Mahakama Kuu yamwachia huru George Sanga na Wenzake wawili, Kada wa CHADEMA walishikiliwa kwa miaka 5 gerezani kwa tuhuma za mauaji

Mahakama Kuu yamwachia huru George Sanga na Wenzake wawili, Kada wa CHADEMA walishikiliwa kwa miaka 5 gerezani kwa tuhuma za mauaji

Wewe mwongo mkibwa. Wakili wa chama, wakati watu tumechangishwa mara kadhaa kulipia gharama za mawakili!!

Msiwe mnaropoka vitu ambavho hamna uhakika navyo.
Kwamba Chadema ilimtelekeza Sanga Gerezani?

Wajomba fanyeni kampeni zenu lakini Mswalieni Mtume, kuna maisha baada ya Uchaguzi.

Halafu ni mgombea yupi wa Chadema ambaye hakuwa Chadema, ambaye unaweza kumuondoa kwenye lawama ikiwa George Sanga alitelekezwa Gerezani?
 
ndiyo mumwambie aache kuua watu safari nyingine anaozea jela
 
Ili haki ipatikane, lazima wananchi waelekeze nguvu zao kwa wahusika moja kwa moja (wakamataji, wapelelezi, waendesha mashitaka na mahakimu/majaji). Habari za CCM, serikali ni vichaka tu vya kujifichia waovu.
 
Huyu kijan na wenzake wanapaswa kuchangiwa pesa ili ziwasaidie kuanza upya maisha.

Miaka mitano si michache.

Sheria zetu hovyo Sana , mtu anakaa miaka mitano mahabusu?
 
Kwamba Chadema ilimtelekeza Sanga Gerezani?

Wajomba fanyeni kampeni zenu lakini Mswalieni Mtume, kuna maisha baada ya Uchaguzi.

Halafu ni mgombea yupi wa Chadema ambaye hakuwa Chadema, ambaye unaweza kumuondoa kwenye lawama ikiwa George Sanga alitelekezwa Gerezani?
Ujinga na mihemko iliyoko uku mitandaoni ndiyo inayoonyesha hali halisi za akili zetu zilivyo.watu wanajiropokea tu nakufwata mikumbo.no reason kabisa.alafu unawaona wanakwambia lissu ataleta mabadiliko wakati wao wenyewe hawana mabadiliko kwenye fikra zao.
 
Mahakama Kuu Kanda ya Iringa imewaachia huru wanachama watatu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA akiwemo aliyekuwa Katibu wa Jimbo George Sanga na wenzake Gudluck Mfuse na Octatus Mkwela kutokana na kutokutwa na hatia ya kuhusika na mauaji ya kada wa Chama cha Mapinduzi Emmanuel Mlelewa.

Akisoma hukumu hiyo kwa njia ya mtandao mkoani Njombe Jaji Mfawidhi Kanda ya Iringa Danstan Ndunguru amesema washtakiwa hao wameachiwa huru kutokana na upande wa jamhuri kushindwa kuthibitisha mashtaka yao.

Amesema ushahidi pekee uliotolewa na mashahidi hao ni wa kimazingira kwani hakuna ambaye ameona washtakiwa hao wakifanya kosa hilo mahakama kushindwa kujiridhisha kuwa washtakiwa hao wamefanya kosa.

"Ili uweze kuthibitisha ushahidi wa kimazingira lazima ujitosheleze lakini jamhuri imeshindwa kuthibitisha" amesema Ndunguru.

Amesema sababu nyingine iliyofanya washtakiwa hao kutokuwa na hatia ni baadhi ya mashahidi muhimu akiwemo mkuu wa upelelezi mkoa kushindwa kufika mahakamani.

Kwa upande wa mawakilii upande wa utetezi ukiongozwa na Dickson Matata na wenzake alisema kesi hiyo ilikuwa na mashahidi 14 upande wa jamhuri na 5 upande wa utetezi.

Amesema katika kesi hiyo namba 5236 ya mwaka 2024 kati ya mashahidi hao 14 hakuna hata mmoja aliyesema mahakamani kuwa amemuona mmoja kati ya washtakiwa hao akimuua Emmanuel Melwa.

"Kwenye kesi yetu hakuna mshtakiwa hapa aliyekiri... kwa kufuata utaratibu kukiri kuliozungumziwa mahakamani ni kwa shahidi polisi akiwa kwa RCO alimsikia George Sanga akikiri na kuwataja wenzake" amesema Matata.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Nyasa Joseph Mbilinyi ameitaka serikali kumaliza kesi iliyokuwa Kibaha kama ya George Sanga na wenzake na zote ambazo hata siyo wanachama wa chama hicho lakini wapo gerezani kwa sababu mbalimbali za kisiasa.

"Tunaitaka Serikali imalize kesi hizi kwasababu nchi yenye wafungwa wa kisiasa kwenye mipaka yake huwa haieshimiki duniani" amesema Mbilinyi.

Snapinsta.app_470948260_616481840825966_4259830395954127098_n_1080.jpg
 
Back
Top Bottom