Mahakama Kuu nchini Zanzibar yafuta kifungu kinachozuia uagizaji wa vileo

unadhani hakuna sheria ndogo za kulinda utamaduni?.
Wewe mkojani huna uchumi wala rasilimali zozote utautoa wapi utamaduni? Utafuata utamaduni wa anayekulisha...(mtalii).
 
Ni wakati wa kugonga Glassi hapa hapa Duniani Ahera yabaki Mahesabu tu.

Kunywa Kistaarabu.
 
640x640.jpg

Na hii ni kwa ajili ya wale Maustazi siku ya Eid baada ya pilau.
 
Wadau hamjamboni nyote?

Taarifa kamili hapo chini:

Mahakama Kuu, Zanzibar imebatilisha kifungu cha 33(1) cha Sheria ya Kudhibiti Vileo (LCA) ya mwaka 2020 kinachoweka ukomo wa kampuni zinazoruhusiwa kuagiza vileo ikisema kinakinzana na Katiba ya Zanzibar.

Uamuzi huo umetolewa na Jaji George Kazi katika hukumu ya kesi ya kikatiba iliyofunguliwa mahakamani hapo na kampuni ya Quality Meat and Beverage Supplies (QMB), dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Kampuni hiyo ilifungua kesi baada ya kunyimwa leseni ya uagizaji vileo kutokana na masharti ya kifungu hicho, yanayoweka ukomo wa kampuni tatu tu zinazoruhusiwa.

Katika kesi hiyo ya kikatiba namba 01 ya mwaka 2023, pamoja na mambo mengine kampuni hiyo ilikuwa ikiiomba Mahakama itamke masharti ya kifungu cha 33 (1)(a)(b)(c)(d), (2) na (3) cha Sheria ya Vileo Sheria namba 9 ya mwaka 2020 inakinzana na Katiba. Pia iliomba mahakama izingatie kifungu cha 43(1) na (2)(a)(b)(c)(d)(e) cha Sheria ya Ushindani Sawa na Ulinzi Sawa kwa Mlaji (FCFCPA) namba 5 ya mwaka 2018.

Katika maombi mbadala, kampuni hiyo iliiomba Mahakama ikiipendeza ielekeze wale wote walioathirika na masharti ya sheria hiyo, wapewe nafuu za kisheria kwa mamlaka yake kabla ya kutungwa au kufanyika kwa marekebisho katika Sheria ya Vileo kuweka masharti ya usawa.

Jaji Kazi katika hukumu aliyoitoa Aprili 4, 2024 baada ya kusikiliza hoja za pande zote amekubaliana na hoja za kampuni hiyo na kuamua kuwa kifungu hicho cha Sheria ya Vileo hakipaswi kutumika na ni batili kisheria, hivyo hakitekelezeki.
View attachment 2956858

MCL
Safi sana. Haki imeshinda. Sheria hiyo ilikua inaenda kinyume na katiba. Nilikua Zanzibar mwezi uliopita. Nilihangaika sana kupata Pombe ya kunywa baada ya masaa ya kazi. Nashukuru baadae nilipata Chimbo nikamwagilia moyo. Kazi na dawa. By the way, nilifurahi kuona Kitimoto ikiuzwa Zanzibar. Safi sana
 
Wadau hamjamboni nyote?

Taarifa kamili hapo chini:

Mahakama Kuu, Zanzibar imebatilisha kifungu cha 33(1) cha Sheria ya Kudhibiti Vileo (LCA) ya mwaka 2020 kinachoweka ukomo wa kampuni zinazoruhusiwa kuagiza vileo ikisema kinakinzana na Katiba ya Zanzibar.

Uamuzi huo umetolewa na Jaji George Kazi katika hukumu ya kesi ya kikatiba iliyofunguliwa mahakamani hapo na kampuni ya Quality Meat and Beverage Supplies (QMB), dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Kampuni hiyo ilifungua kesi baada ya kunyimwa leseni ya uagizaji vileo kutokana na masharti ya kifungu hicho, yanayoweka ukomo wa kampuni tatu tu zinazoruhusiwa.

Katika kesi hiyo ya kikatiba namba 01 ya mwaka 2023, pamoja na mambo mengine kampuni hiyo ilikuwa ikiiomba Mahakama itamke masharti ya kifungu cha 33 (1)(a)(b)(c)(d), (2) na (3) cha Sheria ya Vileo Sheria namba 9 ya mwaka 2020 inakinzana na Katiba. Pia iliomba mahakama izingatie kifungu cha 43(1) na (2)(a)(b)(c)(d)(e) cha Sheria ya Ushindani Sawa na Ulinzi Sawa kwa Mlaji (FCFCPA) namba 5 ya mwaka 2018.

Katika maombi mbadala, kampuni hiyo iliiomba Mahakama ikiipendeza ielekeze wale wote walioathirika na masharti ya sheria hiyo, wapewe nafuu za kisheria kwa mamlaka yake kabla ya kutungwa au kufanyika kwa marekebisho katika Sheria ya Vileo kuweka masharti ya usawa.

Jaji Kazi katika hukumu aliyoitoa Aprili 4, 2024 baada ya kusikiliza hoja za pande zote amekubaliana na hoja za kampuni hiyo na kuamua kuwa kifungu hicho cha Sheria ya Vileo hakipaswi kutumika na ni batili kisheria, hivyo hakitekelezeki.
View attachment 2956858

MCL

Zanzibar siyo nchi.
 
Taratibu wataruhusu vingi.
Hivi Ile kitimoto tunayokula tukiwa Zanzibar inafugiwa Zanzibar kule kule au Wana import kutoka Mbeya?
Wanafuga wenyewe wanadai kufuga siyo Dhambi!....dhambi kula
 
Mnaoshabikia kwamba mh. Simai kashinda how come awe yeye wkt kesi ilifunguliwa akiwa bado waziri?.

Lakini nini impact ya sheria hii kuwa wazi kuruhusu kampuni nyingine kuingiza vileo, unadhani hakuna sheria ndogo za kulinda utamaduni?.
Sheria za nini wakati wazanzibar wengi wanapenda hivyo vinywaji?
Sheria inaweza kuwepo, na bado vinywaji vikawepo kwa wingi zaidi huku serikali ikikosa mapato.
 
Back
Top Bottom