Muigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’ Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Binadamu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dtk. Innosent Mosha ambaye ni shahidi wa nne wa kesi hiyo amesema kwamba baada ya kumpima
ubongo marehemu Kanumba waligundua kuwa umevimba.



Akitoa ushahidi huo leo mbele ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imeelezwa kuwa Daktari huyo aliletewa oda kutoka Jeshi la Polisi kwamba aufanyie uchunguzi mwili wa Steven Kanumba uliokuwa mochwari akishirikiana na daktari mwingine.

Dkt. Mosha amesema kwamba “Tulifungua ubongo wa Kanumba na kuukuta umevimba, mishipa midogomidogo ya ubongo ilikuwa imeingia damu, lakini kabla ya kufungua ubongo, kwenye kisogo kulikuwa na mgando wa damu" Dkt. Mosha.

Ameongeza kwamba “Baada ya kumaliza uchunguzi wetu tulipeleka sampuli kwa Mkemia Mkuu wa Serikali ambapo tulipeleka pia sampuli mbalimbali za viungo vya mwili wake,” amefafanua Dkt. Mosha.

Baada ya Mashahidi kutoa ushahidi wao Mahakama imesema kuwa Muigizaji Elizabeth Michael (Lulu) ana kesi ya kujibu dhidi ya tuhuma za kifo cha msanii Steven Kanumba , hivyo anatakiwa kujitetea


EATV
 

Attachments

  • Lulu2.jpg
    83.1 KB · Views: 547
watamsamehe tu, maana hata kama alitenda kosa, kipindi kile 2012 bado alikuwa minor(below 18 years)
 
dah huyu dogo napata hisia ambazo si nzuri kabisa, kosa la jinai hili
 
Ata Manji alikuwa na kesi ya kujibu halafu mwishoni katusua .... mi sion km kuna ushahid wa kumfunga huyo lulu taking the fact walikuwa wawili chumban na hakuna mtu wa kutoa ushahid direct kwamba alimuona akimuua Kanumba .... nadhan kwake ni simple tu ushahid wa daktari na ushahid wake yy mwenyewe unamnasua .... by the way sitegemei kuwa Lulu alimuua Kanumba
 
Ntoto ntamu kama Yule unadhani atafungwa hiyo itakua chakula ya jaji atamwachia
 
ni kawaida lazima kesi ingekuwepo coz yeye ndo alikuwa na marehemu chumbani
kujitetea kwake ndo pona yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…