Pre GE2025 Mahakama Kuu yaagiza dhamana ya Dkt. Slaa ishughulikiwe haraka

Pre GE2025 Mahakama Kuu yaagiza dhamana ya Dkt. Slaa ishughulikiwe haraka

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Mahakama Kuu ya Tanzania, masijala kuu jijini Dar Es Salaam imegiza shauri la mwanasiasa Mkongwe Nchini Dkt. Wilbroad Slaa lirejeshwe katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa ajili ya kushughulikiwa kwa dhamana yake.

Dkt. Slaa na jopo la mawakili wake walifungua shauri la mapitio la kesi yake katika Mahakama Kuu akipinga mwenendo wa Mahakama ya Kisutu kuahirisha usikilizwaji wa suala la dhamana yake kutokana na maombi ya kupinga dhamana yake yaliyotolewa na Jamhuri.

IMG_0569.JPG
Jaji Arnold Kirekiano leo Januari 30, 2025 amesema kwa kuwa kesi ya msingi iko Mahakama ya Kisutu ambayo ina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo na kwa kuwa hoja ya uhalali wa mashtaka ilishatolewa Kisutu na inasikilizwa na kupangiwa uamuzi amesema si vyema Mahakama Kuu kuingilia kati. Hivyo Jaji Kirekiano ameelekeza Mahakama ya Kisutu itoe uamuzi ambao ilishauandaa.

Dkt. Slaa alikosa dhamana tangu alipopanda kizimbani Januari 10, 2025 kusomewa shitaka linalomkabili la kusambaza taarifa za uongo kupitia mtandao wa X.

IMG_0570.JPG

Soma, Pia:
 
Mahakama Kuu ya Tanzania jijini Dar Es Salaam imegiza shauri la mwanasiasa Mkongwe Nchini Dkt Wilbroad Slaa lirejeshwe katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa ajili ya kushughulikiwa kwa dhamana yake kwa haraka.

Huyu naye aache kuropoka ropoka hovyo. Ona sasa hao akina Maria Sarungi hata hawamsaidii😂😎
 
huyu babu atakuja kufia mahabusu yaani umri huo bado unashindana na wenye nguvu ? hayo matesoi anayoyapata anajipunguzia umri wa kuishi bure hela anayo ya kutosha kula vizuri huku akilea wajukuu sasa anachokitafuta sijui ni nini ana laana ya upadre huyu ndiyo maana hata mkewake alikuwa anamduda ma ngumi
 
Sasa angalia Upumbavu wa hiyo Mahakama ya kisutu.

Sheria ni ileile .

Mahakama kuu inaona ni haki ya Kupewa Dhamana.

Mpuuzi na Chawa wa Mahakama ya kisutu anaona sio Haki.

Yote Kwa yote, utashangaa kesho kutwa anateuliwa kua JAJI WA MAHAKAMA KUU.

hiyo ndo Tanzania Sasa
 
huyu babu atakuja kufia mahabusu yaani umri huo bado unashindana na wenye nguvu ? hayo matesoi anayoyapata anajipunguzia umri wa kuishi bure hela anayo ya kutosha kula vizuri huku akilea wajukuu sasa anachokitafuta sijui ni nini ana laana ya upadre huyu ndiyo maana hata mkewake alikuwa anamduda ma ngumi
Kila nafsi itaonja mauti.
 
Sio kila mtu anatafuta KULA tu, wengine wana causes za kufanya, wasira ndo anatafuta kula alipungukiwa ccm akaenda nccr kuna kipindi, akiona fursa anaitumbulia macho tu
 
Mahakama Kuu ya Tanzania jijini Dar Es Salaam imegiza shauri la mwanasiasa Mkongwe Nchini Dkt Wilbroad Slaa lirejeshwe katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa ajili ya kushughulikiwa kwa dhamana yake kwa haraka.

Hivi huyu mzee kawakosea nini? Kwani wakimpa dhamana atakimbia Nchi? Kwanini kumtesa kiasi hiki?
 
watanyooka tu si kwa maan misaada wanatumia wao tu
Walengwa wanafikishiwa kwa kiasi kidogo sn, nchi imejaa misafara tupu kuanzia DC/RC mpaka juu na sababu ya maana hakuna, teua hamisha tengua zote ni pesa za walipa kodi, utapata maendeleo saa ngapi? fedha zipo lakini nidhamu ya matumizi hakuna zaidi ya wizi
 
Back
Top Bottom