Mahakama kuu imesema msanii Elizabeth Michael (Lulu) ana kesi ya kujibu

Mahakama kuu imesema msanii Elizabeth Michael (Lulu) ana kesi ya kujibu

Ata Manji alikuwa na kesi ya kujibu halafu mwishoni katusua .... mi sion km kuna ushahid wa kumfunga huyo lulu taking the fact walikuwa wawili chumban na hakuna mtu wa kutoa ushahid direct kwamba alimuona akimuua Kanumba .... nadhan kwake ni simple tu ushahid wa daktari na ushahid wake yy mwenyewe unamnasua .... by the way sitegemei kuwa Lulu alimuua Kanumba
Circumstantial evidence itatumika halafu kuna kanuni moja ya kisheria inaitwa the last person to be seen with the deceased itakuwa invoked kwenye mazingira hayo. Pia kumbuka kuna ushahidi wa mdogo wake Kanumba anaitwa Bosco utamuimplicate vzr tu. Amesema Lulu walikuwa chumbani na Kanumba then akasikia some kind of commotion.
 
Inaonesha una elimu ndogo juu ya maswala ya sheria mpenzi.

Kiufupi ni hivi katika aina ya makosa, kuna makosa ambayo yameainishwa kama ya jinai na makosa yasiyo ya jinai kama ya madai.

Sasa hapa kosa la Elizabeth Michael linaangukia katika jinai. Kwa maana kuua, kuiba, kutukana, kujeruhi, kutishia kuuwa au kujeruhi, kupiga, kubaka ama kulawiti mtoto mdogo, kutembea na mwanafunzi, kubaka mwanamke au mwanaume, kuendesha gari bila leseni, kukwepa kodi, kutapeli mali ya mtu, kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu, matumizi mabaya ya ofisi za uma, kuendesha gari haijakatiwa bima, kuuza bima feki, na mengineyo mengi ni aina ya makosa ya jinai kwa tafasiri ya kwamba sheria imeyaweka wazi kuwa ni kinyume cha utaratibu wa nchi.

Hivyo basi unapofanya kosa lolote la jinai, anayekukamata ni askari na ndiye anayepeleka mashitaka( kukusemea) kwenye vyombo vya sheria( mahakama) na huko utakwenda kusomewa tuhuma dhidi yako na pale utakapokutwa na hatia na ushahidi dhidi yako kubaini unahusika moja kwa moja na mashitaka husika then hainaga mjadala hiyo ni unakutwa na adhabu ile iliyoainishwa kwa mujibu wa sheria.

Mama kanumba hata akimsamehe hawezi kufanya chochote katika kuzuia huyu binti asipatwe na adhabu pale akikutwa na hatia kwa maana ametenda jinai na ni yeye dhidi ya serikali si dhidi ya mama kanumba. Binadamu tunaongozwa na hisia ila sheria ndizo zinazoongoza mahusiano yetu hapa duniani.

Kwa mfano mimi nikikukuta wewe na mumeo mnagombana na mumeo anakupiga na kukujeruhi ninaweza kwenda kumchukulia polisi.....wakamshika na kumuweka mahabusu, akafunguliwa kesi ya kushambulia na kudhalilisha mwanamke, akahukumiwa muda usiopungua miezi sita na faini si chini ya laki tano. Basi tu huwa tunakaushiana
Bila shaka utakuwa ni learned brother mkuu.
 
Ila kwakutumia assumption tu, wanawake wa kaskazini mikono yao kuua ipo fasta sana. Ila Lulu mkimwangalia leo mtaona jinsi alivyodata. Yani kama hajaamini Dr atatoa ripoti ile.
 
Mpo wawili tu chumbani.mmoja akafa.Unategemea nani kamuua mwenzake??
Jihu simple ni wewe uliyekuwa naye.
Ataachiwa kama alikuwa chizi
Alikuwa under 18
Ama alikuwa anajihami.Let say angekuwa kavamiwa Na Jambazi Sasa kule ile kujidefend
Kuhusu kuwa under 18,Kuna ushahidi wa video yake mwenyewe akisema yeye ni.mkubwa Sasa ndo Mana amepeqa driving license. kwenye Birt part yake.
Hapo tuombe Muujiza tu.
But kama angeinvoke defense ya self defense angefanikiwa kdg hapo huwa ni partial defense na cyo full. Nadhani kwenye defense ataegemea kwenye suala la umri.
 
Utetezi wa Lulu. Kwa namna yoyote ile mimi sijasababisha kifo cha Kanumba,na mimi ndiye nilieshambuliwa na marehemu kutokana na umbile langu nilikuwa mdogo na alikuwa na uwezo wa kufanya chochote kwenye mwili wangu kwa sababu yeye ndo alikuwa na silaha
 
Sasa atajibu nini naliona gereza lile
Wangemwacha tu mtu mwenyewe kashajifia
Haya mapenzi kweli yanaua
 
Kafungwe tu,..mi natofautiana sana na wa tz weng wanafiki,hypocrites kabsaa,..hata kama ni miaka5,..kanumba was a great man.uskute kalimsukuma akajigonga ukutan,.kafungwe tu
 
Tatizo ni wakili Kibatala.. Kibatala jitoe kesi iishe
 
Watu wana uelewa mdogo sana.
Huenda kweli hawezi kumuua ila inawezekana katika kujilinfa akampiga Na.kitu kizito kwa nia ya kujiokoa.But unfortunately ukatokea kifo
But kesi IPO.Na kesi aina hii.ni kifungo cha maisha.
Ila angeua kwa makusudi ndo kesi yake ni kunyongwa.
Lulu kesi yake ni kuua bila kukusudia na adhabu yake nikifungo kisichozidi miaka 30 ila angeua kwa kukusudia ni kifungo cha maisha au kunyongwa! Hiyo ndo criminal law under Penal Code ya Tanzania!
 
Af haka katoto yaan hakana waswas,kanatikisa kichwa kanachat
 
justice is justice.. no one above the law.
let judges decide.
 
Kafungwe tu,..mi natofautiana sana na wa tz weng wanafiki,hypocrites kabsaa,..hata kama ni miaka5,..kanumba was a great man.uskute kalimsukuma akajigonga ukutan,.kafungwe tu
Sheria ifuatwe tu. Ila Wabongo wanafiki sana.
 
Alafu huyu dogo angejua kesi yake inaanza Lini angejibebea mimba tu. Hapo Najua muheshimiwa hakimu angeliangalia tumbo lake jicho la huruma lingemjia tu.
 
Masikini Lulu. Wamsamehe tu.
Ningekuwa mimi ndo mama kanumba ningesamehe tu kwani hata akifungwa mwanae hawezi kurudi

kesi ya kuua sio kama ya kuibiwa simu au kutukana mtu mama kanumba hana uwezo wa kusema kesi iishe
 
Ayaaa hii Kesi kumbe yaweza mfanya akaenda Segerea huyu mtt
Yaan ataenda kwa walivomkomalia na ushahidi wq kutosha mzuri tu......!!!!!atapata jibu la Dunia na Gunia vina tofauti ya herufi moja tu ya mwanzo[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Back
Top Bottom