Mahakama kuu imetoa hati kukamatwa Nabii na Mtume Josephati Mwingira

Mahakama kuu imetoa hati kukamatwa Nabii na Mtume Josephati Mwingira

Wamkamate wasituambie wanamsaka! (najua kuna viji siasa vitaingia ktk issue hii subirini muone kama kuna cha maana.)

mi mwenyewe nasubiria hivyo visiasa maana siku hizi siasa ni dili kwa watanzania kuliko kitu kingine, mi binafsi hii kitu inaitwa siasa naichukia ile mbaya maana sio siasa tena bali ni mipasho tu
 
Mwamakula, nafurahi unaanza kukunjua makucha yako polepole kutuonyesha wewe ni nani. Tumeambiwa sana @Zijaribuni kila roho" Roho wa Mungu hapingani na Mungu. Ukiona hayo yanatokea, basi aliye shambani abaki shambani na aliye darini asishuke, maana hata Ibilisi alikuwa mkuu wa malaika Mbinguni mwenye kuaminiwa sana. Alipoanza kujijengea kiburi hakupewa nafasi ya kujirekebisha hata ajapo tena Mwana wa Adam kwa mara ya pili.
Well said Ndugu,barikiwa!!!!

Lakini kweli mimi si wa Paulo wala wa Petro, ila nazungumzia habari za jiwe kuu la pembeni ambalo waashi walilikataa lakini kumbe ndilo linaloufanya msingi wa ujenzi kuwa imara zaidi. Ikifka mwisho wa siku wewe baki kwa Kakobe au Mwingira, lakini wale waliompokea ajaye kuhukumu dunia watanyakuliwa pamoja naye wala sio kupitia ukatoliki au upentekoste. Hizo ni dini za duniani tu, ambazo wakati mwingine ni chanzo cha vipato kwa walio wachache. Dini iliyo nzuri ni ile ambayo yawezekana hutapenda kuisikia ikitajwa, maana sio wote waendao makanisani wanakwenda kwa malengo yanayofanana. Ndio maana wengine hulala usingizi tangia kuanza kwa ibada hadi wakati wa kutoka nje, kisha huwasalimia wawapendao pamoja na kuwashika mikono wachungaji na mashehe na viongozi wa dini wawaone kwamba walihudhuria. Heri yao wanaojua kwa hakika wanamwamini nani na wakawa na msimamo wasiyumbishwe na mtu. Paulo alisema hata yeye alikuwa anapigana vita ili asije akawapeleka wengine Mbinguni na yeye akabaki. Rose Muhando anasema usiwe kama mpiga debe anayewaambia watu panda twende, kisha yeye anabaki palepale.

Simwamini Kakobe wala Mwingira wala binadamu yeyote awaye yote kwa habari ya kwenda mbinguni. Lakini naungana na yeyote anayeamini kama mimi ambaye tuinaweza kuongea lugha moja ya rohoni na kutiana moyo, maana kama binadamu, wote tumeoza pia, kutiana moyo ni agizo tangu enzi za manabii kabla ya kuzaliwa Yesu Kristo.
Well said NDUGU,barikiwa
 
Mwingira kabomoa mwenge kwa sababu uwanja ni mali ya efatha mwenge jamaa wa AFRO PLUS wanajua hilo sema walikuwa wanakomaa kwa sababu mapepo ndio wanafanya kazi nao.Mwingira ni mmiliki halali wa eneo lote hilo. Kama kaamua kuboa ni haki yake kwa sababu lipo kwenye umiliki wake.
Kama nabii nilitegemea afuate maneno ya KRISTO ''atakaye kukunyang'anya kanzu mpe na joho pia'' ama kweli YESU ana kazi sana endapo hata wale manabii wake hawafuati maneno yake!!! hususani ukiangalia na yale ya Mapinga!
Nanyi ndugu zangu mnaomtetea basi chagueni upande either wa Yesu au Mwingira lakini kwa elimu yangu ndogo ya dini naamini MWINGIRA yupo kwa maslahi yake na si ya YESU kwani Yesu havipendi vya dunia kama anavyovipenda MWINGIRA.
TAFAKARI
 
Nabii na mtume joe devi huyu pia ni mjasiriamali mzuri tu mf ukiwa pale kwenye centre yake kisongo viti vya mbele vinalipiwa sh 10000 vya nyuma 5000 then 2000 nk leso zenye sahihi yake sh 5000 kupeleka maombi binafsi israel 100000 na kuendelea naye pia tumwite nabii?

