Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 59,804
- 134,593
Katiba ni kama Bible, kuisoma na kuielewa anahitaji upako fulani ambao mimi nimejaaliwa kuwa nao.Ni jinsi gani Mahakama itakuwa moved ikiwa kuna kifungua cha miezi kumi na mbili kubadili hiyo Sheria na sio papo kwa papo kuwa Sheria hiyo ni batili.
Kwa mujibu wa Katiba, Mahakama Kuu Tanzania ndio mamlaka halali ya kutafsiri Katiba, Sheria, taratibu na kanuni, lakini haifanyi jukumu hilo.
Kwa upako wangu wa kuijua dhamira mtunga katiba, mimi Pascal Mayalla, nasema anayebatilisha Sheria yoyote kwa kwenda kinyume cha katiba ni katiba yenyewe!, kazi ya Mahakama Kuu ni kuthibitisha tuu na kutamka kuwa Sheria fulani au kipengele fulani ni batili kinyume cha katiba, na sio kutengua, anayetengua Sheria batili kinyume na katiba ni katiba na sio Mahakama.
Hivyo tangu kutoka kwa hukumu ya Mahakama Kuu kuwa Sheria fulani ni batili kinyume cha katiba, hapo hapo, from there and then, Sheria hiyo inakuwa imetenguka!.
Kazi ya serikali na Bunge ni kufanya tuu process ya kuifuta from the books of laws.
Hivyo hata ile hukumu ya CJ kuhusu mgombea binafsi, CJ na full bench yake, wakikosea kuirudishia Bunge ile sheria batili eti kwa kuliheshimu Bunge, kwa vile ni Bunge ndilo lilitunga hiyo Sheria batili, Bunge ndilo lenyewe liutoe ubatili huo!, as a result mpaka leo, mpaka kesho, katiba yetu ina kipengele batili, hivyo ni katiba yetu sio katiba batili bali ni katiba batilifu!.
P