Naam wanabodi,
Mnamo mwanzoni mwa Mwaka jana kuliibuka nenola kashfa ambalo ni KRA (Kisutu Revenue Authority) linalosemekana lilikuwa linaulenga mhimili wa 3. Ilikuwa ni kipindi ambacho kesi nyingi zilizopelekwa kwenye ofisi ya mhimili huu pale Kisutu kwa Mheshimiwa mmoja kwa jina la "Mh Simba" .
Ilifika pahala ikaonekana kuwa ni kama ofisi hiyo ilikuwa inatumiwa na Shujaa Mwendazake kama sehemu ya kukusanya fedha au kuwaumiza maadui zake kiuchumi na si kutoa haki.
Naam tumeshuhudia leo Kamanda wa anga na wenzake wakifutiwa makosa na kutakiwa kurejeshewa michango yao waliyolipa kwa control number kipindi hicho takriban 350m.
Leo hii tunaona kuwa kumbe ile ishu bado inawatafuna watu kama kina Kambole, Laikini la kujiuliza hapa ni Je kuzushwa kwa maneno hayo ambayo yanachukuliwa kama Kashfa kwa mhimili wa 3 limetokana na nini hasa?
Je ni vile wanademokrasia/wanaharakati kukosi imani na ofisi hiyo iliyokuwa chini ya Mh Simba?
Je ni wakati wa Mamlaka kuendelea kutafuta mchawi wa sakata hilo au kutibu majeraha yanayoonekana kusababishwa na ofisi hiyo ya pale jiarani na Maktaba?
Nimejaribu kufukunyua Machapisho mengi ya wanaharakati kuhusu Ofisi hiyo kama ilivyo hapo chini:
Chambua:
Mheshimiwa Thomas Simba anastahili kuwa Commissioner General wa KRA (kisutu revenue authority) kama itatungiwa sheria rasmi. Ameifanyia kwa mafanikio
064N:
Aliambia afanye kama mwanaFA Kunta akagoma, wakampeleka kisutu revenue authority
Mkulima wa ndizi:
Kumbe KIsutu Revenue Authority imezalisha zaidi ya Bilioni 73 kwenye ile issue ya uhujumu? Kumbe tunaweza kupata hata bilioni 100 kwa njia hii? Vipi inaweza kuwa official source of income?
#MATAGA
Jackson Mnyawami:
Katika kesi hiyo, Wakili Jebra Kambole anatuhumiwa kwa kuidharau mahakama kwa kuchapisha maudhui katika ukurasa wake wa Twita kuwa "Kisutu Revenue Authority (KRA)" kwa tafsiri isiyo rasmi ni "Mamlaka ya Mapato Kisutu"
Mengineyo
-Tuendelee kuchangia hiyo kisutu Revenue Authority (KRA) Tusichokee
-
Meko na Kisutu Revenue Authority yake wote wezi tu
-
Tunajenga standard geji sasa kwa fain za K. R. A(kisutu revenue authority)
-
30 ×4=120 40x4= 160 70x1=70 TOTAL 350M Kisutu Revenue Authority.
#KRA
-
Wafanye haraka kufungua account yaani tunaham sana tuchangie fasta tulipe huko Kisutu Revenue Authority
-Mda si mrefu tunakaribia kumalizana na KRA(kisutu revenue authority)jamani tuendelee kuonesha mshikamano wetu dhidi ya watesi wa haki zetu hii ndo nguvu ya umma wao si wana dola
-Meko siunatufanya sisi tunavunja vibubu vyetu na hela umeficha unakojua sisi tumamuachia mungu Tukamue tu maana umeona hupati kodi sasa unatumia kisutu kua njia yakupata pesa.Wapen kesi ingine maana upinzani ushakua mtaji wenu wakuvuna pesa Kisutu revenue authority
-
Muheshimiwa @MayorUbungo unatukosea watanzania Hawa hawajahukumiwa bali wamedhulumiwa uhuru na haki zao Mahakama ndiyo inayotoa hukumu na sio pale Kisutu Revenue Authority KRA.
Mimi nadhani ipo haja ya Mhimili wa tatu kujisafisha pale ofisi ya Kisutu, otherwise tuache kazi iendelee.