Uzalendo wa Kitanzania
JF-Expert Member
- Mar 8, 2020
- 3,585
- 8,106
Wadau hamjamboni nyote?
Taarifa kamili hapo chini:
Mahakama Kuu, Zanzibar imebatilisha kifungu cha 33(1) cha Sheria ya Kudhibiti Vileo (LCA) ya mwaka 2020 kinachoweka ukomo wa kampuni zinazoruhusiwa kuagiza vileo ikisema kinakinzana na Katiba ya Zanzibar.
Uamuzi huo umetolewa na Jaji George Kazi katika hukumu ya kesi ya kikatiba iliyofunguliwa mahakamani hapo na kampuni ya Quality Meat and Beverage Supplies (QMB), dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Kampuni hiyo ilifungua kesi baada ya kunyimwa leseni ya uagizaji vileo kutokana na masharti ya kifungu hicho, yanayoweka ukomo wa kampuni tatu tu zinazoruhusiwa.
Katika kesi hiyo ya kikatiba namba 01 ya mwaka 2023, pamoja na mambo mengine kampuni hiyo ilikuwa ikiiomba Mahakama itamke masharti ya kifungu cha 33 (1)(a)(b)(c)(d), (2) na (3) cha Sheria ya Vileo Sheria namba 9 ya mwaka 2020 inakinzana na Katiba. Pia iliomba mahakama izingatie kifungu cha 43(1) na (2)(a)(b)(c)(d)(e) cha Sheria ya Ushindani Sawa na Ulinzi Sawa kwa Mlaji (FCFCPA) namba 5 ya mwaka 2018.
Katika maombi mbadala, kampuni hiyo iliiomba Mahakama ikiipendeza ielekeze wale wote walioathirika na masharti ya sheria hiyo, wapewe nafuu za kisheria kwa mamlaka yake kabla ya kutungwa au kufanyika kwa marekebisho katika Sheria ya Vileo kuweka masharti ya usawa.
Jaji Kazi katika hukumu aliyoitoa Aprili 4, 2024 baada ya kusikiliza hoja za pande zote amekubaliana na hoja za kampuni hiyo na kuamua kuwa kifungu hicho cha Sheria ya Vileo hakipaswi kutumika na ni batili kisheria, hivyo hakitekelezeki.
MCL