Mahakama kuu imetoa hati kukamatwa Nabii na Mtume Josephati Mwingira

Wamkamate wasituambie wanamsaka! (najua kuna viji siasa vitaingia ktk issue hii subirini muone kama kuna cha maana.)

mi mwenyewe nasubiria hivyo visiasa maana siku hizi siasa ni dili kwa watanzania kuliko kitu kingine, mi binafsi hii kitu inaitwa siasa naichukia ile mbaya maana sio siasa tena bali ni mipasho tu
 
Well said NDUGU,barikiwa
 
Kama nabii nilitegemea afuate maneno ya KRISTO ''atakaye kukunyang'anya kanzu mpe na joho pia'' ama kweli YESU ana kazi sana endapo hata wale manabii wake hawafuati maneno yake!!! hususani ukiangalia na yale ya Mapinga!
Nanyi ndugu zangu mnaomtetea basi chagueni upande either wa Yesu au Mwingira lakini kwa elimu yangu ndogo ya dini naamini MWINGIRA yupo kwa maslahi yake na si ya YESU kwani Yesu havipendi vya dunia kama anavyovipenda MWINGIRA.
TAFAKARI
 

Na watu hawaachi through supernatural power wana pata kile wanachotarajia kwa kuchangia hicho kiasi, nawajua watu ambao wamefanikiwa kwa imani. Ninachoweza kusema kwa kupitia michango hii watu wengi wameweza kufikiwa na kupata faraja kwakuwa ndiyo vituo pekee vilivyobaki Afrika vinavyotoa “Counseling” au ushauri nasaha kwa lugha ya Kikwere kwa gharama nafuu. Ulya wana vituo ambavyo si vya kidini mbinu ni hizi hizi group therapy au individual therapy na watu wanalipia gharama kubwa sana aidha wao binafsi au kupitia bima za afya, si vema tukiwabeza watu hawa wana mchango mkubwa sana kwa jamii yetu
 

acha kudanganya watu ndugu yangu! kama ana document za umiliki kwa nini hakutoa notice? lile eneo lote ni mali ya shirika la serikali linaitwa mang'ula sema km vile lilishakufa so mwingira anataka kuchukua eneo kwa nguvu na vitisho! kuna kesi ipo mahakamani toka 2005 na mwingira anadai ana document za umiliki sasa kwa nini asizipeleke mahakamani kuthibitisha umiliki wake? anataka kutapeli ardhi na ameshawalisha sumu waumini wake hata uwambie nini hawasikii!
 

kanisa la mwenge ni mali ya waumini si mwingira peke yake nenda wizara ya mambo ya ndani watakuonyesha usajili wa kanisa. Kama kanisa lilinunua uwanja wa mwenge wewe ulitaka wauache kwa huyo mbabe afro plus amiliki kinyume na sheria? Ata YESU alipoana hekalu Yerusalemu limevamiwa na wahuni na wafanya biashara alitumia nguvu kuwatoa!!
 

hujiulizi kwa nini nabii wako na jeshi lake waliamua kubomoa hicho kiwanda usiku na so mchana kweupe? amka kutoka usingizini unadanganywa wewe!
 

mwambie mwingira akuonyeshe document za umiliki! akikuonyesha me najitoa jamii forums!
 

.
Haiwezekani kumpotezea mtu ambae kwa hakika unamwona akidanganya. Ndio maana neno la mungu limetutaka kuwatambua manabii wa uongo/makristo kwa matunda yao. Mwingira kumkimbia mke na kwenda kwa kimada ni jambo dogo? Kugombania mali hata kwa kuziharibu za wengine ndio wito alioitiwa? Lazima ndg ujifunze kutofautisha haki na dhulma, ni lazima uelewe Mungu sii kilele za midomoni na mazingaumbwe. Mungu ni adili na haki na anaweza kumtumia mlevi wa kulabuni kukusahihisha wewe unaejiona kuwa karibu nae kumbe uu mbali nae kuliko iwezavyo kudhaniwa. Kuna mengi kwa huyu Mwingira yanayoidhalilisha njia ya haki na kuhuzunisha sana Roho mtakatifu ambayo sina haja ya kuyaandika humu. Ni afadhali neema ya Mungu impitia ili aweze kutubu na kuirejelea njia ya haki kabla ya ile hukumu iliyo kuu.
Na siku zote ukiona mtu anaejiita mtumishi na silaha yake kubwa ni kutishia watu kupata matatizo ambayo Mungu atawapiga kwa kumfurahisha huyo mlalamishi, jua kwa hakika huyo sii Mungu muumba bali mmojawapo ya miungu ambayo ipo mingi. Watu wameisha farakana na kweli na wanaziabudu nyota za mbinguni na wala hawana habari. Wanaupokea ufunuo kwa vile viumbe vilivyoanguka toka kale. Kazi yao ni kupigana kimazingaumbwe tuu maana wapo katika ufalme uliofitinika. Wangesemaje kwa mtu kama Stefano ambae akijaa Roho mtakatifu aliwaombea msamaha wauaji waliomwua kwa mawe? Ingelikuwa ni wao wangelaani laana zote katika hazina ya baba yao mwovu. Ingelikuwa ni wao kwa kisa cha Abraham na Loti katika suala la mali wangethubutu kumwacha jarani yao ajichagulie kwanza? Hapana!! Ndio maana leo wanatafutwa na mamlaka kwa kosa la kupora mali kinguvu. Mungu warehemu!!
.
 

yaana wamiliki wote waliokuwa wapo pale kabla Mwingira alipowaondoa hawakujua hili wewe pamoja na Afro plus ndio wajuaji kuliko wale watu walikuwa wapo mwanzo . Wale wengine mbona walikubali kuondolewa na Mwingira pamoja na serikari kipindi hicho? Kama mmiliki ni Mangura hao Afro plus wamepata wapi umiliki wa pale? Acha longo longn mmiliki pale ni kanisa ndio maana unaliona lipo pale
 
...leo hii Josephat Mwingira kafunguliwa kesi nyingine Mahakama Kuu - D'salaam. Kesi hiyo imefunguliwa na kampuni ya mawakili ya Ngalo & Co. Advocates. Kesi iliyofunguliwa imepewa namba 6 ya 2012.
 
...leo hii Josephat Mwingira kafunguliwa kesi nyingine Mahakama Kuu - D'salaam. Kesi hiyo imefunguliwa na kampuni ya mawakili ya Ngalo & Co. Advocates. Kesi iliyofunguliwa imepewa namba 6 ya 2012.

kafanya nini?
 
Hivi leo ni tarehe ngapi tangu thread hii ianzishwe? Bado polisi wanamsaka tu? hwajamkamata!
 
Piga Tanganyika jeki peleka selo. Manabii wa uongo wapo kibao mtaani nje gozi ya kondoo ndani mbwa mwitu. Hata biblia ilisema watatokea wengi sana. Toka lini nabii akasakwa na polisi kama si utapeli.:hat:😛oa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…