Mahakama Kuu imewaruhusu Halima Mdee na wenzake 18 kufungua kesi ya kupinga CHADEMA kuwavua uanachama


Pascal yupo wapi atupe habari za nyongeza maana inaelekea anazo kwani anayajua sana haya mambo ya kina mdee 19
 

Watanzania tujiamini huwezi kuishi na kufikiri huta kuwa na maisha mazuri bila mshahara wa serikali wakati wewe una nguvu na elimu. Nashukuru Mungu sijawahi kuhonga wala kuchukuwa pesa yeyote ya seikali toka nimalize Form 6. Hii imenipa uhuru wa kuweza kusema chochote na kutokuwa tegemezi. Pamoja na hayo standard yangu ya maisha ni zaidi ya mbunge wa Tanzania.
 
Ilikuwa ni suala la muda tu,ila huwa pia najiuliza hawa kina dada wanajiamini kwasababu gani? Pia,why CDM kupitia wanasheria wao hawakufungua kesi ya kughushi nyaraka za Chama Kwa manufaa yao binafsi?..... anyway hii Dunia ndogo sana kuna siku ukweli utafahamika tu
 
Hao kovid si waachie tu. Usumbufu wote huu!?? Na wanajua hawahitajiki. Shame
 
Mahakama ni chombo cha mwisho cha utoaji haki na kutafsiri sheria

Kasome katiba
Nakushukuru sana kwa dhamira ya kunisaidia. Kwenye Katiba sioni sehemu inayozungumzia mipaka ya Mahakama. Hayo madaraka ya uamuzi wa haki, ni haki zote chini ya jua? Pia ungesaidia ungeelezea kama Katiba za nchi nyingine zime "address" suala hili kwa sababu Katiba yetu pia inaweza kuwa na mapungufu.



Sent from my ONEPLUS A5000 using JamiiForums mobile app
 
..Na mimi sio mwanasheria, ila nitaeleza kile ninachoelewa.

..Mahakama haiwezi kulazimisha kina Halima wawe wanachama wa Chadema.

..Inachoweza kuamua ktk mazingira haya ni kama Chadema ilizingatia katiba yake ktk kuwavua uanachama kina Halima.
Nakushukuru sana. Ina maana mahakama itaanua kama CDM ilifuata utaratibu wake ambao ilijiwekea na kama ilivunja sheria yo yote nyingine na si vinginevyo!?

Sent from my ONEPLUS A5000 using JamiiForums mobile app
 
Ujue wana mbwa wamewafuga ndani ya Chadema
 
Nakushukuru sana. Ina maana mahakama itaanua kama CDM ilifuata utaratibu wake ambao ilijiwekea na kama ilivunja sheria yo yote nyingine na si vinginevyo!?

Sent from my ONEPLUS A5000 using JamiiForums mobile app

..mahakama inaweza kusema wamefukuzwa kihalali.

..mahakama inaweza kusema hawajafukuzwa kihalali.

..mahakama HAIWEZI kusema Chadema isiwafukuze.
 
..mahakama inaweza kusema wamefukuzwa kihalali.

..mahakama inaweza kusema hawajafukuzwa kihalali.

..mahakama HAIWEZI kusema Chadema isiwafukuze.
Mahakama I naweza endesha kesi hadi 2025
 
Maushungi naye ovyo tu. Kama kuna anayemtegemea ameliwa
 
Mahakama I naweza endesha kesi hadi 2025

..kweli kesi inaweza kucheleweshwa mpaka 2025.

..kuna watu huenda mahakamani kwa malengo ya KUCHELEWESHA haki kupatikana, na sio kutafuta haki.

..yuko jamaa mmoja wa CUF alidhulumiwa ubunge wa jimbo la Mbagala kesi yake ilipigwa dana-dana mpaka kipindi cha ubunge kikaisha, na kesi ikakosa maana.
 
Mkuu kwani hujui mambo ya chadema?

Kwanza walikataa kutambua matokeo ya urais wakaaminisha wafuasi wao kwamba hawatateua wabunge wa viti maakumu.

Ila baadae kina Mbowe na Mnyika wakapeleka majina kinyemela ila wakawazuga wafuasi kwamba wamejiteua.

Na ukumbuke sain inayoenda kwa msajili na spika ni ya katibu tu siyo ya kamati nzima.
 
Waliondoka kina Slaa ma Zitto hakikufa ndio sembuse Hawa viti maalum ambavyo ni vya burebure?

Kama JPM na udikteta wote ule CHADEMA haikufa ndio sembuse kwa huyu Bibi?

Get serious
Mkuu kwa hiyo kufa kwa chama unataka mpaka kifutwe?
 
..Kamati Kuu haikuwateua.

..Mnyika amekana kutia saini nyaraka zozote.

..hiyo ina maana waliapishwa bila kuteuliwa na chama, na bila barua.
Unategemea Mnyika angekubali
 
Uanachama umeisha koma ndio maana wanafungua vikesi kujaribu kuukomboa. Kesi inakokwenda watatueleza vizuri uhalali wao unaanzia wapi. Amen
Nikikumbuka wale wabunge wa CUF walivyofurumishwa na Spika Ndugai huwa najiuliza haki iko wapi!. Akina mama Sofia Simba vs Bernard Membe (kachero mbobezi) walifukuzwa kana kwamba ni wanachama wachanga kwenye chama!.Hawa COVID - 19 wapo bungeni kwa uwakilishi wa chama kipi na wanakingiwa kifua kwa faida na maslahi ya Nani?.

Naamini na kuamini 2025 maamuzi ya wapiga kura yataheshimiwa kwa mbunge wanaemtaka ili kuepuka aibu hii inayoendelea katika nchi yetu. Tukubali kuwa siasa ni pamoja na kuwa na wabunge wa vyama shindani waliochaguliwa kihalali na maamuzi ya wananchi kuheshimiwa. Tunaogopa kukubali kuachana na COVID 19 kwa sababu tutabaki wenyewe na ivo maamuzi tutakayoyafanya yataonekana ya upande mmoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…