Na watu hawaachi through supernatural power wana pata kile wanachotarajia kwa kuchangia hicho kiasi, nawajua watu ambao wamefanikiwa kwa imani. Ninachoweza kusema kwa kupitia michango hii watu wengi wameweza kufikiwa na kupata faraja kwakuwa ndiyo vituo pekee vilivyobaki Afrika vinavyotoa “Counseling” au ushauri nasaha kwa lugha ya Kikwere kwa gharama nafuu. Ulya wana vituo ambavyo si vya kidini mbinu ni hizi hizi group therapy au individual therapy na watu wanalipia gharama kubwa sana aidha wao binafsi au kupitia bima za afya, si vema tukiwabeza watu hawa wana mchango mkubwa sana kwa jamii yetu
 
Mwingira kabomoa mwenge kwa sababu uwanja ni mali ya efatha mwenge jamaa wa AFRO PLUS wanajua hilo sema walikuwa wanakomaa kwa sababu mapepo ndio wanafanya kazi nao.Mwingira ni mmiliki halali wa eneo lote hilo. Kama kaamua kuboa ni haki yake kwa sababu lipo kwenye umiliki wake.

acha kudanganya watu ndugu yangu! kama ana document za umiliki kwa nini hakutoa notice? lile eneo lote ni mali ya shirika la serikali linaitwa mang'ula sema km vile lilishakufa so mwingira anataka kuchukua eneo kwa nguvu na vitisho! kuna kesi ipo mahakamani toka 2005 na mwingira anadai ana document za umiliki sasa kwa nini asizipeleke mahakamani kuthibitisha umiliki wake? anataka kutapeli ardhi na ameshawalisha sumu waumini wake hata uwambie nini hawasikii!
 
Kama nabii nilitegemea afuate maneno ya KRISTO ''atakaye kukunyang'anya kanzu mpe na joho pia'' ama kweli YESU ana kazi sana endapo hata wale manabii wake hawafuati maneno yake!!! hususani ukiangalia na yale ya Mapinga!
Nanyi ndugu zangu mnaomtetea basi chagueni upande either wa Yesu au Mwingira lakini kwa elimu yangu ndogo ya dini naamini MWINGIRA yupo kwa maslahi yake na si ya YESU kwani Yesu havipendi vya dunia kama anavyovipenda MWINGIRA.
TAFAKARI

kanisa la mwenge ni mali ya waumini si mwingira peke yake nenda wizara ya mambo ya ndani watakuonyesha usajili wa kanisa. Kama kanisa lilinunua uwanja wa mwenge wewe ulitaka wauache kwa huyo mbabe afro plus amiliki kinyume na sheria? Ata YESU alipoana hekalu Yerusalemu limevamiwa na wahuni na wafanya biashara alitumia nguvu kuwatoa!!
 
Mwingira kabomoa mwenge kwa sababu uwanja ni mali ya efatha mwenge jamaa wa AFRO PLUS wanajua hilo sema walikuwa wanakomaa kwa sababu mapepo ndio wanafanya kazi nao.Mwingira ni mmiliki halali wa eneo lote hilo. Kama kaamua kuboa ni haki yake kwa sababu lipo kwenye umiliki wake.

hujiulizi kwa nini nabii wako na jeshi lake waliamua kubomoa hicho kiwanda usiku na so mchana kweupe? amka kutoka usingizini unadanganywa wewe!
 
kanisa la mwenge ni mali ya waumini si mwingira peke yake nenda wizara ya mambo ya ndani watakuonyesha usajili wa kanisa. Kama kanisa lilinunua uwanja wa mwenge wewe ulitaka wauache kwa huyo mbabe afro plus amiliki kinyume na sheria? Ata YESU alipoana hekalu Yerusalemu limevamiwa na wahuni na wafanya biashara alitumia nguvu kuwatoa!!

mwambie mwingira akuonyeshe document za umiliki! akikuonyesha me najitoa jamii forums!
 
hahahaaa
Uzuri waumini wake tunajua kila kitu yaani historia yake na mambo yake yoote mpaka pale alipo, hakuna jipya utakalo sema wewe sisi tukawa hatulijui kusuhu Apostle & Prophet Josephat Elias Mwingira. Lakini pamoja na yote hayo, Mungu amuona yeye ana nafuu kuliko wewe.

ningekushauri usipende kuwaongelea vibaya watumishi wa Mungu (yeyote yule). Unajua ametumwa na nani wewe? Kwa sababu unaweza kujikuta una fight against him, who he stands for THE ALMIGHT GOD (MUNGU MKUU), na itakapofikia hapo sijui kama utabaki salama kibs.

