Mahakama kuu yaamuru serikali kusitisha zoezi la wanajeshi kwenda mtaani kuzuia maandamo

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Mahakama Kuu yaiamuru serikali kusitisha mara moja zoezi lake la kupeleka wanaeshi mtaani ili kutuliza maandano.

Hili limekuja baada ya Ikulu kutoa taarifa kuwa Rais Ruto amekataa kusaini Muswada wa Fedha na kuurudisha Bungeni.


Mahakama pia imeamuru Usalama wa Taifa Kenya pamoja na Polisi kuwaachia watu wote waliokamatwa kwenye maandamano haya bila masharti yoyote, na kama wamekatwa basi wapelekwe mahakani ndani ya masaa 24

====

Pia soma: LIVE - Yanayojiri Maandamano Kenya: Waandamanaji wafika Bungeni, wawili wauawa kwa risasi
 
Kenya hadi rahaa, wana support hadi ya mahakama kuu
Sisi huku tujaribu tuone polisi watakavyotunyofoa juujuu😂
Mkuu hata Kenya haikuja kirahisi. Ni kazi kubwa imefanyika. Nawaonea wivu kwa sababu nchi yao inaendeshwa kisomi na mihimili yote inafanya kazi. Unafikiria nchi ya Afrika rais aliye madarakani kushindwa kumuweka mtu wake kama Kenyatta alivyoshindwa ni rahisi. Na bado kabla ya hapo walishatengua matokeo ya urais.
 
Jeshi letu imara la JWTZ, makambi yote (mfano Makutopora, Ngerengere, nk), askari wangemwaga kila mtaa wa Kenya ili kufanya usafi asubuhi na kurejea mchana Dodoma kwa ajili ya lanchi.
 
Kenya hadi rahaa, wana support hadi ya mahakama kuu
Sisi huku tujaribu tuone polisi watakavyotunyofoa juujuu😂
Woga umewajaa baada ya waandamanaji kuchoma jengo lao la mahakama ya rufaa

Wanaogopa wasiwavamie kwenye makazi Yao

Waandamanaji wamevamia jengo la bunge na kuharibu na la mahakama wakaharibu

Mahakama ya Kenya imejaa woga wajinga wakubwa

Majaji wa Tanzania chukulieni huo uamuzi wa majaji Kenya kama uamuzi wa aibu usiozingatia taaluma Wala weledi Bali woga tu
 
Kajiongeza 2 hapo maana ingekuwa show kali
 
Kenya hadi rahaa, wana support hadi ya mahakama kuu
Sisi huku tujaribu tuone polisi watakavyotunyofoa juujuu😂
Kuna maiti zaidi ya 10 hiyo mahakama yenyewe imefika mahali imeona wasipoenda soft Ile vumbi itachafua Kenya wakose pa kuendeshea vx zao kmmk wanasiasa na hizo elite group huuma na kupuliza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…