Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,267
Mahakama Kuu Jiji Dar es salaam leo Julai 2, 2021 imetupilia mbali ombi la kusimamisha mchakato wa uchaguzi mkuu wa viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) uliopangwa kufanyika Agosti 7, 2021 Jiji la Tanga
Jaji Edwin Kakolaki alifikia uamuzi huo baada ya kukataa ombi la "matengenezo ya hali ya sasa (Maintenance of status Quo)" ambayo iliwasilishwa na mawakili wa mwombaji Ally Saleh ambaye alikuwa mmoja wa wagombea nafasi ya Urais katika Shirikisho hilo.
Mawakili wanaomwakilisha mwombaji ni Frank Chacha, Nafikire Mwambona na Steven Mosha.
Jaji alikuwa amealikwa kutoa maagizo kusubiri uamuzi wa dai lingine la zuio la muda kufanya mchakato wa uchaguzi linalowakabili wadhamini waliosajiliwa na TFF, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi na TFF.
Wadaiwa hao wanawakilishwa na mawakili Alex Mushumbusi na Kennedy Alex ambapo kesi hiyo imepangwa kusikilizwa July 9, 2021.