Maana hata Yesu mwenyewe hakuja kwa ajili ya wema bali wenye dhambi ili wapate kutubu.
NAKUSHAURI UTUBU ili mungu akusamehe usije kufa na dhambi hiyo.

ukiona hukubaliani na mtumishi mpotezee tu. haitakupunguzia chochote.

Regards
G

.
Haiwezekani kumpotezea mtu ambae kwa hakika unamwona akidanganya. Ndio maana neno la mungu limetutaka kuwatambua manabii wa uongo/makristo kwa matunda yao. Mwingira kumkimbia mke na kwenda kwa kimada ni jambo dogo? Kugombania mali hata kwa kuziharibu za wengine ndio wito alioitiwa? Lazima ndg ujifunze kutofautisha haki na dhulma, ni lazima uelewe Mungu sii kilele za midomoni na mazingaumbwe. Mungu ni adili na haki na anaweza kumtumia mlevi wa kulabuni kukusahihisha wewe unaejiona kuwa karibu nae kumbe uu mbali nae kuliko iwezavyo kudhaniwa. Kuna mengi kwa huyu Mwingira yanayoidhalilisha njia ya haki na kuhuzunisha sana Roho mtakatifu ambayo sina haja ya kuyaandika humu. Ni afadhali neema ya Mungu impitia ili aweze kutubu na kuirejelea njia ya haki kabla ya ile hukumu iliyo kuu.
Na siku zote ukiona mtu anaejiita mtumishi na silaha yake kubwa ni kutishia watu kupata matatizo ambayo Mungu atawapiga kwa kumfurahisha huyo mlalamishi, jua kwa hakika huyo sii Mungu muumba bali mmojawapo ya miungu ambayo ipo mingi. Watu wameisha farakana na kweli na wanaziabudu nyota za mbinguni na wala hawana habari. Wanaupokea ufunuo kwa vile viumbe vilivyoanguka toka kale. Kazi yao ni kupigana kimazingaumbwe tuu maana wapo katika ufalme uliofitinika. Wangesemaje kwa mtu kama Stefano ambae akijaa Roho mtakatifu aliwaombea msamaha wauaji waliomwua kwa mawe? Ingelikuwa ni wao wangelaani laana zote katika hazina ya baba yao mwovu. Ingelikuwa ni wao kwa kisa cha Abraham na Loti katika suala la mali wangethubutu kumwacha jarani yao ajichagulie kwanza? Hapana!! Ndio maana leo wanatafutwa na mamlaka kwa kosa la kupora mali kinguvu. Mungu warehemu!!
.
 
acha kudanganya watu ndugu yangu! kama ana document za umiliki kwa nini hakutoa notice? lile eneo lote ni mali ya shirika la serikali linaitwa mang'ula sema km vile lilishakufa so mwingira anataka kuchukua eneo kwa nguvu na vitisho! kuna kesi ipo mahakamani toka 2005 na mwingira anadai ana document za umiliki sasa kwa nini asizipeleke mahakamani kuthibitisha umiliki wake? anataka kutapeli ardhi na ameshawalisha sumu waumini wake hata uwambie nini hawasikii!

yaana wamiliki wote waliokuwa wapo pale kabla Mwingira alipowaondoa hawakujua hili wewe pamoja na Afro plus ndio wajuaji kuliko wale watu walikuwa wapo mwanzo . Wale wengine mbona walikubali kuondolewa na Mwingira pamoja na serikari kipindi hicho? Kama mmiliki ni Mangura hao Afro plus wamepata wapi umiliki wa pale? Acha longo longn mmiliki pale ni kanisa ndio maana unaliona lipo pale
 
...leo hii Josephat Mwingira kafunguliwa kesi nyingine Mahakama Kuu - D'salaam. Kesi hiyo imefunguliwa na kampuni ya mawakili ya Ngalo & Co. Advocates. Kesi iliyofunguliwa imepewa namba 6 ya 2012.
 
...leo hii Josephat Mwingira kafunguliwa kesi nyingine Mahakama Kuu - D'salaam. Kesi hiyo imefunguliwa na kampuni ya mawakili ya Ngalo & Co. Advocates. Kesi iliyofunguliwa imepewa namba 6 ya 2012.

kafanya nini?
 
Hivi leo ni tarehe ngapi tangu thread hii ianzishwe? Bado polisi wanamsaka tu? hwajamkamata!
 
Piga Tanganyika jeki peleka selo. Manabii wa uongo wapo kibao mtaani nje gozi ya kondoo ndani mbwa mwitu. Hata biblia ilisema watatokea wengi sana. Toka lini nabii akasakwa na polisi kama si utapeli.:hat:😛oa
 
Back
Top Bottom