Jk alikua baba wa demokrasia. Alikua kiongozi mzuri mno.
Fahamu jk alkua mwanajeshi, angetaka kuongoza nchi kibabe angeweza tu, lakini alikua mpole na mcheshi mwenye kutaka Suluhu kwenye mambo Mengi.
Fahamu Katika uongozi wa JK mambo Mengi yalikuwa wazi, zile habari za escrow na Richmond Jakaya aliacha wananchi wazijue na wajue mambo yanayoendelea kwenye nchi yao, alkua na uwezo mkubwa sana wa kutumia ubabe kuficha zile taarifa. Mzee Kikwete alkubali kukosolewa, alkua mvumilivu mno. Aliruhusu freedom of speech.
Pamoja na uanajeshi wake aliongoza nchi kiraia, sijawahi muona kikwete kavaa magwanda ya kijeshi, au ENZI zake sikuwahi kumwona Dc akiwa amevaa magwanda ya mgambo. Nchi iliongozwa katika misingi ya kufata Sheria. Hakukua na matisho. Na akikaa pale magogoni DAIMA alkua anafkiria wananchi wake, siku zote alfikiria maisha Bora Kwa watu wake. Jakaya Kikwete alkua mwanaume na nusu.