Mahakama kuu yatupilia mbali ombi la kusimamisha mchakato wa uchaguzi wa viongozi wa TFF

Mahakama kuu yatupilia mbali ombi la kusimamisha mchakato wa uchaguzi wa viongozi wa TFF

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Mahakama Kuu Jiji Dar es salaam leo Julai 2, 2021 imetupilia mbali ombi la kusimamisha mchakato wa uchaguzi mkuu wa viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) uliopangwa kufanyika Agosti 7, 2021 Jiji la Tanga

Jaji Edwin Kakolaki alifikia uamuzi huo baada ya kukataa ombi la "matengenezo ya hali ya sasa (Maintenance of status Quo)" ambayo iliwasilishwa na mawakili wa mwombaji Ally Saleh ambaye alikuwa mmoja wa wagombea nafasi ya Urais katika Shirikisho hilo.

Mawakili wanaomwakilisha mwombaji ni Frank Chacha, Nafikire Mwambona na Steven Mosha.

Jaji alikuwa amealikwa kutoa maagizo kusubiri uamuzi wa dai lingine la zuio la muda kufanya mchakato wa uchaguzi linalowakabili wadhamini waliosajiliwa na TFF, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi na TFF.

Wadaiwa hao wanawakilishwa na mawakili Alex Mushumbusi na Kennedy Alex ambapo kesi hiyo imepangwa kusikilizwa July 9, 2021.
 
Hizo hoja zilikuwa dhaifu mno, Ally Saleh alikuwa anapoteza muda bure

Alichofanya Karia ni kuwapelekea mahakama Katiba ya TFF tu.

Yaani Karia anaupiga mwingi sana, wapinzani wa Karia wamepigwa nje ndani.
 
Ila Tanzania bhana! Yaani jitu limetokea zake huko Somaliland! Sikjui lilikuja nchini kama lihamiaji haramu!! Halina historia yoyote ile ya kucheza mpira hapa nchini, linatumia ujanja ujanja wa kujipitisha kwa wadau wa mpira kupitia chama cha majambazi (ccm)!

Leo eti linawaweka kando wenye mpira wao, akina Ali Mayay!!! Ili tu lipige hela za TFF.
 
Kama Kuna Sheria ya kukata Rufaa Ally Sareh akakate fasta,Kama mbwai iwe mbwai.
 
Mahakama Kuu Jiji Dar es salaam leo Julai 2, 2021 imetupilia mbali ombi la kusimamisha mchakato wa uchaguzi mkuu wa viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) uliopangwa kufanyika Agosti 7, 2021 Jiji la Tanga...
Kauli mbiu "Uhuru na Umoja" kiitikio "Nguvu yetu" Kisha tunarudia kinyume chake " Nguvu yetu" kiitikio "Uhuru na Umoja"

Tushirikiane kupush iwe slogan permanent ya taifa letu tafadhari tumshauri mama Samia aichukue hii kauli iwe salamu ya kudumu ya kitaifa. Nawasilisha
 
Haya mambo miaka yote huenda kwa mtindo huu, kesi mahakamani zinashindwa kwasababu ya kanuni walizojiwekea huko TFF, kwanza zile kanuni feki zifutwe ndio haki itapatikana, bila hivyo kwenda mahakamani ni kupoteza muda tu.
 
Ndo maana tunasema Karia hana kosa, Katiba ilikuwepo kabla ya Karia

Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF ndo wameweka hizi Kanuni.
 
Ila Tanzania bhana! Yaani jitu limetokea zake huko Somaliland! Sikjui lilikuja nchini kama lihamiaji haramu!! Halina historia yoyote ile ya kucheza mpira hapa nchini, linatumia ujanja ujanja wa kujipitisha kwa wadau wa mpira kupitia chama cha majambazi (ccm)!

Leo eti linawaweka kando wenye mpira wao, akina Ali Mayay!!! Ili tu lipige hela za TFF.
Kauli za kibaguzi tu hizi. Mbona amewashinda kwa hoja? Jibuni kwa hoja!!!
 
Kauli za kibaguzi tu hizi. Mbona amewashinda kwa hoja? Jibuni kwa hoja!!!
Kwani ni uongo siyo Msomali? Sasa inakuwaje mtu atoke zake Somalia huko, halafu aje awawekee vikwazo vya kipuuzi Wazawa na wachezaji walio lipambania hili Taifa katika medani za mpira wa miguu, kuliongoza Shirikisho lao?
 
MAHAKAMA Kuu jijini Dar es Salaam leo Julai 2 imetupilia mbali ombi la kusimamisha mchakato wa uchaguzi wa viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) uliopangwa kufanyika Agosti 7,2021.

Jaji Edwin Kakolaki alifikia uamuzi huo baada ya kukataa kutoa ombi la "kudumisha hali ya sasa" ambayo iliwasilishwa na mawakili wa mwombaji, Ally Salehe, ambaye alikuwa mmoja wa wagombea wa nafasi ya urais.

Mawakili wanaowakilisha mwombaji ni Frank Chacha, Nafikire Mwambona na Steven Mosha. Jaji alikuwa amealikwa kutoa maagizo kusubiri uamuzi wa dai jingine la zuio la muda kufanya mchakato wa uchaguzi linalowakabili Wadhamini walisajiliwa na TFF, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi na TFF.

Wadaiwa hao wanawakilishwa na Mawakili Alex Mushumbusi na Kennedy Alex. Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa Julai 9, 2021.

HABARILEO
 
Kwani ni uongo siyo Msomali? Sasa inakuwaje mtu atoke zake Somalia huko, halafu aje awawekee vikwazo vya kipuuzi Wazawa na wachezaji walio lipambania hili Taifa katika medani za mpira wa miguu, kuliongoza Shirikisho lao?

[emoji706][emoji706]
 
Unataka atoke Bukoba?

Si ndiye Malinzi huyu huyu aliwahi kushika nafasi hapo TFF na madudu yake hata hayasemeki?
Kwani ni uongo siyo Msomali? Sasa inakuwaje mtu atoke zake Somalia huko, halafu aje awawekee vikwazo vya kipuuzi Wazawa na wachezaji walio lipambania hili Taifa katika medani za mpira wa miguu, kuliongoza Shirikisho lao?
 
Kwani ni uongo siyo Msomali? Sasa inakuwaje mtu atoke zake Somalia huko, halafu aje awawekee vikwazo vya kipuuzi Wazawa na wachezaji walio lipambania hili Taifa katika medani za mpira wa miguu, kuliongoza Shirikisho lao?
Mbona hata wazazi wake wote wamezaliwa humu.tupe ushahidi km Karia ni muhamiji.
 
Back
Top Bottom