Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Mahakama Kuu imetupilia mbali pingamizi la awali Serikali dhidi ya maombi ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) ya kibali cha kufungua shauri la kupinga tozo kwenye miamala ya simu.
Hata hivyo wakati mahakama hiyo ikitupa pingamizi la Serikali, pia imeyatupa maombi kama hayo yaliyofunguliwa na Mwanaharakati Odero Charles Odero baada ya kukubaliana na hoja moja ya pingamizi la Serikali kuwa hati ya kiapo chake kilichokuwa kinaunga mkono maombi hayo ina kasoro za kisheria.
Uamuzi huo wa umetolewa leo Jumatano, Septemba 8,2021 na Jaji John Mgetta.
Akitoa uamuzi wa pingamizi la Serikali, Jaji Mgetta ametupilia mbali hoja zote tatu za Serikali akisema kuwa hazina mashiko.