Mahakama Kuu yatupilia mbali ombi la kibali cha kupeleka maombi ya kufanyia mapitio uhalali wa Makamu wa Rais, Dr. Mpango kuendelea kubaki madarakani

Mahakama Kuu yatupilia mbali ombi la kibali cha kupeleka maombi ya kufanyia mapitio uhalali wa Makamu wa Rais, Dr. Mpango kuendelea kubaki madarakani

Joined
Jun 26, 2024
Posts
16
Reaction score
16
Mahakama Kuu imetupilia mbali ombi la Wakili Tenzi Anthony Nyundulwa (Mleta Maombi) la kuomba kibali cha kupeleka maombi Mahakama Kuu kufanyia mapitio uhalali wa Makamu wa Rais, Dr. Philip Mpango kuendelea kubakia madarakani kufuatia taarifa za kuwasilisha barua ya kujiuzulu katika nafasi hiyo kwa Rais.

Ombi hilo lilifunguliwa chini ya Shauri la Madai namba 1948 ya mwaka 2025 katika Mahakama Kuu (Masjala Kuu) Dodoma na kutolewa maamuzi na Jaji Rumisha tarehe 7 Februari 2025.

Mleta maombi katika Shauri hilo alikua akipinga uhalali wa kitendo cha Rais Samia kupokea barua ya kujiuzulu kwa Dkt. Philip Mpango akijiuzulu nafasi yake ya makamu wa rais wa Tanzania na kumruhusu kuendelea kushikilia wadhifa huo kinyume na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 kama ilivyofanyiwa marekebisho.

Mleta maombi pia amepinga hatua za Dkt. Philip Mpango kuendelea kutenda kazi na kushikilia nafasi ya makamu wa rais wa Tanzania baada ya kuwasilisha barua yake ya kujiuzulu, kwa kuwa kujiuzulu kunakuwa halali pindi tu barua hiyo inapowasilishwa.

Katika Shauri hilo Mleta maombi alioomba Mahakama iridhie kutoa kibali kwa muombaji kuwasilisha maombi ya mapitio ya kimahakama kwa ajili ya amri zifuatazo:
  1. Mahakama itoe tamko rasmi kwamba Ofisi ya Makamu wa Rais iko wazi kwa mujibu wa ibara ndogo ya (2)(c) ya Ibara ya 50 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kufuatia kitendo cha Dkt. Mpango kuwasilisha barua ya kujiuzulu nafasi yake ya Makamu wa Rais kwa Mheshimiwa Rais Samia .
  2. Amri ya kumlazimisha Rais Samia kuteua mtu mwingine kushika nafasi hiyo kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (4) ya Ibara ya 50 na Ibara ya 48(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, kama ilivyorekebishwa.
  3. Amri ya kumzuia Dkt. Mpango, kuendelea kutekeleza majukumu ya Makamu wa Rais na kushikilia Ofisi ya Makamu wa Rais, kwani kujiuzulu kwake kulianza kutekelezwa mara tu baada ya kuwasilisha barua hiyo kwa Rais.
  4. Gharama za maombi.
Maombi haya yalisikilizwa kwa upande mmoja (ex-parte) na Mahakama baada ya kumsikiliza mleta maombi iliamua kutupilia mbali ombi hilo kwa sababu kwamba mleta maombi alishindwa kuithibitishia Mahakama kwamba kuna kesi na hoja za msingi za kubishaniwa.

Mahakama ilifikia uamuzi huo baada ya mleta maombi kutokuwasilisha barua ya Makamu wa Rais kujiuzulu katika nafasi yake hivyo kuiwia Mahakama ugumu wa kujua kama barua hiyo ilielezea kujiuzulu kwake kutaanza lini, kama kulianza siku barua ilipopokelewa au tarehe za mbeleni. Mahakama ilisema kutoa kibali kwa jambo hilo kufanyiwa mapitio ingekua imejielekeza vibaya kwa kuzingatia taarifa ambazo haziko katika rekodi za Mahakama wala za mleta maombi.

Mahakama pia ilisema kwa kuwa barua hiyo ni nyaraka ya Umma, mleta maombi angeweza kuipata na kuiambatanisha katika maombi yake kwa kuwa sio nyaraka ya siri, lakini hakufanya hivyo wala kueleza sababu za kutokufanya hivyo.

Kesi hii imeendelea kuacha maswali yasiyo na majibu kwa mleta maombi, Mahakama na Wananchi kwa ujumla kuhusiana na kilichoandikwa katika barua hiyo ya kujiuzulu iliyotangazwa kwa mara ya kwanza na Rais Samia katika Mkutano Mkuu Maalum CCM Taifa uliofanyika tarehe 19 Januari, 2025, Dodoma.
 

Attachments

Ilikua kesi ya msingi kabisa ila ndio hivyo tena!
Tuungojee wakati.
 
Bi Kizi mkazi kila kitu sio kutangaza.. washauri wake wa sheria na hotuba wampe tuition
 
Kuna siku Rais atatangaza kujiuzulu hadharani kwa kutaka sifa
 
Ikumbukwe mlalamikaji alishindwa kuleta barua ya makamo wa Rais kujiuzuluu.... mahakamani..
 
Back
Top Bottom