Mahakama Kuu Tanzania imeamuru Jamhuri kurudisha fedha za faini za kesi ya Freeman Mbowe na wenzake 7 wa CHADEMA

Hahahaaa siku zote haki itakulinda.....huyu mama naanza kumsoma sasa...tulichelewa kumpata..jiwe alikua anatufukia walah
Mkuu Mama yupo vizuri sana tena sana.

Apewe muda tu. Na ndio maana tunasisitiza kwamba mama aachwe afanye kazi na neema zitapatikana kwa kila mmoja wetu
 
Hii ndio namna pekee ya kuwafanya polisi was Tanzania kufanya kazi kwa kutumia vichwa vyao sio matumbo yao, kila watakapokuwa wanafanya madudu kama haya na mahakama kutenda haki na kisha serikali kulipishwa fidia watakoma uonevu.
 
Naweza nkapingana na wewe mkuu.

Huoni kama hili linadhihirisha kwamba kumbe anaehitajika ni kiongozi muadilifu tu?? Kupitia katiba hii hii mbona haki zinapatikana??

Najaribu tu kujenga hoja na wala sio kwamba napinga katiba mpya movement
Sio kwel, vp huyo kiongozi akifa au akitoka madarakani?, ila kikuwa na katiba bora kna kuwa na miongozo thabiti itayom-guide huyo kiongoz na co kufanya hisan km sasa
 
viongozi utawala wa magu walimuangusha ila sidhani kama ni yeye alipiga hizo hela ,
 
Namuunga mkono mama na ninamwombea mema milele
 
Kwanini ulikubali kuchangia (kama ulitoa mchango kweli)??
MasterP,

kukaa sero wakati unandugu wa kukuchangia ili utoke sero...! Wananchi tuliitika wito, na kwa heshima ya Mbowe, ki ukweli nilichangia, sasa zinaporudishwa tena, basi akumbuke kuturudishia tu basi...! siyo tena eti zikajenge ofis, inabidi atuulize tuliochanga tukubali, kwa mfano kama mimi, mimi ni CCM, Pesa yangu kwenda kujenga ofsi ya chama kingine, sikubali, lakini endapo Mtanzania yeyote akiwa kwenye mateso, nipo radhi kuchanga chochote ili atoke kwenye hayo mateso ila sio kuchangia chama
 
Kwahiyo ulichanga ya nini wakati ilikuwa hiari na watu walitoa kama msaada
Mkuu, nilichanga kumchangia Mtanzania mwenzangu ili atoke kwenye mateso hayo na si vingine, zinaporudi, pesa yangu sikubali ikajenge jengo la chama tena, hiyo hayakuwa malengo yangu
 
Kwani Mwendazake alikuwepo mahakamani wakati akina Mbowe na wenzake wanahukumiwa? Hakimu alikuwa ni Mwendazake?

Na leo hii hakimu ni Rais Samia?
Hukumu ilitolewa kwa kumwangalia kiranja mkuu..
Katika utawala ule waliibuka watesi na wakitaka kumrrifdhisha mkubwa.
Sasa walau haki inatamalaki. Angalia uchaguzi wababe walifanya watakavyo na hawakukemewa ili mradi waliibeba ccm. Ndivyo mkubwa alivyotaka na waovu walitumia nafasi hiyo kudhulumu.
Sasa tuna mtu mwema.
 
Tuliochanga kwa moyo mmoja kutokana na udhalimu wa yule mwovu, kwa moyo radhi kabisa, tunatamka kuwa pesa hiyo ni yao tuliowachangia. Ni kifuta machozi kwa mateso waliyopitia, na fursa walizozipoteza kwa kuwekwa ndani na yule mwovu shetani.
 
Hakika. Huyu ndio anafaa kuombewa sana ili atuvushe, maana anaupiga mwingi sana kuweka mambo sawa pale palipokuwa pamepinda
 
Aliyewahukumu kwa uonevu na kuchukua hela zao kafa.
Waliohukumiwa bado wanaishi na hela zao wanarudishiwa.

Damu ya binti yetu Akwilina isingeweza kupotea hivi hivi.

Kweli wahenga hawakukosea waliposema "He who pursues an innocent chicken often stumbles....and most likely collapses for keeps"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…