Mahakama Kuu: Kifungu kinachoruhusu kuficha mashahidi wa kesi ni batili na kinyume na Katiba

Mkuu ww ni mgeni wa nchi hii? Hiyo kuficha mashahidi wa siri Lisu alikataa akasema ni kinyume na katiba. Ila serekali ikashikilia kuwa ni sheria halali, na mahakama ikakubaliana na na mawakili wa serekali! Inshort kesi hasa za kisiasa nchi hii zinaendeshwa kwa maagizo toka juu, na sio sheria zinasema nini. Ingekuwa mahakama zinafuata sheria zitakavyo, Lisu leo asingekuwa mahakamani, maana ushahidi mkuu wa kesi alishaumaliza.
 
Nakubaliana na wewe 💯 lakini ili kufika kujua mahakama itasema nini ni lazima mawakili wa Lissu kesho wailete hiyo hukumu mahakamani tuone kina Jaji Ndunguru watasema nini.

Mahakamani Kila kitu ni lazima kiletwe kwanza mbele ya mahakama ndipo mijadala mingine itafuatia.
 
Majaji wamekuwa too lenient! Sheria yenye madhara haipaswi kupewa hata sekunde moja zaidi ya kuendelea kuumiza watu. Hicho kifungu ni haramu ab initio—kilipaswa kuwa severed immediately!
 
Mzee wa PPR, kuna tofauti kubwa kati ya what is na what should be!
 
Majaji wamekuwa too lenient! Sheria yenye madhara haipaswi kupewa hata sekunde moja zaidi ya kuendelea kuumiza watu. Hicho kifungu ni haramu ab initio—kilipaswa kuwa severed immediately!
Kilichonikera na majaji kina Ngunguru kukubali kujinyima fursa ya kuwa sehemu ya mhimili unaojitegemea.

Hebu fikiria kile kisanduku kilivyokuwa kabla ya Lissu kukilalamikia. Walikubalije hata wao kutokumuona shahidi?
 
Mahakama zetu ni Mahakama huru, hazifanyi kazi kwa maelekezo au kwa maagizo ya mtu yeyote!, sio mimi ninayesema haya ni katiba ya JMT ya mwaka 1977. "
Mahakama zipi hizo?

Katiba ipi hiyo unayoizungumzia ni ile iliyoitwa kijitabu?.

Ukweli unakubana moyoni na unajua fika 100% judiciary ya Tanzania ni subordinate wa executive na ulilijua vile vizuri siku umemuuliza Magufuli lile swali 2016 .


View: https://youtu.be/Ta0URHvUlko?si=l0OzuLzYZovayLZh
Magufuli alikujibu kabisa yeye kama head wa executive ni mhimili uliojichimbia , pensheni, mishahara , posho na ruhusa za safari kwa judiciary na vitu vingine anaweza kusitisha na wasimfanye chochote , katika nchi zenye mihimili huru asingethubutu kuongea vile maana asingepona kwenye mihimili huru siku ile ile judiciary wangechukua hatua ila kwa sababu sio huru na ukweli unaujua hata baada ya pale nini kilifuatia kwako ukiwa pia kama member wa judiciary.
 
Kilichonikera na majaji kina Ngunguru kukubali kujinyima fursa ya kuwa sehemu ya mhimili unaojitegemea.

Hebu fikiria kile kisanduku kilivyokuwa kabla ya Lissu kukilalamikia. Walikubalije hata wao kutokumuona shahidi?
kama tukishakubali ni kesi za maelekezo, nadhani hata majaji tunatakiwa tuwahurumie --- kutowahurumia majaji pia ni kuukataa uhalisia
 
Asante.
Na mawakili wa Lissu wakiileta hapo mahakamani hoja hiyo mawakili wa serikali si watapinga ili kuichelewesha zaidi kesi maana hilo ndo lengo lao kuu?
Mie naona maadam mashahidi wenyewe ni wa mchongo na Lissu kaonesha kuwamudu wao wakomae tu hivyo hivyo hadi mwisho wa kesi.
 
Haya mambo nimeyaandika sana

- Ili Mahakama Itende Haki: Mahakimu na Majaji waombe Kazi wasailiwe wenye Jicho la Haki ndio waajiriwe, Watazibaini kesi za Kubambikwa

- https://www.jamiiforums.com/posts/39541633/bookmark

- Katiba Yetu Ina Matobo: Serikali Ikikosea, Inashitakika. Je, Bunge na Mahakama Zinapowakosea Watanzania Kama Makosa Haya Tunawashitaki Wapi?

P
 
Sawa ...Nimekoshwa na uwepo wa Jaji CHUMA mie.Hana Mbwembwe nyingiiii..Aliwahi kumsimamia Kesi ya Madai Shemeji yangu Mmoja hapo Mwanza kwa gharama zake.Mwajiri-Tajiri na Mawakili wake,walitikiswa na wakatikisika.Hukumu ya kupiga Mali za Mwajiri iliposomwa.Waliomba poo.Wakaja home kuongea Kifamilia yaishe na yeye tukamshirikisha ,akasema basi sawa..Siku ya kupiga mnada mali waje tu na kile kiasi cha pesa kilichoamriwa na Mahakama wainunue wao.Ilikuwa Hoteli ,nikashuhudia Kwa mara ya kwanza,mfanyakzi wa Hoteli akimuuzia Hoteli mwenye Hoteli.
 
Hakukua na haja ya kuweka rejea nyingi , ukweli unaujua mahakama za Tanzania sio huru hata kwa 1% ni mateka wa executive.

Mkuu wa mhimili kupatikana kwa kuteuliwa na rais ambaye ni kada mwenzie wa CCM tayari mhimili huo unakua compromised.

Wakenya wana matatizo yao mengi tu ila mahakama zao ni huru hebu angalia hapa mchakato wa kumpata CJ unaongozwa na nani na unapitia hatua zipi hadi hatua ya mwisho ndio utajua mahakama zao kwanini zinaretain mamlaka .

Mchakato ni wa wazi , kwanza watu wataona tangazo la umma na linakuwa wazi maana nafasi hutangazwa kuwa ipo wazi baaada ya CJ kustaafu , wataangalia vigezo, watafanya maombi , watachujwa na mchujo kama unavyoona unaendeshwa live kwenye TV maana yake kila mtu anaona mwisho wa siku kamati hiyo ndio itampata mtu mmoja kwenda sasa kuthibitshwa na kuapishwa kuwa CJ.

Ila kwa Tanzania rais akiamka na jina lake mfukoni anaweza kumpa mtu u-CJ ndio maana hata hadi kipindi cha nyuma mtu aliyefariki jina lake lilitokea kwenye teuzi .


View: https://x.com/i/status/1382903636632727557
Ndio maana leo unaona ex-CJ kama Maraga na Willy Mutunga walisimama waziwazi kumkosoa Ruto kwenye mauaji ya Gen -Z June 2024 bila hofu sababu hawana wasiwasi wa kutishiwa kuondolewa viinua mgongo vyao au kutokuwepo katika "tume" ambazo kwa Tanzania ni dili kwa wastaafu.

Leo hii ex-CJ kama Chande anakubali kutumika kama toilet paper kusafisha uchafu wa October 29 sababu makahakama sio huru na hana cha kupinga akiitwa kwenye tume , Kenya rais haundi tume kihuni kama zinavyoundwa Tanzania na kugeuzwa kichaka cha kupiga pesa.
 
Ni jinsi gani Mahakama itakuwa moved ikiwa kuna kifungua cha miezi kumi na mbili kubadili hiyo Sheria na sio papo kwa papo kuwa Sheria hiyo ni batili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…