Samcezar
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 13,095
- 22,731
Inaonesha una elimu ndogo juu ya maswala ya sheria mpenzi.Masikini Lulu. Wamsamehe tu.
Ningekuwa mimi ndo mama kanumba ningesamehe tu kwani hata akifungwa mwanae hawezi kurudi
Kiufupi ni hivi katika aina ya makosa, kuna makosa ambayo yameainishwa kama ya jinai na makosa yasiyo ya jinai kama ya madai.
Sasa hapa kosa la Elizabeth Michael linaangukia katika jinai. Kwa maana kuua, kuiba, kutukana, kujeruhi, kutishia kuuwa au kujeruhi, kupiga, kubaka ama kulawiti mtoto mdogo, kutembea na mwanafunzi, kubaka mwanamke au mwanaume, kuendesha gari bila leseni, kukwepa kodi, kutapeli mali ya mtu, kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu, matumizi mabaya ya ofisi za uma, kuendesha gari haijakatiwa bima, kuuza bima feki, na mengineyo mengi ni aina ya makosa ya jinai kwa tafasiri ya kwamba sheria imeyaweka wazi kuwa ni kinyume cha utaratibu wa nchi.
Hivyo basi unapofanya kosa lolote la jinai, anayekukamata ni askari na ndiye anayepeleka mashitaka( kukusemea) kwenye vyombo vya sheria( mahakama) na huko utakwenda kusomewa tuhuma dhidi yako na pale utakapokutwa na hatia na ushahidi dhidi yako kubaini unahusika moja kwa moja na mashitaka husika then hainaga mjadala hiyo ni unakutwa na adhabu ile iliyoainishwa kwa mujibu wa sheria.
Mama kanumba hata akimsamehe hawezi kufanya chochote katika kuzuia huyu binti asipatwe na adhabu pale akikutwa na hatia kwa maana ametenda jinai na ni yeye dhidi ya serikali si dhidi ya mama kanumba. Binadamu tunaongozwa na hisia ila sheria ndizo zinazoongoza mahusiano yetu hapa duniani.
Kwa mfano mimi nikikukuta wewe na mumeo mnagombana na mumeo anakupiga na kukujeruhi ninaweza kwenda kumchukulia polisi.....wakamshika na kumuweka mahabusu, akafunguliwa kesi ya kushambulia na kudhalilisha mwanamke, akahukumiwa muda usiopungua miezi sita na faini si chini ya laki tano. Basi tu huwa tunakaushiana